April 16, 2016

MAOMBI YA ASUBUHI (Sabato ya 4/16/16)
- Saa 11-12 (Maombi ya binafsi/ Nyimbo za Injili)
- Saa 12-1 (Maombi ya Jumla kama Familia)
- Mada Ya Leo = HUDUMA YA NENO LA INJILI
SIFA & SHUKRANI: Tumshukuru MUNGU kwa:
- Baraka tele & uaminifu wake kwetu
- Tabia yake isiyobadilika
- Msamaha wa dhambi zetu
- Nafasi nyingine ya Uhai Leo.
- Mwimbie MUNGU nyimbo za sifa kwa shangwe kuu.
FAMILIA YA SAUTI YA INJILI (Wagonjwa Wetu)
MAHITAJI & CHANGAMOTO ZINGINE
- Mkutano mkubwa wa injili, BUNDA Mjini, Tanzania.
- Familia ya Mstaafu Okeyo wa Tanzania Unio, Aliyekua Mrs. Okeyo, amelala usingizi wa mauti, tuombee hiyo familia. (Kwa maelezo zaidi wasiliana na Elder Kikiwa)
- Ndugu Edwin Magak, anasafiri kwenda “Suba in Homa Bay county” 9kenya) tumuombee na kikundi chao kinachoitwa (The Promise) , ili wahudumu huko Sabato hii.
- Tumuombee dada yetu apate (a) MCHUMBA, Mcha Mungu, atakaye kua serious kufunga naye Ndoa, kulingana na Mapenzi ya Mungu. (b) Apate Ruhusa Kazini siku ya Sabato,
- Aliyekua ICU (kenya) amelala usingizi wa mauti. Tuombee washiriki wa Calvary Ministers, Fedha za kusafirisha mwili kwa maziko; Mjane mchangwa aliachwa nyuma.
USHUHUDA WA LEO (N/A)
AHADI YA LEO (Ezekieli 20:12)
- “Tena naliwapa Sabato Zangu, ziwe ishara kati ya MIMI na wao, wapate kujua ya kuwa MIMI, BWANA, Ndimi Niwatakasaye”
TUNAKARIBISHWA KUFANYA YAFUATAYO:
- Kutoa ushuhuda wa Matendo makuu ya MUNGU
- Kuweka Audios za Maombi (Sauti), ama Kuandika.
- Kutujulisha kama OMBI LAKO limejibiwa (ili tupunguze list)
- Kushiriki katika kipindi kingine cha Maombi Ya Jioni (Saa 3 Usiku)