Isaya 2: Mwongozo wa Biblia

23-BSG-2A: MWONGOZO WA IBADA

Mwongozo wa Ibada Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Isaya 2/ Dhima: “Njoni, twende juu Mlimani kwa Bwana”/ 23-BSG-2A, (Isaya 2:2-5)/ Wimbo: “Tis almost time for the Lord to come.” (SDAH 212)

UCHUNGUZI: Wamishenari: Kuwaalika wengine waipokee Injili– (Isa. 2:3; Zab. 34:8; 2 Wafalme 7:9; Isa 52:7; Yohana 4:17-18, 25, 29; Yohana 1:46, 41-49; 16:30; Mat 12:23; Mat 28:19-20; Ufu. 22:17)

TAFAKARI: Sura hii huanzisha mjadala mrefu kuhusu ujeo wa ufalme wa Mungu na Hekalu Lake; Siku ya BWANA, na Urejeshwaji wa Israeli (Isaya 2:1–4:6). Sura ya 2 inaweza kugawanya kama ifuatavyo– Zama: Siku za mwisho (Isa 2:2a); utukuzwaji wa ufalme wa Mungu (Isa 2:2); kusudi la ufalme wa Mungu duniani (Isa 2:3-4); wito kwa waumini: kutembea nuruni, hedaya ya Bwana (Isa 2:5). Sehemu iliyosalia ya sura hii hujadili kuhusu Siku ya BWANA ijayo, na Hukumu ya Kutisha (Isa 2:6-22).

MAANA YA KIIBADA: Shairi hili [Isaya 2:2-5] lina msingi katika ujumuluku (inayohusu ulimwengu mzima) wa ahadi kwa Ibrahimu (Mwa. 12:2–3; 22:16–18). Kusudi la ufalme wa Mungu duniani (2:3-4) ni kuwavuta na kuwaokoa wasiyokolewa bado ili kuja kwa BWANA; kuwaamsha watu wote wasikie na kutii Neno la Mungu; na kuleta amani duniani. Hebu zingatia kwamba matokeo yatakuwa Kazi Jumuluku ya Kimishenari– “Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu.” (Isaya 2:3). “Wenyeji wa mji huu watauendea mji huu, wakisema, Haya! Twendeni zetu kwa haraka tuombe fadhili za Bwana, na kumtafuta Bwana wa majeshi” (Zek. 8:21, 22), na kwa Israeli, “Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi” (Zek. 8:23). Ahadi hii ya utundizaji (ukusanyaji) wa mataifa ili wamwabudu Mungu wa kweli haikutimizwa kwa Israeli halisi, kwa sababu ya kushindwa kwao kukidhi masharti faradhi, lakini itatimizwa kiroho, kwa watu wa Mungu katika kizazi hiki.” (SDA BC 4:105).

Wapendwa, “ikiwa ulimwengu utasema, Njoni, twende juu mlimani (3), lazima watu wa Bwana watii wito huo kwa kusema, njoni, twende (5): faradhi ya kwanza ya uinjilisti ni kuwa na kanisa linaofaa kujiunga nalo!” (Tyndale Old Testament Commentaries). Majirani/wafanyakazi wenzako wakikuona, hivi wanapata chochote chenye mvuto? — Mwenendo, matendo, maneno, uadilifu wako, nk. Je kuna chochote maishani mwako (kama mwanafunzi wa Kristo) kinachofaa kuigwa? Mungu anawatafuta watu, masalia waaminifu watakaowaelekeza wengine kwa Kristo, kwa sheria Yake, kwa Neno Lake, kwa kazi Yake inayoendelea hekaluni mbinguni, naam, kwa Ujio Wake wa Pili! Je u miongoni mwa waaminifu hawa? Je unaenenda katika nuru ya Neno Lake?

