NEMBO YETU (Our Logo)
BIBLIA TAKATIFU: (Mwongozo Pekee)
- Hii huduma ya “Sauti Ya Injili’ ilianzishwa ili kufundisha watu Kweli zote za Biblia.
- Mtume Paulo akiandika anatunakumbusha akisema: (16) “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; (17) ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16)
- Mafundisho utakayo sikia humu yamejengwa katika Biblia Takatifu.
- Tunashauku yakutoa masomo/ mahubiri mbalimbali katika kila Sura, kila Kitabu cha Biblia – (yaani: Mwanzo hadi Ufunuo)
- Tunashauku pia ya kutoa masomo kulingana na mada mbalimbali katika Biblia – (angalia mpangilio uliowekwa katika ukurasa wa Nyumbani -“Home page”)
MSALABA WA YESU KRISTO = (“Sauti Ya Injili”).
- Neno “INJILI” ni “Habari Njema” za wokovu kwa njia ya Bwana na Mkombozi wetu YESU KRISTO.
- Msalaba wa Yesu ndio Ujumbe, Hoja, na Fundisho letu kuu.
- Msalaba ndiyo tegemeo pekee la Ulimwengu huu, ndiyo tumaini pekee kwa kila muumini.
- Mtume Paulo akiandika anasema: “Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa” (1 Wakorintho 2:2)
- Kristo Yesu ndiye Sauti pekee tunayopaswa kuisikia na kuzingatia.
- Kristo Yesu ndiye “Sauti Ya Injili”
TUFE: (Harakati za Injili Ulimwenguni kote)
- Tufe Linawakilisha Ulimwengu Mzima (cf. Mathayo 24:14)
- Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika Ulimwengu Wote, kuwa ushuhuda kwa Mataifa Yote; hapo ndipo ule mwisho Utakapokuja.
- Kristo Yesu anatukumbusha akisema: “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache.”
- Katika ulimwengu huu, bado kuna watu wengi ambao bado hawajapokea habari njema hizi za Injili.
- Ili kufanikisha zoezi hili Sauti ya Injili SDA inatumia njia mbalimbali ili kuwasilisha Injili hii, si kwa waswahili tu, lakini kwa watu wote ulimwenguni. Tunaomba maombi yenu kwani bado kuna upungufu mwingi ili kukamilisha hili zoezi. Bwana Atubariki Sote!
TARUMBETA: (Ujumbe wa Malaika Watatu)
- Tarumbeta zinatumika kupiga mbiu ili watu wote wasikie.
- Tarumbeta pia ni Ishara Ya Nyimbo = (NZK # 161) “Piga Panda Na Ya Makelele Yesu Yuaja Tena”
- Katika Agano la Kale Tarumbeta ziliandaa watu kuwa tayari kwa ajili ya Siku Kuu Ya Upatanisho = (The Day of the Atonement)
- Katika Agano Jipya, Ufunuo 14:6-12 Malaika Watatu wanaonekana wakipiga mbiu “kwa Sauti Kuu“ kuonya walimwengu wamrudie MUNGU wao, kwa nini? “Kwa Kua Saa Ya Hukumu Yake Imekwisha Kuja”
Ndugu mpendwa, historia ya Ulimwengu huu inafikia ukingoni, tukio kuu ambalo Ulimwengu huu utashuhudia ni MAREJEO YA BWANA NA MWOKOZI WETU YESU KRISTO. Lakini kabla ya Marejeo hayo, kuna Hukumu inayoendelea sasa.
Maandiko yanasema:
“Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.“ [Ufunuo 1:3]
“Tazama, Yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina.” [Ufunuo 1:7]
“Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.” [Ufunuo 22:7]
“12 Tazama, Naja upesi, na ujira Wangu u pamoja Nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo. 13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho. 14 Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” [Ufunuo 22:12-14]
Bwana Atubariki sote, tunapoendelea kuisikia “Sauti Yake”, naam, “Sauti Ya Injili” na kukata shauri sasa, kuitii sheria Yake, kujihoji nafsi zetu, kwa nini? “Kwa Kua Saa Ya Hukumu Yake Imekwisha Kuja”.
Amina.