April 18 -2016

 

MAOMBI YA ASUBUHI (Jumatatu ya 4/17/16)
1. Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
2. Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia ya Sauti Ya Injili)
3. Mada Ya Leo = TOBA, UNGAMO, MSAMAHA
SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:
1. Baraka tele & uaminifu wake kwetu
2. Tabia yake isiyobadilika
3. Msamaha wa dhambi zetu
4. Nafasi nyingine ya Uhai Leo.
5. Mwimbie MUNGU nyimbo za sifa kwa shangwe kuu.

WAGONJWA WETU (5)
Sisi sote tu wagonjwa wa kiroho, hivyo tuombee ili Tabibu Mkuu atuponye

(Barbara) “Wapendwa mnisaidie kumuombea mama yangu”.
• Ana maumivu makali sana ya mguuni yapata sasa miaka 25.
• Amesha ona madaktari mbali mbali, lakini hali bado si nzuri.

(Mpendwa Mmoja) “Naomba muombe kwa ajili ya wagonjwa wangu”:-
• Dada Tatu Mkomagi.
• Dada Mercy Swai

Rafiki yake Sule Mwassy (Mable) amepata depression, amezimia akakimbizwa Hospitali.

Andrew Songa, anaumwa sana, na amekimbizwa Hospitalini.
MAHITAJI & CHANGAMOTO ZINGINE
Mkutano mkubwa wa injili, BUNDA Mjini, Tanzania.

Ibrahim and Lydia, ilikua wafunge ndoa, lakini kabla ya ndoa, mimba ikajitokeza, sasa wamerudi kwenye madarasa ya ubatizo, tuwaombee Bwana awaimarishe kiimani.

Nina “diploma yangu ya “procurement and supply management” lakini siwezi pata ajira. Naomba maombi yenu.

George anataka 100 USD by 25th April ili kuhudhuria program ya kuuza vitabu huko Norway

USHUHUDA WA LEO
Ikielezwa na Mr. Oleruto – (imetafsiriwa from English –Swahili)

Habari za leo wapendwa? Nataka kuchukua muda maalum kuwashukuru kundi hizima kwa namna ya pekee .. Zaidi sana kikundi chetu cha maombi (TGV Prayer Band). Nafurahi sana, na nataka kuwaambia ndugu zangu wapenzi kua MUNGU ANAJIBU MAOMBI

Mimi mwenyewe nina ushahidi: baada ya ombi la pamoja na admin wetu (dada ELSIE)…. “tumekuwa tukiomba pamoja” na Mungu kwa uhakika akajibu maombi yangu

Tuendelee kuomba na maombi yetu yatajibiwa. AMINA.

Mungu abariki kundi hili zima: {Majukwa ya Sauti Ya Injili yote (English/Kiswahili)}

Mimi sijui aliyenioongeza huma, lakini tangu nijiunge nanyi, sijawahi juta. SIFA NA SHUKRANI KWA BWANA WETU.
AHADI YA LEO (2 Nyakati 7:14)
IKIWA WATU WANGU, WALIOITWA KWA JINA LANGU,
• Watajinyenyekesha, Na Kuomba,
• Na Kunitafuta Uso Wangu,
• Na Kuziacha Njia Zao Mbaya;
• Basi, Nitasikia Toka Mbinguni,
• Na Kuwasamehe Dhambi Yao,
• Na Kuiponya Nchi Yao.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:
1. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
2. Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
3. Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
4. Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)

Karibuni katika CHUMBA CHA MAOMBI ili tushiriki ibada ya maombi pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published.