SAUTI YA INJILI: Sehemu hiyo imeandikwa kana kwamba Mungu anazungumza nawe moja kwa moja — kwa sababu Yeye anafanya hivyo. Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, Yesu Kristo anakuja hivi punde (Ufu. 1:7) lakini watu wengi hawajaisikia injili na kufanya maamuzi kwa ajili ya Kristo. Je ungependa kujiunga katika juhudi hii ya kuitangaza Injili maeneo mengi na mbali? Je ungependa “Kwenda” haraka mitaani na njiani, na katika barabara kuu, na kuwaita walemavu, viwete na vipofu, nk. ili wawe tayari kwa ajili ya mapambazuko? Pili, nakualika sasa uje Kwangu: Nitawafundisha njia Zangu, na kuwafanya mwenende katika mapito Yangu (2:3b). Nitakusafisha na kukuakifisha kwa ajili ya ufalme wa utukufu ujao. Je utasalimisha vyote na kuja Kwangu?

Shauku Yangu: Kwa neema ya Mungu, nataka kuwa Kitabu Mafunzo kwa ajili ya Kristo (Mat 5:16). Kupitia matendo yangu, nataka kuwavuta na kuwaalika watu wengi kadiri niwezavyo ili waje kwa BWANA; kuwaamsha watu wote waitii injili.

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.” (Isaya 2:5) “Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru” (Waefeso 5:8).

23-BSG-2B: MWONGOZO WA MAOMBI

Mwongozo wa Maombi Unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Isaya 2/ Dhima: Tembea katika Nuru / 23-BSG-2B, (Isaya 2:5)/ Andiko Msingi: “Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.” (Isaya 2:5)/ Wimbo: Brightly beams our Father’s mercy [Mwandishi: P. P. Bliss (1871)]

Maelezo ya Ufunguzi: Nasihi ya kwanza: Enendeni na Bwana (linganisha nasihi ya pili katika Isa. 2:22). “Katika nuru humaanisha katika nuru ya fadhila ya Bwana (Hes. 6:25), uwepo na uangalizi Wake (Zab. 27), kweli Yake (Zab. 43:3) na neno Lake lililofunuliwa (Zab. 119:105).” (Tyndale Old Testament Commentaries)

Nani aliye Nuru ya BWANA? Yesu Kristo. Katika Yeye nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu huangazwa (2 Kor. 4:6), na utukufu ukamilifu wote wa silika ya kiungu hudhihirishwa. Yeye ndiye nuru hasa ikaayo na Mungu, Yeye ndiye aliyemtuma; alikuja ulimwenguni humo kama nuru iliyotumwa kutoka juu. Yesu Kristo ndiye “mng’ao wa utukufu Wake (ikiakisi utukufu wa Mungu wa Shekina, Nafsi mwenye Nuru, nuru angavu ya kiungu) na chapa ya nafsi Yake” (Ebr. 1:3). Yeye ndiye nuru waliyopewa Wamataifa. Yeye ni mwasisi wa nuru yote; nuru jisimu: jua, mwezi, na nyota. Yeye ni Nuru ya Injili ya neema ya Mungu. Yeye ni nuru ya kiriho ya neema mioyoni mwa watu Wake. Yeye ni nuru ya utukufu wa milele: “Na mji ule hauhitaji jua wala mwezi kuuangaza, kwa maana utukufu wa Mungu huutia nuru, na taa yake ni Mwanakondoo.” (Ufu. 21:23)

Wapendwa, kuenenda katika Nuru hii ni kutembea kwa imani katika Yesu, kuishi kwa kuamini katika mafundisho Yake, na kumfuasa (kumwiga). Kutembea kwenye nuru ya Injili humaanisha: kuipokea, kuitetea, kuishikilia imara, na kuidumisha, na kutembea kadiri inavyoelekeza na kuongoza.

