KUHUSU SISI (About Us)
Sauti Ya Injili (TGVS) ni huduma ya Injili ya Kikristo iliyo na shauku ya kuwasilisha Neno la Mungu kote ulimwenguni.
- Sauti Ya Injili SDA ni moja kati ya huduma nyingi za kujitegemea zinazoweka msisitizo kwenye “BIBLIA TAKATIFU”
- SYI inaimarisha watu kiroho katika Njia Kuu Tano: Kampeni za Uinjilisti , Tepu za Injili (Mahubiri), Mikutano Mbalimbali Ya Injili, Mwendelezo wa Masomo mbalimbali katika Biblia, Mtandao, na kadhalika.
- Sauti Ya Injili SDA ni sehemu ya THE GOSPEL’S VOICE, Makao Makuu: Memphis, Tennessee, USA.
- Sauti Ya Injili SDA inalenga kuwasilisha Injili kwa waswahili wote popote pale ulimwenguni.
Dira Yetu: Kutoa masomo mbalimbali katika Biblia.
Dhamira yetu: Kuharakisha marejeo ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo kwa kuandaa na kufundisha watu Kweli Zote Za Biblia, ikiwemo Ujumbe Wa Malaika Watatu (Ufunuo 14:6-12)
Kaulimbiu Yetu: “Soma; Elewa; Shuhudia”
Misingi Ya Imani Yetu: Biblia Takatifu.
BWANA AKUBARIKI UNAPOENDELEA KUSIKIA INJILI HII.
Mambo Tunayofanya.
- Kwa bidii zote tunatafuta Kusoma, Kuelewa, na Kushirikisha wengine (kushuhudia) Neno la Mungu.
- Kufundisha kile tulichojifunza kwa wengine – (rejea ukurasa wa “Nyumbani” kwenye tovuti yetu)
- Huduma ya Maombi – (tunaomba kwa ajili ya mahitaji ya watu kila wiki)
- Kuandaa na kutoa Masomo Mbalimbali ya Biblia.
- Kumwimbia Bwana kwa “Zaburi Na Tenzi Na Nyimbo Za Rohoni”, (Efe 5:19)
- Kuandaa watu kwa ajili ya utayari wa marejeo ya Bwana na Mwokozi wetu, Yesu Kristo.