Sauti Ya Injili

Mchungaji Mpenzi Hukuita Uje; Katika Zizi Lake Panapo Salama;

Akina Wanawake, Waume Vijana, Yesu Aliye Kweli, Huwaita Kwake

 • Huita Kwa Moyo Wa Huruma, ‘Uluyepotea Uje Kwangu’;
 • Hivi Kukungoja Anadumu, Bwana Yesu Mchunga.

 

Akatoa Maisha Kwa Ajili Yetu; Ataka Wapotevu Waje Kwake Sasa;

Tusijihatirishe; Kwake Tu Salama;  Sikia Wito Wake, Mchungaji Wetu.

 

Tusikawie Tena, Adui Shetani,   Kama Mbwa Wa Mwitu, Atatuharibu;

Tunaitwa Na Yesu, Mkombozi Wetu,  Tuingie Zizini, Panapo Nafasi


 

Hitaji Kuu la Mwanadamu ni = “SAUTI YA INJILI”

 • (3: 23) = “Watu Wote Wametenda Dhambi Na Kupungukiwa Na Utukufu Wa Mungu”

Injili Ni Nini? = Gr. euangelion (INJILI) = “Habari Njema”

 • Katika (3: 23) = “Watu Wote Wametenda Dhambi Na Kupungukiwa Na Utukufu Wa Mungu”
 • Katika (6: 23a) = “Kwa Maana Mshahara Wa Dhambi Ni Mauti” (habari mbaya)
 • Katika (6: 23b) = “Lakini Zawadi Ya Mungu Ni Uzima Wa Milele Katika Kristo Yesu Bwana Wetu” (habari njema)

 

Habari Njema ya Nani? = “KRISTO YESU” (Angalia Warumi 1:1-6)

 1. Paulo, mtumwa wa KRISTO YESU, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa aihubiri INJILI YA MUNGU;
 2. Ambayo MUNGU amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika maandiko matakatifu;
 3. Yaani, HABARI ZA MWANAWE, aliyezaliwa katika ukoo wa Daudi kwa Jinsi Ya Mwili,
 4. Na kudhihirishwa kwa uweza kuwa MWANA WA MUNGU, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, kwa UFUFUO WA WAFU, YESU KRISTO Bwana Wetu;
 5. Ambaye KATIKA YEYE tulipokea Neema Na Utume ili mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya JINA LAKE;
 6. Ambao katika hao ninyi mmekuwa wateule wa YESU KRISTO;

 

Kwanini INJILI?

 • Watu wote ulimwenguni ( 3:10), bila kijali Rangi, Sura, Kimo, Jinsia, Uwezo, Imani, Elimu, Bara, Ukoo, Vyeo, nk.
 • Watu wote ni wenye dhambi (Warumi 5: 8) mbele za MUNGU aliye pekee MTAKATIFU (cf. 1 Samweli 2:2 )
 • Huyu MUNGU pia ni = HAKIMU WA HAKI (Zaburi 7:11; 2 Timotheo 4:8).

 

Swali? Ina maana gani kua yeye ni Hakimu wa Haki?

 • Atahukumu wanadamu wote kwa Haki, pasipo upendeleo.
 • Atahukumu waovu na kutoa adhabu ya uasi katika Jahanamu (Ufunuo 20: 11-15)
 • Kwa nini? = Kwa kukiuka Sheria Takatifu Yake ( 3:10).

 

Sikiliza ndugu Mpendwa Msomaji:

 • Tangu uasi wa Adamu na Hawa, shetani amewalaghai watu kua wanawezajipatia WOKOVU kwa njia zao wenyewe
 • Huu ni UONGO na cha kushangaza ni kua UONGO huu bado unasadikiwa na wengi hata Leo Hii (Karne ya 21)
 • YESU alionya haya katika (Mathayo 7:13-14)
  • (13) Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na NJIA NI PANA iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
  • (14) Bali mlango ni mwembamba, na NJIA IMESONGA iendayo uzimani, nao waionao ni wachache

 

Lakini Fundisho la Biblia ni wazi kuwa mwanadamu ana tatizo sugu la Dhambi na kamwe hawezi kujiokoa mwenyewe;

 • Hali ya mwanadamu ni hali ya kukatisha tamaa, na isiyo na Matumaini kabisa (Mathayo 19:25-26).
 • Yeye ni “mfu katika makosa [yake] na dhambi” (Waefeso 2:1);
 • Yeye ana “tabia ya asili” isiyoweza kupokea, kukubali, ama kuamini mambo ya  kiroho; “mambo ya Roho wa Mungu” (1 Kor 2:14.)

 

Kwa Nini? = Kwa sababu “mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo” (2 Cor.4:4; cf. Efe 4:18).

 

Zaidi sana wanadamu kwa Asilia wana sifa zifuatazo:

 • Ni Maadui wa Mungu (Warumi 5:10; Yakobo 4: 4);
 • Wanajitenga mbali na Mungu (Efe 2:19; Kol 1: 2. 1; Zab 58: 3);
 • Wao ni waasi kwake (Waefeso 2:. 2; Kol 3: 6; Tito 3: 3.; cf Ayubu 21:15);
 • Hawana elimu kuhusu Mungu (Zaburi10: 4; 14: 1; 53: 1; 2 Thes 1: 8.; Ayubu 8:13);
 • Wana uadui juu ya Mungu (Rum 8:7; Kol 1:20)
 • Wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu (2 Tim 3: 4);
 • Wanamchukia Mungu (Zab 81:15;. Rom 1:30);
 • Wanajisi, na wasiomcha Mungu (Zab 5:10; 1 Tim 1:9);
 • Wako chini ya ghadhabu ya Hasira yake (Yohana 3:36; Rum 1:18; Efe 5: 6).