Tunapokuja katika Kipindi cha Maombi leo, tunaalikwa— “kuenenda kama watoto wa nuru” (Efe. 5:8); kuenenda kwa busara na hadhari, kadiri istahilivyo wito wa Mungu, wa neema anaotuita kwayo, na ufalme anaotuita kuuingia. Kristo anamwita kila mmoja wetu kujitenga na dhambi, na kutembea katika upya wa uzima; kushamirisha nuru ya injili na “tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu” (Tito 2:13). Tafadhali zingatia kwamba tunapokuwa tumeongoka kikamilifu, mara tu Kristo hajarejea, nchi itaangazwa kwa utukufu Wake (Ufu. 18:1) “Licha ya harakati za kishetani kuifunika dunia gizani, sasa Mungu ataiangaza kwa nuru tukufu ya ukweli uokoao (Yohana 1:4, 9)” – (SDA BC 7:860). Je uko tayari kuwa nuru ndogo kwa ajili ya Yesu?

Maadili ya Kukuza: Imani, Maombi, Kutembea katika nuru ya BWANA.

Dhambi za Kuepuka/Kuungama: Kushindwa kujisalimisha kikamilifu kwa Mungu na kuyafuata mapenzi Yake; kutoishi maisha ya utauwa; ushirikina; upiga-ramli; kufanya mikataba na wasiomcha Mungu (Isa. 2:6); kutumainia vitu, mali, utajiri; kutumainia nguvu, uwezo binafsi (Isa 2:7); ibada ya sanamu (Isa 2:8); kiburi; kushindwa kutii mausia→ Usimfaridi mwanadamu (kuliko Mungu, Isa 2:22)

Jambo la Kumshukuru Mungu Kwalo: Yesu: Nuru ya ulimwengu; ufalme wa Mungu duniani; utaalifu (hali ya kilimwengu) katika maarifa kuhusu Mungu; wamishenari waliojiadhimu kwa kazi ya injili.

Watu wa Kuombewa: Wapogofu (waumini waliorudi nyuma); waombee waumini wote waenende katika nuru. “Bali tukienenda nuruni, kama Yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu Yake Yesu, Mwanawe, yatusafisha dhambi yote.” (1 Yohana 1:7)

Masuala ya Kuombea: Kitabu cha Isaya; Fursa ya Kumwendea Mungu; Ahadi ya Siku ya Yehova; Uhuru wa Kuabudu (Kutano la Kiroho); Ubora na Utukufu wa Kanisa; Marudi na Mausia katika Isaya; Maandalizi kwa ajili ya Hukumu Ijayo; Mwenendo wa Ukristo katika Siku za Mwisho; Wamishenari: Wakristo wote wanaohudumu kama Wamishenari (Ujumuishwaji Timilifu wa Mshiriki); Amani; Kuhuzunikia Dhambi; Wokovu (Mbingu kwa Waliokolewa); Hekalu (Miili Yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu); Neno la Mungu Lishamiri; Ari katika Kuifanya Kazi ya Mungu.

Ahadi ya Leo: “Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” (Yohana 8:12)

Hatua ya Maamuzi: Tumia wasaa fulani kujichunguza: Je unaona maishani mwako yoyote miongoni mwa Dhambi Mahususi zilizoorodheshwa hapo juu? Ikiwa ndivyo; ungama na kutubu mara moja. Kumbuka, “Dhambi ambazo hazijafanyiwa toba na kuachwa hazitasamehewa, na kufutwa kwenye vitabu vya kumbukumbu, bali zitasimama ili kushuhudia dhidi ya mdhambi husika katika siku ya Mungu.” (The Faith I Live By, uk. 211). Tumia muda fulani kuombea mambo yaliyoorodheshwa hapo juu; mwombee mtu fulani anayepambana na dhambi hizi. Endapo una Mahitaji ya Maombi, tafadhali, yaandike hapa chini, na mtu fulani atayaombea. Mungu akubariki!

