4/22/2016

MAOMBI YA ASUBUHI (Ijumaa ya 4/22/16)

 1. Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
 2. Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia ya Sauti Ya Injili)
 3. Mada Ya Leo = KAZI YA INJILI HAPA KTK SAUTI YA INJILI

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:

 1. Baraka tele & uaminifu wake kwetu
 2. Tabia yake isiyobadilika
 3. Msamaha wa dhambi zetu
 4. Nafasi nyingine ya Uhai Leo.

WAGONJWA WETU

 1. Sisi sote tu wagonjwa wa kiroho, hivyo tuombee ili Tabibu Mkuu atuponye
 2. Mama yake Barbara – ana maumivu makali sana ya mguuni yapata sasa miaka 25.
 3. Dada Tatu Mkomagi.
 4. Dada Mercy Swai
 5. Rafiki yake Sule Mwassy (Mable) amepata depression, amezimia akakimbizwa Hospitali.
 6. Andrew Songa, anaumwa sana, na amekimbizwa Hospitalini.
 7. Debora & Mwanae
 8. A.B.M,Mwanza-TZ. (dada yangu: anaumwa sana. Tumwombee)
 9. A.B.M,Mwanza-TZ. (mama amekua akihudhuria cliniki: HTN & PUD, at BMC, sasa anasumbuliwa na CHF, Congestive Heart Failure.

MAHITAJI & CHANGAMOTO ZINGINE

 • Mkutano mkubwa wa injili, BUNDA Mjini, Tanzania.
 • Mwenye -diploma ya “procurement and supply management” lakini hajapata ajira.
 • George anataka 100 USD by 25th April ili kuhudhuria program ya kuuza vitabu huko Norway
 • Advocate Kinja = “nipo kwenye partnership ya kufungua campuni, lakini bado mipango ya mtaji haijakaa sawa naomba Mungu afungue njia”

USHUHUDA WA LEO

 1. Tony ametoka hospitali baada ya oparesheni
 2. Nimemaliza mitihani yangu salama

AHADI YA LEO (Matayo 3:2)

 • Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 1. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 2. Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
 3. Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
 4. Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)

Karibuni katika CHUMBA CHA MAOMBI ili tushiriki ibada ya maombi pamoja.

Ombi hili limetolewa na Mr. Advocate Kinja

Na lihimidiwe jina lako, Eee Mfalme Baba na Mungu wetu wa mbinguni.

Tazama ni jioni nyingine tena, tunakuja kwako Baba yetu, tupokee kwa jinsi tulivyo, maana tu wanyonge na wadhaifu hatujiwezi, tushike mkono.

Baba, Tusamehe dhambi na makosa yakiwa ya siri ama ya wazi, Tusamehe lkn huenda tumetenda kwa kujua ama kutokujua tunaomba utusamehe Mungu wetu.

Muda huu, wana na binti zako tunajinyenyekeza miguuni pako tunakusihi Munguwetu, tukusanye km vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, maana tutakua salama.

Ktk juma hili la kazi tumetembea huku na kule ktk maisha haya yule mwovu ametujeruhi tunakuomba tugange Bwana, maana huenda tulijitahidi kwa uwezo wa kibinadamu kujinasua lkn hatukuweza na hawezi kwa uwezo wetu, tugange majeraha yetu Baba.

Mfalme wa amani, wana wako wameleta mahitaji yao mbele zako, wakiomba rehema zako, tafadhali Yesu nakuomba, usituache maana magonjwa yanawatesa watumishi wako, nakuomba tafadhali Yesu, km ilivyokua zamani ulivyosema na wagonjwa wakapo, leo hii nakuomba tena Yesu gusa kwa mkononao wakapone. Huenda wapo mahospitalini ama majumbani mwao, Bwana mkono wako unafika kila mahali sema neno waja wako wapone.

Wapo ambao wanachangamiro za kifamilia nakuomba Yesuingilia kati, maana wewe wazijua magumu wanayopitia hayaelezeki hata wamekata tamaa leta tumaini kwao.

Zipo ndoa ambazo ucku huu usipo ingilia kati ndoa hizo ucku huu ndoa hizo zinavunjika, Baba wa mbinguni ingilia kati na ukaziponye ndoa hizi, upendo amani na furaha ikatawale hatimae jina lako litukuzwe Mungu wetu.

Wapo wanaohitaji mitaji ktk kufungua biashara Yesu nakuomba ingilia kati wapatie mitaji ili Bwana jina lako litukuzwe, lkn wakurudishie zaka na sadaka zikafanye kazi ya utume ulimwenguni.

Wapo wanafunzi nao wanachangamoto za kimasomo, nakuomba Mungu wangu sema nao, nakila wanalopitia Yesu onyesha mlango wa kutokea na watu wako waendelee kukutumaini Wewe Mungu wa mbinguni.

Baba, tazana tupo masaa matakatifu ya sabato tubakuomba km ulivyoibariki Sabato yako ikawa takatifu nakuomba nasi ututakase ili mibaraka ya sabato iandamane nasi Bwana.

Tunakusihi Mungu wetu, tupatie Roho wako Mtakatifu ili aweze kutufunulia yaliyo mapenzi yako ili tuyatende hapa duniani km huko juu mbinguni.

Tunapoendelea kujifunza kupitia watumishi wako tunakusi tubariki, maana tunajua unasema nasi kupitia watumishi wako ambao ni wanadamu pia.

Tuvute kwa kamba za pendo lako, na kwa damu iliyomwagika pale kalvari oooh Yesu itusafishe na kututakasa, zaidi ya yote tuandae kwaajili ya ufalme ujao.

Tunaomba haya kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu amina.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published.