Marko 5: Mwongozo wa Biblia

MARKO 5: MASWALI NA MAJIBU.

Mwongozo wa Biblia/ Marko 5, (41-BSG-5J)/ Maswali na Majibu.

[1] Nini dhima kuu katika Injili ya Marko 5? Miujiza ya Ukombozi, Uponyaji, na Ufufuo.

[2] Kisa cha kwanza kinatufundisha nini kuhusu mapepo? Mapepo ni malaika walioanguka. Wakati Lusiferi alipoanguka kutoka mbinguni, aliwachukua baadhi ya malaika pamoja naye- (theluthi moja, Ufu. 12:4). Yuda 6 pia huwataja malaika waliotenda dhambi. Baadhi ya mapepo tayari wamefungwa kwa “vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu” (Yuda 1:6) kwa ajili ya dhambi zao. Wengine wako huru kuzurura na hujulikana kama “falme na mamlaka, wakuu wa giza hili, majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho” (Waefeso 6:12; Wakolosai 2:15). Mapepo bado yanamfuata Shetani kama kiongozi wao na kufanya vita na malaika watakatifu. Shetani na malaika zake (mapepo) wanachukia sana watakatifu wa BWANA, hivyo hufanya kila njama kuwajaribu, kuwaangusha, kuwatesa, na ikiwezekana kuwauwa.

[3] Je, mapepo bado yanaweza kuwaingia watu leo? Ndiyo. Mapepo, kama roho wachafu, wana uwezo wa kuteka na kuumiliki mwili. Milki ya mapepo hutokea wakati mwili wa mtu fulani unadhibitiwa kabisa na pepo. Hii haiwezi kumtokea mtoto wa Mungu, kwa kuwa Roho Mtakatifu anakaa katika moyo wa muumini katika Kristo (1 Yohana 4: 4).

[4] Nini matokeo gani ya milki ya pepo? Tabia isiyo ya kawaida (1 Sam 18:10-11; 19: 9-10); kusababisha vurugu (Mt 8:28), kutumia nguvu zisizokawaida (Mk 5:4), kusababissha uharibifu binafsi (Mk 5:5; 9:22), kusababisha upofu au kushindwa kusema (Mt 12:22; Mk 9:17), kusababisha mtu kupata maumivu na mashambulio (Mk 9:18, 26), na kuugua magonjwa (Mt 4:24; Mk 1:32).

[5] Je, Yesu Kristo anaweza kutukomboa kutokana na mapepo? Ndiyo (soma Mt 8:16; Mk 1:32; Lk 4:40; Mt 4:24; 9:32; 12:22; 15:22; Mk 7:25-26).

[6] Je, huyu mwenye pepo alikuwa na maisha ya namna gani? Aliishi makaburini; Hakuna ye yote aliyeweza kumfunga, hata kwa minyororo; Sikuzote, usiku na mchana, alikuwako makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikata-kata kwa mawe.

[7] Je, mtu huyu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili? La. Alikuwa na pepo wabaya.

[8] Nguruwe walimaanisha nini kwa Wayahudi? – “Kwa mujibu wa sheria ya Agano la Kale (Mambo ya Walawi 11:7), nguruwe walikuwa wanyama “wachafu”. Hii ilimaanisha kwamba hawangeweza kuliwa au hata kuguswa na Myahudi. Tukio hili lilitokea kusini mashariki mwa Bahari ya Galilaya katika eneo la Gerasenes (5:1), eneo la Mataifa.” — [Bruce B. Barton, Mark, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1994), 132].

[9] Kwa nini Yesu alituma pepo kuwa nguruwe? Wakamwomba, wakisema: Tupelekeni nguruwe ili tuingie ndani yao! (5:12)

[10] Kwa nini wachungaji wa hawa nguruwe walikimbia? Waliogopa! “Walikimbia na kuripoti mjini na nchini. Watu wakaja kuona kile kilichotokea” (5:14)

[11] Ni nini kinachovutia kuhusu kisa hiki? Wageresi wakamwendea Yesu, walipofika – “wakamwona yule mwenye pepo, ameketi, amevaa nguo, ana akili zake, naye ndiye aliyekuwa na lile jeshi; wakaogopa” (5:15).

[12] Mwitikio wao ulikuwa nini? Hofu! Waliogopa sana; walimwomba Yesu aondoke katika eneo/ mipaka yao (5:15, 17)

[13] Kwa nini Yesu alimkatalia yule aliyekuwa na pepo kumfuata? Alihitaji awe mmisionari katika Kijiji chakena khabari njema za wokovu.

[14] Utume wake ulikuwa nini? Agizo gani alipewa? — “Enenda zako nyumbani kwako, kwa watu wa kwenu, kawahubiri ni mambo gani makuu aliyokutendea BWANA, na jinsi alivyokurehemu” (5:19)

[15] Decapolis ilikuwa nini? Miji kumi ya Hellenistic (5:20)

 

41-BSG-5Y: SAHUMU YA JIONI.