Sala: Baba, tunakushukuru tena kwa neno Lako katika Isaya sura ya 1. Tunakushukuru kwa ajili ya tumaini lililopo katika sura hii, kwamba watu wengi wataisikia injili na kuja Kwako. Tusaidie kuwa wamishenari wale waliotumwa kutoka Kwako watakaotangaza injili na kuwavuta wengi waje kwa Yesu Kristo. Tusamehe, Bwana, dhambi zilizoorodheshwa katika sura hii. Na ilhali tukiwa na Nuru (Yesu Kristo), hebu tusaidie ili tumwamini Nuru ili tuweze kuwa watoto wa Nuru (Yohana 12:36). Tufundishe jinsi ya kuenenda kama watoto wa nuru (Efe. 5:8). Tusaidie kufuzu kuungia Mji ule mtukufu—ambapo “Na mataifa watatembea katika nuru yake. Na wafalme wa nchi huleta utukufu wao ndani yake.” (Ufu. 21:24) Tunakushukuru Bwana, Nasi tunaomba mambo haya, tukiamini na kutumaini, katika jina la Yesu Kristo, Amina.

Isaya 2: Mwongozo wa Kujifunza Biblia

23-BSG-2C: MUHTASARI WA SURA

 • Wahusika: Mungu, Isaya
 • Neno la Msingi: Siku za Mwisho (Isaya 2:2)
 • Maandiko Makini: Isaya 2:1, 2-5, 12, 13, 14-18, 19, 20, 21-22.

Maneno Muhimu:

 • [Isa. 2.3] “sheria” (Ebr. torah) = itikadi, mafundisho, maelekezo
 • [Isa. 2:4] “Naye atafanya hukumu” (Ebr. spt) = hukumu, pitisha uamuzi, nafidhisha haki, tawala
 • [Isa. 2:4] “Taifa/ Mataifa” (Ebr. goy) = watu, wapagani, kafiri
 • [Isa. 2:5] “BWANA” (Ebr. yhwh) =Yehova
 • [Isa.  2:9, 11, 17] “nyenyekeshwa, dhilishwa” (Ebr. spl) = shusha, angusha, dhili, tweza
 • [Isa. 2:10] “ukajifiche mavumbi” (Ebr. shh) = ogopa, chutama, jiinikiza, kaa kipya, bomoka

Kwa Usomaji Zaidi: Sifa za ufalme wa Mungu; ujio wa ufalme wa Mungu; Ujio wa Kwanza/Pili wa Masihi; zama za Masihi; utukufu (Usajifu) wa Mungu; Mungu kama Jaji; Mungu Bwana; lengo la Mungu la umoja; jamii ya Wanadamu na Mungu; Milenia; Utume wa Yesu Kristo; Mapenzi ya Mungu katika AK

Ufafanuzi kwa Dhima: Mika 4:1-3; Yer. 17:5; Isa 27:13; Luka 24:47; Zab. 146:3; Yer. 3:17; Mdo. 2:17; Isa 13:6; Yoeli 1:15; Isa 56:7.

Amri Fanani: Mik. 4:1-3; Luka 23:30; Kumb. 18:10-14; Hosea 10:8; Ufu. 6:15-16; Yer. 31:6; 50:5; Ayubu 40:13

