April 17, 2016

Silhouettes of Three Crosses

MAOMBI YA ASUBUHI (Jumapili ya 4/17/16)

 1. Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
 2. Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia ya Sauti Ya Injili)
 3. Mada Ya Leo  = UFALME WA MBINGUNI

 

Maombi

SIFA & SHUKRANI: Mshukuru MUNGU kwa:

 1. Baraka tele & uaminifu wake kwetu
 2. Tabia yake isiyobadilika
 3. Msamaha wa dhambi zetu
 4. Nafasi nyingine ya Uhai Leo.
 5. Mwimbie MUNGU nyimbo za sifa kwa shangwe kuu.

Wagonjwa Wetu

 • Sisi sote tu wagonjwa wa kiroho, hivyo tuombee ili Tabibu Mkuu atuponye
 • (barbara) Wapendwa mnisaidie kumuombea mama yangu. Ana maumivu makali sana ya mguuni yapata sasa miaka 25. Amesha ona madaktari mbali mbali, lakini hali bado si nzuri
 • (mpendwa mmoja) “Naomba muombe kwa ajili ya mgonjwa anayeitwa Dada Tatu Mkomagi.Na mwingine anaitwa Dada Mercy Swai”

MAHITAJI & CHANGAMOTO ZINGINE

 • Mkutano mkubwa wa injili, BUNDA Mjini, Tanzania.
 • Ibrahim and Lydia, ilikua wafunge ndoa, lakini kabla ya ndoa, mimba ikajitokeza, sasa wamerudi kwenye madarasa ya ubatizo, tuwaombee Bwana awaimarishe kiimani
 • (dada) Nina “diploma yangu ya “procurement and supply management” lakini siwezi pata ajira. Naomba maombi yenu.

USHUHUDA WA LEO (na ndugu Oleruto); (imetafsiriwa from English –Swahili)

Habari za leo wapendwa?

 • Nataka kuchukua muda maalum kuwashukuru kundi hizima kwa namna ya pekee …..
 • Zaidi sana kikundi chetu cha maombi (TGV Prayer Band). Nafurahi sana, na  nataka kuwaambia ndugu zangu wapenzi kua MUNGU ANAJIBU MAOMBI
 • Mimi mwenyewe nina ushahidi: baada ya ombi la pamoja na admin wetu (dada ELSIE)…. “tumekuwa tukiomba pamoja” na Mungu kwa uhakika akajibu maombi yangu
 • Tuendelee kuomba na maombi yetu yatajibiwa. AMINA.
 • Mungu abariki kundi hili zima: {Majukwa ya Sauti Ya Injili yote (English/Kiswahili)}
 • Mimi sijui aliyenioongeza huma, lakini tangu nijiunge nanyi, sijawahi juta.
 • SIFA NA SHUKRANI KWA BWANA WETU.

AHADI YA LEO (Zaburi 66:19-20)

 • 19 Hakika MUNGU amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.
 • 20 Na ahimidiwe MUNGU asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.

TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:

 1. Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
 2. Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
 3. Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
 4. Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)

Karibuni katika CHUMBA CHA MAOMBI ili tushiriki ibada ya maombi pamoja.


Advocate Kinja: Tuombe tafadhali

Baba, muumba wa mbingu na nchi, bahari na chemichemi za maji, tunalihimidi na kulitukuza jina lako wakati huu.

Weweni Mungu wa miungu Mfalme wa wafalme na Bwana wa Bwana, ni kuu sana jina lako, ni Mungu unaeishi na kutawala malimwengu yote, tunakurudishia sifa na shukrani wana sauti ya injili ucku huu.

Tukiwa tumejeruhiwa na kuumizwa ktk mahangaiko yetu, tunahitaji faraja yako ya pekee kwetu, maana faraja ya kweli yapatikana kwako tu.

Lkn Bwana, tunakuja kwako kwa jinc tulivyo tusamehe pale tulipoenda na kutenda kinyume na mapenzi yako, tunakuja tunakukaribia wewe maana titapata pumziko la haki. Dhambi zetu ni nyingi km mchanga wa bahari, lkn wewe unatuita tuje tesemezane nawe maana dhambi utazisafusha zitakua nyeupe km ilivyo sufu, tutakase kwa damu yako ili tuweze kusimama kwa zamu zetu.

Masaa haya tunaleta haja zetu mbele ya kiti chako tunaamini sijio lako c zito hata uctuckie sauti yetu, lkn kwa kua hatujui kuomba, kwa kupitia kwa Roho wako Mtakatifu yeye anayetusaidia tena anagua icvyoweza kuelezeka na ayabadilishe maombi yetu yakawe manukato mazuri nawe ukatujibu sawasawa na mapenzi yako.

Wapo wavonjwa, tunawaweka mikononi mwako wewe uliye tabibu mkuu Yesu tena mwenye huruma, tena unaleta faraja kwa wagonjwa wapatie uponyaji kwa kila anaumwa, wapo ambao wamepata depression Yesu unajua ni kwa namna ambavyo wanateseka, nakuomba tenda muujiza pekee na madaktari washangae, kwamba ni kwa namna gani wamepona, na jina lako likatukuzwe nahali hapo.

Wapo wengine wagonjwa majumbani na hawa nao ucwapite, yupo yule mama mwenye kidonda na yule mwenye mafua ya muda mrefu lkn hayaponi, nakuomba Yesu kwakua wametambua kua wewe ni tabibu mkuu dhihirika kwa watu hawa, kwa ajili ya utukufu wako.

Bwana umetuita na kutuweka kukutumikia ktk maishayetu, lkn zipo changamoto tunazokutana nazo hata Wakati fulani kibinadam tunakata tamaa sababu ya ugumu wa maisha, wachumba wametukimbia, tupatie tumaini na tunapokumbana nayo tukutegemee wewe uletaye faraja ya kweli.

Upo mkutano wa injili ktk eneo la Bunda tunaendelea kuuombea ufanikiwe na kwa njia ya Roho Mtakatifu aendelee kusema na mioyo ya watu wako ili mavuno yakaonejane kwa wakati wake, tunawaombea sana viongozi wetu walioratibu mkutano huu, wakiongozwa na Roho wako, wapatie ujasiri waimarishe wasimame wakitangaza ujumbe wako na kuwalisha kondoo zako.

Mfalme wetu, ipo ndoa mbele yetu, tunaendelea kuwaweka mikononi mwako maharusi uwalinde na kuwatunza hadi cku ya tukio wabayoingojea sana na ikatimie kwa utukufu wa jina lako.
Wapo wanaohitaji kufikia malengo yao, Bwana wewe wawajua, na kwakua unajua mwisha tangu nwanzo, jidhihirishe maishani mwao wakutukuze Mungu wa mbinguni. Wapo wanaohitaji ajira fanikisha Bwana maana vyeti vyao wanavyo lkn kazi hawana, hawa nao ucwapite, wanapokukaribia wakusanye ukawalatie faraja ya kweli wanapofanikiwa walitukuze jina lako.

Baba watujua hata wale wanaohktaji mitaji ya kufungua makampuni onekana kwao, wanapoomba hata na kufunga wakikulilia Yesu wangu weww ndiwe tumaini letu.

Yapo mengine mengi hatujaomba lkn wajua ni mahitaji yetu, tutendeee kqa kadiri ya mapenzi yako.

Tunajikabidhi mikononi mwako maana hutatuacha hata km dhoruba na tufani xivume kiasi gani wewe upo nasi, tunaomba haya kupitia kwa Yesu Kristo aliye Bwana na mwokozi wetu Amina.

Leave a Reply

Your email address will not be published.