Kwa nini kuwe na Huduma hii ya Sauti Ya Injili?
Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote kama ushuhuda kwa mataifa yote, na ndipo ule mwisho utakapokuja.
• Injili lazima ihubiriwe ulimwenguni pote ndipo Yesu Atakuja Tena ( Matayo 24:14).
• Ulimwengu hauwezi kusikia Injili pasipo mhubiri (Warumi 10:14).
Katika (Warumi 10:17), mtume Paulo anasema “Imani huja kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Mungu”.
• Sauti ya Injili ipo ili kutoa mhubiri / wahubiri wa Injili.
• Sauti ya Injili ipo ili kuwaonya watu kuhusu hatari za kufuata “Injili Nyingine” (2 Wakorintho 11: 4),
• Sauti ya Injili ipo ili kuhubiri Ujumbe wa Malaika Watatu (Ufunuo 14: 6-13, Ufunuo 18: 1-4)
• Sauti ya Injili ipo ili kuhamasisha watu kiiimani kwa njia ya Neno la Mungu.
Katika (Mathayo 4: 4) Yesu anasema “Mtu Hataishi Kwa Mkate Tu, Ila Kwa Kila Neno Litokalo Katika Kinywa Cha Mungu”.
• Yesu ni Neno (Yohana 1: 1).
• Yesu anasema kwamba neno lake ni KWELI (Yohana 17:17), tena ni UZIMA (Yohana 6:63).
• Kumfahamu Yesu ni kuwa na UZIMA WA MILELE (Yohana 17: 3).
• Sauti ya Injili ya ipo kwa ajili ya kuwasaidia watu kumjua Yesu kupitia kurasa za Biblia Takatifu.
Ninawezaje Kushiriki?
• “SOMA” (Isome Biblia), “ELEWA” (Tafuta uelevu wa aya unayoisoma),”SHUHUDIA” (mwambia mwingine kuhusu Kristo Yesu)
• Gundua baadhi ya mahitaji ya huduma hii na jinsi gani unavyoweza kusaidia.
• Gundua uzuri wa YESU na Neno Lake kwa kusikiliza ujumbe huu mwenyewe.
• Toa msaada wako wa hali na mali ili kuboresha zaidi hii Huduma ya Injili.
• Soma ushuhuda wa watu kama wewe ambao wamekwisha barikiwa na Huduma hii.
• Tueleze jinsi huduma hii ilivyoleta badiliko fulani katika maisha yako.
• Mwambie jirani, rafiki, na familia yako kuhusu hii Huduma ya Injili.
Wchungaji; Wahubiri; Wainjilisti; Waimbaji
• Bado tunahitaji wahubiri wengi walio na shauku kama yetu, ili tufanye kazi hii pamoja.
• Kama Bwana anuzungumza nawe, Tafadhali toa Masomo yako ili tuyapakie (upload) Hapa.
• Tunahitaji pia Wahariri, Waandishi, Watafsiri; Wafadhili; na kadhalika.
Bwana akubariki ndugu msomaji/ msikilizaji katika kazi Yake njema.
• Mtuombee pia kila siku ili tufanikishe na kubariki wengi katika shughuli hii njema na takatifu, panapo nafasi.
• Kumbuka maneno ya Kristo: “Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache.”
• OMBI LETU: “Ee Mwokozi Yesu, tufanye kuwa sehemu ya watendakazi Wako waaminifu”Katika Jina la Yesu Kristo, Amina!
KARIBUNI SANA WAPENDWA, BWANA ATUBARIKI SOTE.