Teofania: Mik. 1:3; Zab. 18:6-15; Hab. 3:3-14; Yoeli 3:16

23-BSG-2D: UTANGULIZI WA SURA

“Isaya 2:5–21 hujikita katika hali ya kidini na kushindwa kwa miungu ya uongo; 3:1–4:1 hudurusu anguko la jamii tengamano kwa sababu ya hali ya ndani ya kuzorota kwa maadili. Mabano au kijumuishi husika huundwa kwa mashairi mawili adhimu, kuanzia kile ambacho Sayuni ilikusudiwa kuwa (2:2–4) na kuishia kile ambacho Sayuni itakuwa punde (4:2–6). Sura za 2–4 hushabihiana na sura ya 1, siyo tu katika maudhui, bali pia katika falsafa dahili (husika). Kazi ya mwanadamu daima ni uharibifu, pamoja na ufaradhi (hali ya kutoepukika) bayana: malengo kama vile kutengeneza pesa (2:7ab), au usalama kupitia silaha (2:7cd), huchangia sana kuharakisha ujio wa siku ya hukumu kama ilivyo kutengeneza na kuiabudu miungu (2:8); juhudi bora za binadamu katika kuunda jamii salama hukabiliwa na ‘uharibifu’ wa kiungu (3:1–7) kwa sababu ya kutotambua utakilifu (hatari kubwa) wa dhambi ya mazungumko (3:8), ni kile ambacho kingedhaniwa kuwa ufahari usiokuwa na madhara wa kabati lililosheheni mavazi na mapambo (3:16–23) kwa kweli huakisi ubatili na upuuzi wa kilimwengu. Lakini kamwe Bwana hastaajabishwi. Sayuni hukabiliwa na ghadhabu isiyoepukika, lakini Sayuni itakombolewa. Bado Bwana atatimiza muwala ambao watu Wake waliupotoa.” [J. Alec Motyer, Isaiah: An Introduction and Commentary, Tyndale Old Testament Commentaries, (Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1999), 20:57–58].

23-BSG-2J: MASWALI NA MAJIBU

KUONA KILICHOPO

[1] Nini maudhui makuu katika sura hii?

[2] Je sura hii inazungumza nini kuhusu Mungu?

TAMBUA KIINI:

[3] Siku za mwisho ni zipi? (2:2) – kimsingi “sehemu za mwisho za siku”. Sehemu za mwisho za siku zilianza kwa ujio wa kwanza wa Kristo (Ebr. 9:26; 1 Kor. 10:11). Kipindi hiki kitafikia tamati kwa ujio wa pili wa Kristo. Kirai husika kimetumiwa katika AK kwa ajili ya wakati ambapo wokovu wa kimasihi ungetimizwa. Katika Agano Jipya, kirahi hicho kinahusika bayana katika wakati baada ya ujio wa kwanza wa (Mdo. 2:17; Ebr. 1:2; Yak. 5:3; 1 Pet 1:5, 20; 2 Pet 3:3; 1 Yn. 2:18).

[4] Upi ni mlilma wa nyumba ya Yehova? (2:2) Mlima Sayuni.

[5] Kwa nini uliitwa mlima mrefu kuliko yote? (2:2) “Zaburi 48:1–2 hurejelea Sayunu kama Mlima mtakatifu wa Mungu, na husifu kimo chake. Taswira ya Yerusalemu au Sayuni kama mlima mrefu sana pia hujitokeza katika Zab. 78:68–69; Eze. 40:2; na Zek. 14:10. Waisraeli zamani waliitazama Sayuni kama mahali nadhimu kwa ajili ya ibada katika ulimwengu wa kale.” (Faithlife Study Bible)

[4] Ni wapi sheria na neno la BWANA vitatokea? (3) Kutoka Sayuni.

[5] Nini itakuwa kazi ya hekalu la Bwana (kanisa) katika siku za mwisho? (2:2–3)

 • Patakuwa mahali makini na muhimu duniani; watu watapakimbilia
 • Patawavutia na kuwaalika watu kuja kwa BWANA
 • Patawaamsha watu walisikie na kulitii Neno la Mungu
 • Pataleta amani dunia: watakalibu panga zao kuwa plau

[6] Nini ambacho mataifa hawatajifunza tena? (2:4e) Vita – “Taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.”

