sifa za mtu aliyethibitishwa na kuimarishwa

Somo: KARAMA ZAKE NI KWA KUTUTHIBITISHIA NA KUTUTIA NGUVU.

Fungu Kuu: 1 Petro 5:10-11

 • Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu. Uweza una yeye hata milele na milele. Amina.

Imebarikiwa roho iwezayo kusema,

 • Mimi nina hatia mbele za Mungu: lakini Yesu ni Wakili wangu.
 • Nimeiasi sheria yake. Siwezi kujiokoa;
 • Bali naifanya damu ya thamani iliyomwagika Kalvari kuwa utetezi wangu wote.
 • Nilipotea katika Adamu, lakini nikarejeshwa katika Kristo.
 • Mungu aliyeupenda ulimwengu hivyo kiasi cha kumtoa Mwana wake wa pekee ili afe, hataniacha niangamie nikiwa nimetubu na kujuta rohoni mwangu.

Hatanitazama mimi, kwani mimi sifai kabisa;

 • Bali ataangalia uso wake yeye Aliyetiwa mafuta,
 • Atamtazama yeye aliye Badala yangu na Mdhamini wangu,
 • Atasikiliza ombi la Wakili wangu,
 • Aliyekufa kwa sababu ya dhambi zangu, ili nipate kufanywa kuwa haki ya Mungu katika yeye.

Kwa kumtazama yeye nitabadilishwa na kufanana na sura yake.

 • Siwezi kubadilisha tabia yangu mwenyewe, isipokuwa kwa kushiriki neema yake yeye ambaye ni wema wote, haki yote, rehema na ukweli.
 • Lakini kwa kuendelea kumtazama yeye, nitapata roho yake na kubadilishwa nifanane naye
 • Moyo ambao umejazwa kwa neema ya Kristo utadhihirishwa kwa amani na furaha yake;
 • Na pale Kristo anapokaa, tabia itatakaswa, itakuzwa, itaadilishwa na kutukuzwa.

UPENDO WA MUNGU

Muumbaji wa ulimwengu wote anataka kuonesha upendo kwa wote wanaoamini katika Mwana wake wa pekee kama Mwokozi wao binafsi, kama ampendavyo Mwana wake.

 • Hata mpaka hapa wakati huu tumepewa upendeleo wake wenye neema hadi kufikia kiwango hiki cha ajabu.
 • Amewapa watu karama ya Nuru na Ukuu wa mbinguni 
 • Ametoa hazina zote za mbinguni pamoja na yeye.
 • Siyo tu kwamba ametuahidi uzima unaokuja, yeye pia anatupatia karama za kifalme ambazo zitaadilisha, zitaongeza na kukuza tabia zetu.

Bwana anao udhihirisho wenye thamani zaidi wa neema yake kwa ajili ya kutia nguvu na kutia moyo.


“SIFA ZA MTU ALIYETHIBITISHWA NA KUIMARISHWA”

(1) DAIMA HUMWELEKEA YESU:

 • Kamwe haridhiki na hali yake ya udhaifu wa kibinadamu
 • Kamwe hayatazami mapungufu na makosa yake kisha akakomea hapo
 • Kamwe hawi katika hali ya kukata tamaa na kuvunjika moyo.
 • Humtazama Kristo, na kwa imani,
 • Tabia na sifa stahilifu ya Mwokozi, Wakali, Mpatanishi, Mbadala na Mtetezi wake huwa yake baada ya “kutubu na kujutia” hatia na dosari zake.

(2) HUTEGEMEA MABADILIKO:

 • “Kwa kumtazama Yeye nitabadilishwa na kufanana na sura Yake.”
 • Yaani kwa njia ya “kushiriki neema Yake”—wema, haki, rehema na ukweli.
 • Matokeo ya mabadiliko haya ya moyoni hudhihirishwa maishani: “amani na furaha Yake” na “tabia itatakaswa, itakuzwa, itaadilishwa na kutukuzwa.”

Sisi kama raia wa neema Yake,

 • Yesu angependa tufurahie “kila kitu kitachoadilisha, kitakachodhihirisha kikamilifu, na kukuza tabia zetu.”

JE, MUNGU YUKO TAYARI KIASI GANI?

 • “Hata mpaka hapa na wakati huu fadhila Zake za wema zimekabidhiwa kwetu hadi kufikia kiwango hiki cha ajabu… karama ya Nuru na Ukuu wa mbinguni.”
 • Kitendo cha Mungu kumtoa Kristo kwa ajili yetu, ni sawa na kutupatia “hazina zote za mbinguni.”
 • Ndani ya Kristo “hazina zote za hekima na maarifa zimesitirika.” Wakolosai 2:3.

Leave a Reply

Your email address will not be published.