Marko 8: Mwongozo wa Biblia

41-BSG-8A: MWONGOZO WA IBADA

Marko 8: Mwongozo wa Ibada/41-BSG-8A (Marko 8:)/Dhima: Yesu ni Nani Kwako?/Wimbo: Nataka Nimjue Yesu! (NK # 54)

Uchunguzi: Yesu, Mwana wa Mungu — (Mat. 8:29; 27:43, 54; Marko 3:11; 15:39; Luka 1:35; 3:21–22; 4:41; 9:35; 22:70; Yohana 1:34, 49; 5:18; 10:30, 36; 11:4; 14:9–10; 19:7).

Tafakari: Katika sura hii, Yesu Yesu anawalisha watu 4,000. Mafarisayo wanadai ishara ya muujiza kutoka kwa Yesu, lakini Yeye anawakatalia. Yesu anamponya Kipofu. Kisha anatabiri kifo Chake Mwenyewe. Anawauliza wanafunzi Wake swali muhimu zaidi katika vizazi vyote: Watu huninena Mimi kuwa ni nani?” (Marko 8:27, 29). Kisha anawauliza wanafunzi kwamba wao wanadhani Yeye ni nani, na Petro kisahihi anambainisha Yesu kuwa Masihi.

Kuna dhima nyingi hapa, lakini kwa kusudi la ‘Wasaa wa Ibada’ asubuhi hii, Mwalimu wa Kiungu huvuta mawazo yetu ili yazingatie Yeye ni nani. Wakati wakisafiri katika miji ya Kaisaria Filipi, Yesu aliwauliza wanafunzi Wake, “Watu huninena Mimi kuwa ni nani?” Walijibu kwa kukisia vile ambavyo hadhara ilimdhania Kristo – baadhi walisema, Yohana Mbatizaji, Eliya; wengine, mojawapo wa Manabii. Kisha Yesu akaelekeza tena swali hilo kwao (v. 29) ikimaanisha, alitegemea wawe na ufahamu bora zaidi ya hapo. Wapendwa, Marko 8:27–33 ni kiini cha kimuundo cha Injili nzima ya Marko. Kujua wadhifa wa Yesu Kristo ni muhimu sana kwa jamii yote ya wanadamu. Hatimaye, Petro alijibu kisahihi: “Wewe ndiwe Kristo” (v. 29). Katika Mat 16:16, Petro anaongeza, “Mwana wa Mungu aliye hai.” Haleluya!

Maana ya Kiibada: “Wanafunzi walijibu swali la Yesu kwa mtazamo tashibia (wa wengi) kwamba Yeye alikuwa mojawapo wa manabii wakuu aliyefufuka. Hii ililandana na rekodi ya imani za watu katika Yohana 6:14–16. Pengine imani hii ilitokana na Kumbukumbu 18:18, ambapo Mungu alisema angemwinua nabii kutoka miongoni mwa watu…. Haitoshi kujua kile ambacho wengine wanasema kumhusu Yesu: Lazima ujue, uelewe, na kukubali wewe binafsi kwamba Yeye ni Masihi. Lazima uhame kutoka udadisi hadi katika nadhama (kufanya maamuzi ya dhati kwa ajili Yake), kutoka kuhalili hadi usabihifu. Ikiwa Yesu angekuuliza swali hili, ungelijibuje? Je Yeye ni Bwana na Masihi wako?” – [Bruce B. Barton, Mark, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1994), 233, 234].

Sauti ya Injili: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, wakati wa uhamwilisho Wake, Yesu Kristo alikuwa siyo tu Mwanadamu fulani mwenye mawazo adhimu, Mhubiri, Mwalimu wa kiungu, Mtenda-miujiza — alikuwa, na bado angali, Mungu mmoja wa kweli (Yn. 17:3; Ebr. 1:8); Mpatanishi pekee kati ya Mungu na wanadamu (1 Tim 2:5); chanzo cha uhai – Uzima wa Milele (Yn. 3:16, 36; 10:28; 14:6; 17:3; Rum. 6:23). Mwanangu, “wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” isipokuwa Yesu Kristo, (Matendo 4:12). Kumjua na kumtii Yesu, humaanisha uzima wa milele; kumkataa Yesu, humaanisha hukumu ya milele (Yn. 3:18). Nakualika umtafakari Yesu, na kumkubali kama Bwana na Mwokozi wako. Je utafanya hivyo?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka – 1. Kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai/ 2. Kumtii Yeye kwa kuzishika Amri Zake/ 3. Kumwomba anisamehe dhambi zangu na kuniandaa kwa ajili ya Ufalme Wake.

Iweni na Siku Yenye Baraka: “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.” (Yohana 3:36) “Amwaminiye Yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yohana 3:18)

Ibada Kupitia Uimbaji: Nataka Nimjue Yesu! (NK # 54)

  1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu; Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

         [Pambio] Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu; Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

  1. Nataka nimjue Yesu, na nizidi kusikia; Anenapo kitabuni, kunidhihirisha kwangu.
  2. Nataka tena zaidi, daima kupambanua; Mapenzi yake, nifanye yale yanayompendeza.
  3. Nataka nikae, kwa mazungumzo matamu; Nizidi kuwaonyesha wengine wokovu wake!

Mwisho: Ambaza kwenda chini hadi Kipengele (41-BSG-8B) kwa ajili ya ‘Mwongozo wa Maombi.’ Bwana Akubariki!