[7] Je unabii huu humaanisha kwamba ulimwengu utakuwa bora na wala si kuharibika zaidi? (2:4) “Bila shaka—pale Kristo atakaporejea. Baadhi huona unabii huu kama ubainishi wa utawala wa baadaye wa Kristo duniani. Wengine huona amani iliyoelezewa katika andiko hili kuwa imetimizwa kwa maana ya kiroho kupitia ujio wa Kristo na uzinduzi wa ufalme wa Mungu, ambapo wakati huo utakamilishwa pale Yesu anaporejea. Japo tunajua kwamba hatimaye Mungu ataondoa dhambi zote, na kwa mantikio hiyo, vyanzo vya vita na migogoro mingine, tunapaswa bado kuendelea kufanya kazi tukiitarajia siku hiyo, tukiwasaidia watu na mataifa kusuluhisha tofauti zao (Mat 5:9; Yak. 3:18).” (NIV Quest Study Bible).

[8] Nini maana ya ushirikina na upiga-ramli? (2:6) Ushirikina katika imani au mwenendo wowote unaojikita kwenye tumaini la mhusika katika unasibu au nguvu turufushani zisizo za kisayansi wala mantikifu. Upiga-ramli ni jitihada ya kujipatia urajufu katika suali au hali fulani kwa njia ya usihiri, mchakato au adaa iliyosanifiwa (Wikipedia).

“Wafilisti walitumia ishara, fali, na shaniasili zingine ili kubashiri wakati ujao. Kitendo cha Israeli kutegemea uganga na ramli ulikiuka agano lao na Yehova. Wafilisti walikuwa majirani wa Israeli upande wa magharibi mwa pwani ya Mediteraniani.” (Faithlife Study Bible)

[9] Jinsi gani ufahirishi (dhana ya kupenda kuhodhi mali) na urajilisi (masuala ya vita) uliiathiri Yuda? (2:7–8) Walipoteza imani yao katika sanamu za kibinadamu ambazo hazikuwa na nguvu, mathalani, fedha, dhahabu, hazina, farasi, na magari. “Huabudu kazi ya mikono yao, vitu vilivyofanywa kwa vidole vyao wenyewe.”

[10] Kwa nini Isaya alimwomba Mungu asiisamehe Yuda? (2:9) Kwa sababu ya kiburi. Hawakujinyenyekesha—walikuwa na kiburi na wenye kujikweza wakati huo—lakini siku moja, watanyenyekeshwa wakati wa ujio wa Bwana (Isa. 2:10–12).

“Wakati ule ‘siku ya Bwana’ (v. 12) itakapokuja, wadhambi watakuwa wamevuka muda wa rehema yao nao watakuwa ng’ambo ya uwezekano wa toba (angalia Hosea 13:14; cf. Ebr. 9:28). Mungu hawezi kuwasamehe kwa sababu hawana shauku ya msamaha.” (SDA BC 4:109).

[11] Ni siku gani ambayo Mungu amewawekea akiba wote wenye kiburi na wajikwezao? (2:12) “Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko.” (Mit. 16:18). “Kiburi huwafanya watu wampinge Mungu na kuwaongoza wawatese wanadamu wenzao. Kiburi huwaongoza watu wajizatiti dhidi ya Mungu, wakimshurutisha awe adui yao. Kufuatia hilo, mamlaka ya mbinguni hujipanga dhidi yao. Ni suala la muda tu hadi wanapoangamia, pamoja na kazi zao zote. Isaya aliwaona watu sadikifu wa Mungu wakijivuna na kujitukuza katika mafanikio yao; pia aliwaona wakiwa wamenyenyekeshwa mavumbini mbele ya Muumbaji katika siku ile kuu ya Bwana.” (SDA BC 4:110).

[12] Kwa nini Mungu ainyenyekeshe miti na milima? (2:12–17) “Hadi zama zetu za ghorofa na minara mirefu, hakuna chochote duniani kilichokuwa mashuhuri kuliko mlima mrefu au mti mrefu zaidi, kutegemeana na mandhari ya ukanda husika. Isaya alisema kwamba ishara hizi za ukuu na ustahimilivu zingenyenyekeshwa, ikimaanishwa uwezekano wa kuangamizwa katika siku ambapo Bwana pekee angetukuzwa.” (NIV Quest Study Bible Notes)

[13] Nani atakayetukuzwa? (2:17) Bwana pekee ndiye atakayetukuzwa katika siku hiyo.