 

Sikiliza = Mwanadamu wengi wako kwenye Njia Pana, Njia Ya Uharibifu, Njia Iendayo Upotevuni (Mathayo 7:13; Phil 3:19)

 • Kwa sababu hiyo hawapendi mwangaza wa ukweli wa kiroho (Yohana 3:20)
 • Na hivyo ni vipofu katika mambo ya MUNGU (Mathayo15:14).

 

Kama Watoto Wa Shetani (Mathayo 13:38; Yohana 8:44; Yohana 3:10),

 • Wanaishi chini ya utawala wake (Efe 2: 2),
 • Wao ni wajumbe wa utawala wake (Mathayo 12:26; Wakolosai 1:13)
 • Wao ni “kwa tabia yetu watoto wa hasira” (Efe 2:3)

 

Kwa Hivyo;

 • Wao ni watumwa wa dhambi (Yohana 8:34; Rum 6:17,20)
 • Wao ni “watumwa wa uharibifu” (2 Petro 2:19),
 • Wao ni ” vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu ” (Rum 9:22).

 

Kutokana na Sababu Hizo Hapo Juu,

 • Matendo Ya Sheria, Matendo mema, Jitihada za Binafsi za kujipatia wokovu, nk.
 • Kamwe haziwezi kutatua tatizo sugu la Mwanadamu = “KIFO”
 • KIFO = (Kifo cha Mwili; Kifo cha Kiroho; Kifo cha Milele)
 • DAWA PEKEE ya kuepuka KIFO ni kumruhusu Mungu afanye kazi Fulani ndani ya Moyo wa Mwanadamu Ili apate KUISHI.
 • DAWA PEKEE ni YESU KRISTO = Yeye ndiye Sauti Iokoayo, Sauti Iponyayo, Naam, “SAUTI YA INJILI” ( Waefeso 2: 8-9; 2 Tim 1:9; Tito 3:5).

 

(2 Kor. 5:17) Hata imekuwa, mtu akiwa NDANI YA KRISTO

 • Amekuwa Kiumbe Kipya = (Kuzaliwa Upya)
 • Ya Kale Yamepita =(badiliko ghafla la mwenendo wa maisha)
 • Tazama! Yamekuwa Mapya =(matokeo ya kuzaliwa upya)

 

Zamani sana yapata miaka mia saba (Kabla ya Masihi kuzaliwa), Nabii Isaya alitamka maneno yanayosikika hadi Leo.

Ni nani aliyesadiki habari tuliyoileta? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani? (Isaya 53:1)

 • Hii ni ripoti ya Upendo Mkuu, Neema, na Rehema ya MUNGU katika KRISTO YESU.
 • Hii ni ripoti ya Kristo Mwenyewe, Ofisi yake, Utii wake, Mateso yake, na Kifo chake pale Msalabani.
 • Hii ni ripoti ya Ukombozi unaopatikana kwa NJIA YAKE PEKEE, na kwa JINA LAKE tu .-
 • Ni ripoti nzuri sana kuhusu Uzima Wa Milele unaopatikana tu katika YESU KRISTO.

 

Swali Muhimu Kwako Leo Hii Mpendwa:

 • Je, unaamini ukweli wa Biblila kuhusu INJILI?
 • Je, ameamini “Habari Njema” au “Ripoti Hiyo” kuhusu KRISTO YESU?
 • Je, umemkubali huyu YESU kama Bwana na Mwokozi wako?
 • Je, unaamini kwamba Yeye ni Muumba, Mtegemeza, Mkombozi, na MUNGU pekee wa Kweli na Haki?
 • Je, unaamini kuwa alikuja duniani, akazaliwa kama mwanadamu, akaishi maisha ya unyeyekevu, makamilifu na ya Utii.
 • Je, unaamini kwamba aliteseka kwa ajili yako, akafa, akafufuka, na akapaa Mbinguni?
 • Je, unaamini kwamba yeye ndiye Njia Pekee, Daraja Pekee kati ya Mbingu na Dunia?
 • Je, unaamini kwamba Yeye ni Mtetezi wako?,
 • Je, unaamini kwamba Mlango wa Rehema utafungwa karibuni na Sauti itasikika ikisema “Imekwisha Kua”? = (Ufunuo 16:17)
 • Je, unaamini kwamba huyu YESU Anarudi Tena kwa ajili yako?

 

Sikia wito wa YESU kwako:

 • (Yohana 10:27) = Kondoo wangu husikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata;
 • ( 3:20) =Tazama, nasimama mlangoni,
  • NABISHA; =(NENO Lake, Sauti za Wahubiri, Waimbaji, Waandishi, Bible Study)
  • Mtu Akiisikia Sauti Yangu, = (Ambassadors of Christ) =Kuna Sauti Yaita kwa Upole.
  • Na Kuufungua Mlango,
  • Nitaingia Kwake, Nitakula Pamoja Naye, na Yeye Pamoja Nami.

 

 • (11:28) = Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na Wenye Kulemewa Na Mizigo, nami nitawapumzisha.