Huduma Zingine

INJILI KATIKA  Facebook/ Whats App 

KARIBUNI SANA WAPENDWA

Sauti Ya Injili (TGV Swahili) ni huduma ya Injili ya Kikristo iliyo na shauku ya kuwasilisha neno la Mungu kote ulimwenguni.

SYI inaimarisha watu kiroho katika Njia Kuu Tano:
➡Kampeni za Uinjilisti ,
➡Tepu za Injili (Mahubiri),
➡Mikutano Mbalimbali Ya Injili,
➡Nyimbo za Injili,
➡Mtandao, na kadhalika.

TGVS ni sehemu ya THE GOSPEL’S VOICE (www.thegospelsvoice.org)

DIRA YETU.
➡Kutoa masomo mbalimbali ya Biblia.

DHAMIRA YETU.
➡Kuharakisha marejeo ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo kwa kuandaa na kufundisha watu Kweli Zote Za Biblia, ikiwemo Ujumbe Wa Malaika Watatu (Ufunuo 14:6-12)

KAULIMBIU YETU.
➡”Soma; Elewa; Shuhudia”

📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖📖

UNGANA NASI KWA AJILI YA MAOMBI
• Kila Siku Alfajiri: Angalia “Chumba cha Maombi.”
• Siku 100 za Maombi, March 27 – July 4.
• Ombea jirani yako: changamoto mbalimbali zinazowasibu
• Ombea nafsi yako: utubu, uokolewe, uingie mbinguni
• Ombea viongozi wa serikali: Hekima, Amani, Vibali vya mikutano ya Injili; n.k.
• Ombea viongozi wetu wa kanisa: “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache” (Luka 10:2)
• Ombea huduma hii—(Bado tuna kazi kubwa sana ya kuandaa Masomo).
• Ombea mchakato wa Injili Ulimwenguni kote (Matayo 28:19-20)
• Ombea mtu mmoja atakayesikia kweli hizi za Biblia akapate kuokolewa.
• Jiandae kukutana na Mungu Wako. “Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli”; (Amosi 4:12).