23-BSG-2K: MASWALI YA MJADALA

TAFAKARI NA KUJADILI:

 • Ni zipi taswira zinazokumbukwa zaidi ambazo zimewasilishwa kupitia maneno ya sura hii?
 • Ni njozi gani ya wakati ujao aionayo Isaya katika aya ya 1-4?
 • Nini ambacho Isaya anamwomba Mungu atende katika aya ya 5?
 • Ni dhambi na masaibu gani yamebainishwa katika aya ya 6-9?
 • Ungeakibishaje (andika muhtasari) kweli muhimu zilizodhihirishwa katika sura hii kuhusu kusudi la Mungu na mpango wa Mungu kwa ajili ya watu Wake?

KWA USOMAJI ZAIDI: “Kwa maana kutakuwa siku ya Bwana wa majeshi juu ya watu wote wenye kiburi na majivuno, na juu ya yote yaliyoinuka; nayo yatashushwa chini.” (Isaya 2:12) “Dhambi bainifu ya watu ni kiburi—mwelekeo wa kujitegemea sisi wenyewe au vitu tuvipatavyo na kutengeneza, badala ya kumtumainia Mungu. Hatimaye kiburi huleta hukumu. Isaya huanza kwa kauli ya jumla kuhusu hulka majumui ya kiburi katika aya ya 12, na hukuza kwa mifano ya taashira asilia na za kibinadamu ambazo mara nyingi huinuliwa kama vibadala vya Mungu.” Jadili mifano tisa iliyoorodheshwa katika aya ya 12-18.

KUJITATHMINI: Hukumu ya Mungu inapowadia, vitu vyote ambavyo watu huvitegemea kwa ujeuri—nguvu ya kijeshi, mapatano ya kigeni, nguvu ya kiuchumi, na adaa za kidini–havitafaa kitu. Mungu pekee ndiye atatambuliwa kama astahiliye kutegemewa.

KWA AJILI YA UHAI LEO: “Acheni kumtumainia mwanadamu (dhaifu, mnyonge, na afaye) ambaye pumzi yake i katika mianzi ya pua yake (kwa muda mfupi sana); hivi adhaniweje kuwa ana thamani silikivu

[hulka kutoka ndani ya nafsi yake mwenyewe]

Isaya 2:22, AMP)

Hii ni nasihi ya pili na ya mwisho katika sura hii. Nasihi ya kwanza ilikuwa “enendeni pamoja na Bwana” (angalia Isa. 2:5, 22). Acheni kumtumainia mwanadamu [dhaifu, mnyonge, afaye]! “Ikiwa hiyo ndiyo hatima ya watu waovu, kwa nini kuendelea kuwatumaini? Watu wa Mungu walikuwa wakitumainia werevu wao na katika msaada wa majirani zao wapagani. Wanapaswa kumgeukia Mungu na kujipatia kutoka Kwake msaada na nguvu.

Umuhimu wa maneno, “Mwacheni mwanadamu,” ni sawa na ule wa mausia ya Kristo kwa wanafunzi Wake kama ilivyorekodiwa katika Mat. 10:17, “Jihadharini na wanadamu.” Tena na tena Mungu alitaka Israeli isiweke tumaini lao katika nguvu ya kibinadamu, ama yao wenyewe au mataifa yale jirani kama Misri na Ashuri, lakini badala yake wawe na staamani katika kile ambacho Bwana angewatendea na angekuja kuwatendea, kama wangekuwa waaminifu Kwake. Kama ilivyokuwa pale Bahari ya Shamu, pale Yeriko, na mbele ya malango ya Yerusalemu katika siku za Senakeribu, Mungu alithibitisha utoshelevu wa nguvu ya kiungu.” (SDA BC 411)

