Imani na Uponyaji

Mwalimu: Tajieli Panga (Audio)

4/22/2016 (Muhtasari)

Soma Ellen G. White “Thou Canst Make Me Clean,” uk. 262-271, katika The Desire of Ages.

Wajerumani wana msemo, “Einmal ist keinmal” Kwa maana ya moja kwamoja ni “Mara moja sio cho chote” Ni msemo wa kinahau kwa wazo kwamba kama kitu kitatokea mara moja pekee, basi hakina maana kabisa. Kama ikitokea mara moja tu, huenda kisingetokea kamwe. Kama unakubali au hapana, fikiria wazo hili katika muktadha wa somo la Alhamisi, pale Yesu alipomwambia mtu yule aliyetaka kwenda kumzika baba yake na kisha awe mwanafunzi “Nifuate, waache wafu wazike wafu wao” (Mathayo 8:22).

Yesu alimaanisha nini kwa kudokeza kwamba mtu yule, mtu aliye hai, alikuwa amekufa? Vema, kama “Einmal ist keinmal,” iwapo mara moja si cho chote, basi kuishi katika dunia hii mara moja tu, bila umilele unaofuatia, ni sawa sawa na kama kamwe hukuzaliwa kabisa. Hata ukifa sasa ni sawa tu (tazama Yohana 3:18) Watu wenye akili wa dunia, ambao hawaamini kuhusu maisha baada ya kifo, wamelalamika kuhusu kutokuwa na maana kwa maisha ambayo yanakuwapo hapa mara moja tu, kabla ya kutawanyika milele. Yumkini hii inaweza kuwa na maana gani, wameuliza, iwapo baada ya muda huu mfupi tunaondoka milele na kusahaulika milele? Si kitu cha kushangaza, basi, kwamba Yesu alisema kile alichokisema. Alikuwa anataka kumwelekeza mtu yule kwenye hali halisi iliyo kuu kuliko ile ambayo dunia hii ndani yake na kwa yenyewe, inatoa.


Maswali ya Kujadili:

1. Kutokana na wazo liliyowasilishwa hapo juu, rejea na usome kisa katika kitabu cha Mathayo pale Yesu alipomwambia mtu yule kile alichosema kuhusu kumzika baba yake. Hii inapaswa kutuambia nini kuhusu jinsi gani ni muhimu kuwa na mtazamo mpna (na tunaposema ‘mpana’ tunamaanisha mpana hasa) akilini katika yote tuyafanyayo? Ni kwa jinsi gani teolojia yetu inatusaidia kuelewa jinsi ambavyo hasa mtazamo huu ni mpana?
2. Siku zote hatujui mapenzi ya Mungu katika uponyaji wa kimwili, lakini daima tunajua mapenzi yake kwa uponyaji wa kiroho. Ni kwa jinsi gani hii inapaswa kuathiri maisha yako ya maombi?
3. Ni vitu gani muhimu zaidi ya vyote kwako? Tengeneza orodha na uilete orodha hiyo katika darasa. Unawezaje kujifunza nini kutokana na vipaumbele vya kila mmoja wenu? Vipaumbele vyetu vinatufundisha nini kuhusu sisi wenyewe na kuhusu jinsi ambavyo mitazamo yetu ya dunia, ya Mungu, na ya kila mmoja wetu? Je orodha hiyo ingetofautianaje kama kundi la wasioamini uwapo wa Mungu wangefanya zoezi hilo hilo?

Michango na Maswali

Katika somo la juma hili tumejifunza mambo mengi kuhusu huduma za Yesu alipokuwa hapa duniani.

Kikubwa zaidi ni habari ya UPONYAJI NA UTAKASAJI….

Yesu aliponya watu kiroho na kimwili pia. Aliwatakasa na kuwasamehe dhambi zao. Alikuwa na mamlaka ya pekee sana katika huduma alizozifanya. Uwezo wake hutuwezi kulinganisha na chochote. Yeye ni yote katika vyote.

Tajieli Panga: Swali la tatu ni changamoto sana…

 • Tukisema tuorodheshe nini unataka kwwli kwenye hyo list wengi tungeandka vipaumbele vya mambo ya dunia na isingetofautiana na ya wale ambao hawajamfaham Mungu bado…
 • Tunapaswa kua tofaut hilo ndo lengo la swali maisha yetu, vipaumbele vyetu vinapaswa kua tofaut na pia vyenye mvuto hata kwa wwngne ambao wanapotuona basi wavutwe na kujifunza juu ya Mungu mkuu kupitia kwetu.

Je ni mambo gani tumeyapa vipaumbele??

 • ➡Family
  ➡Ajira,
  ➡Mipango yetu ya mbeleni, nk.

Tajieli Panga: “Kuishi Maramoja tu na kukosa uzima wa milele ni Sawa na kama vile hukuwahi kuishi….”

 • hili nalo limenishangaza.
 • Ni kweli watu wasimjua Mungu hawaoni maana ya maisha….ikiwa kama watakufa watapotea milele zote.
 • Hii ikanikumbusha usemi huu uliozoeleka Duniani…:”we only live once, make the most of it”
 • Lakini kwa sisi tuliona tumaini tunaona maana ya maisha…katika dunia hii na hata ile mpya.

Tajieli Panga: Tuombe

 • Baba wa mbinguni… Ni wakati mwingine tunakuja mbele zako.
 • Tupe mbinu ya kuliishi neno lako. Tusaidie sana.
 • Tupatie na mibaraka yako.
 • Naimani yote utayutendea kwa kadiri ya mapenzi yako.
 • Usiku wa Leo ukawe nasi na utupe amani yako pia.
 • Kipindi kinachofuata cha maombi, uwe nasi kwa jina la Yesu. Amen

Isaac Patrick: Kama hatuwezi kutimiza kanuni za utunzaji wa kweli wa Sabato, basi Mungu ni mwongo au katili kwa kuwa ndiye aliyeamuru na kuiandika kwa chanda Chake mwenyewe

Kutoka 31:18 Hapo BWANA alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

 • Lakini tunajua kuwa Mungu wetu ni mwenye upendo, rehema na fadhili.
 • Yeye ni “Mungu si mtu, aseme uongo”
 • Hesabu 23:19 Mungu si mtu, aseme uongo;Wala si mwanadamu, ajute.
 • Tena Hana kigeugeu Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
 • Na kwamba Yesu Kristo ni Yeye yule Waebrania 13: 8 Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele.

Aliposema “Ikumbuke siku ya Sabato itakase” alisema pia “ni agano la milele.”

 • Wazo la kwamba madai ya kutunza Sabato ni mazito na hayawezekani, kwa kweli, hayapatani kamwe na fundisho la Biblia.
 • Aliyeitoa sheria hii alisema!  1 Yohana 5:3 wala amri Zake si nzito.

Lesoni 2-2026

Leave a Reply

Your email address will not be published.