Marko 5, (41-BSG-5Y)/ Wazo la Usiku kinaloshabihiana na Mpango wa Usomaji wa Biblia wa leo/ Dhima:  Yesu, Mtoaji wa Uzima! Aya Makini: Marko 5:21–43

Utangulizi: Kila mahali Kristo alipokwenda, alikutana na watu wenye matatizo. Wakati Kristo alipofika ufukoni upande wa pili, umati mkubwa ulikuwa pale ukimsubiri na mahitaji mbalimbali (Aya ya 21). Binti wa Yairo alikuwa mgonjwa sana, karibu kufa. Yairo anamsihi Kristo aje mara moja ili kumponya. Yairo alikuwa kiongozi wa sinagogi (Aya ya 22-23).

Mwanamke Asiyekata Tamaa: Yesu Kristo daima alikuwa na umati unaomzunguka (Aya ya 24). Watu walimfuata kwa sababu mbalimbali — umaarufu, changamoto, udadisi, n.k. Katika mstari wa 25, tunatambulishwa kwa mwanamke ambaye alikuwa na suala sugu la kutokwa damu (hemorrhage) kwa miaka 12. Alitumia fedha zake zote bila kupata nafuu. Kwa kweli, hali iliendelea kuwa mbaya zaidi (Aya ya 26). Alishinikiza kupitia umati wa watu na kumgusa Yesu. Aliamini kuwa endapo angegusa tu vazi la Kristo, angefanywa mzima kabisa! (Aya ya 27-29), na hivyo alifanya hivyo! Yesu alijua kwamba nguvu za kuponya zilikuwa zimetoka mwilini Mwake. Akauliza ni nani aliyemgusa (Aya ya 30-31). Yule mwanamke alikuwa na hofu – alikuja na kuanguka mbele Zake na kumwambia ukweli wote (Aya ya 33). Angalia jibu la Kristo kwake: “Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena” (Aya ya 34).

Mfu (Msichana) Aliyefufuliwa: Sura hii inahitimishwa kwa urejesho wa Muujiza wa Uzima. Hapo awali, tuliona kwamba binti wa Yairo, (yapata miaka 12) alikuwa mgonjwa sana, (Aya ya 22-23) lakini sasa amekufa (Aya ya 35). Angalia Maandiko yanavyosema – “Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, Amini Tu” (Aya ya 36). Katika mji huu wa Yairo, sasa kuna Msiba, watu wanalia kwa majonzi makuu.  Yesu anamchukua Petro, Yakobo, na Yohana ndugu ya Yakobo, na kuingia chumabi alipo marehemu. Vilio na simanzi vimetanda! Cha kushangaza, Yesu anasema binti (marehemu) “amelala tu”— na si amekufa! Labda nikukumbushe kuwa Biblia inaita kifo “usingizi” (soma Zab 90:3-6; Ayubu 7:21; 14:10-12; Zab 13:3; Dan 12:2; Mt 9:24; Mk 5:39; Lk 8:52-53). Yesu anamwamuru yule mfu arudi uzimani, na ghafla, maisha yake yanarejeshwa mara moja! (Aya ya 42)

Maana ya Kiibada: Waombolezaji ambao walikusanyika katika mji wa Yairo walikuwa na mshangao mkuu: Labda sasa wange wao walianza kuamini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Pengine walianza kujiuliza: “Nani awezaye kufufua wafu isipokuwa Mungu? Wapendwa, hata leo, Yesu ana uwezo wa kuwafufua wafu, anapochagua kufanya hivyo. Lakini kile ninachotaka kikisisitiza katika hadithi hii, ni wito wa Kristo kwa Yairo, Usiogope, Amini Tu!” (Marko 5:36). Ni wangapi kati yetu wanakosa mibaraka ya Mungu (ya kimwili/ kiroho) kwa sababu tu ya kutoamini? Tatizo letu kuu ni kutokuwa na imani. Yesu aliwaambia wanafunzi Wake – “Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu” (Mathayo 17:20). Je, Mungu ananiambia nini hasa katika ujumbe huu?

USIOGOPE – Kwamba tatizo lako ni kubwa sana kushughulikiwa na Mungu; Kwamba ugonjwa wako hautibiki; Kwamba dhambi zako ni nyingi mno haziwezi kusamehewa; Kwamba upendo wa Mungu unabagua; Kwamba rehema Zake si kwa ajili yako; Kwamba ahadi Zake si kwa ajili yako, Maandiko yanasema hivi,  “Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika Yeye (Yesu Kristo) ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika Yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi.” (2 Wakorintho 1:20)

AMINI TU- Kwamba Mungu anaweza kukuokoa; Kwamba yu tayari kuokoa; Kwamba atakuokoa; Kwamba anaokoa watu Wake! Mtume Paulo anatukumbusha jambo moja makini hapa – “Naye, [Yesu Kristo] kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa Yeye; maana Yu hai sikuzote ili awaombee” (Waebrania 7:25). Yaani, Kristo Yu hai katika hekalu la mbinguni akituombea. Jamani, hii ni zawadi kuu namna gani? Ndugu yangu mpendwa, “Amini Tu!”

Iweni na Usiku Mwema: Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. (Marko 9:23)