Kwa nini hatuna budi kuacha kumtegemea mwanadamu? Kwa sababu pumzi yake imtokapo, uhai hukoma. “Lazima watu wapumue ili waishi. Mungu alimpulizia uhai mwanadamu wa kwanza, Adamu (Mwa. 2:7). Mungu pekee ndiye anaweza kuwa msaada wa kudumu kwa sababu akiwa nafsi wa milele, hazuiliwi kwa mauti. Yeye ndiye awezaye kuitwaa pumzi na kutupatia. Linganisha Ayubu 7:7.” (Faithlife Study Bible) Kwa nini uvitegemee viumbe halifa (silika ifikwayo umauti), nyonge kwa ajili ya msaada wakati ambapo Mungu ametupatia mwongozo na nguvu?

KUCHUNGUZA KWA KINA ZAIDI:

Ni kwa njia zipi njozi ya Yerusalemu Mpya katika Ufu. 21 ni utimizwaji wa maneno ya kinabii ya Isaya katika aya nne za kwanza za sura hii?

UMUHIMU KWA MTU BINAFSI:

Ungeakibishaje kile ambacho sura hii hutuambia zaidi kuhusu kusudi na mpango wa Mungu kwa watu Wake?

23-BSG-2Y: MSAHALA WA JIONI

Wazo la Usiku Linaloshabihiana na “Mpango wa Usomaji Biblia” wa leo: Isaya 2/ Dhima: Sayuni Tukufu ya Siku za Mwisho: a Kimasihi/ 23-BSG-2Y, (Isaya 2:2-5)/ Wimbo: Come, we that love the Lord, and let our joys be known (SDAH 422)

Isaya 2:2–5— 2 Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi. 3 Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana, nyumbani kwa Mungu wa Yakobo, Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. 4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. 5 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana.

UCHUNGUZI: Ahadi ya Mji Mtukufu: mlima wa nyumba ya Yehova (Isaya 2:2-5).

KUTUKUZWA KWA SAYUNI: [1] Kipindi cha Wakati (2:2a): Na itakuwa katika siku za mwisho … Isaya alitazama hadi ng’ambo ya hukumu ya sasa juu ya Yerusalemu hadi katika siku za mwisho (kimsingi, sehemu za mwisho za siku za mwisho). Sehemu za mwisho za siku zilianza kwa ujio wa kwanza wa Kristo (Ebr. 9:26; 1 Kor. 10:11). Kipindi hiki kitafikia tamati kwa ujio wa pili wa Kristo. Kirai husika kimetumiwa katika AK kwa ajili ya wakati ambapo wokovu wa kimasihi ungetimizwa. Katika Agano Jipya, kirahi hicho kinahusika bayana katika wakati baada ya ujio wa kwanza wa (Mdo. 2:17; Ebr. 1:2; Yak. 5:3; 1 Pet 1:5, 20; 2 Pet 3:3; 1 Yn. 2:18).

[2] Shabaha kuu (2:2b): Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima. Mlima wa nyumba ya mlima wa Yehova ni mlima uliokaliwa na hekalu la Mungu. Isaya anaona mlima huu ukitukuzwa juu ya mingine yote. Mara nyingi katika unabii milima huwakilisha falme. Hekalu mlimani hapa huonesha kwamba ufalme wa Mungu ni wa kiroho. Maandiko haya husisitiza uadhama wa kiroho wa Mlima Sayuni. Ndio chanzo pekee cha mafundisho ya kiungu kwa ajili ya mataifa. Utukuzwaji wa Mlima Sayuni huoneshwa pia katika mafunuo mengine ya unabii (Eze. 40:2; Zek. 14:10; cf. Isa 68:15-18). Kitenzi “imarisha” (utaweka imara) hutalibu usalama na udawamu.

[3] Tendo (2:2c): Mataifa yote watauendea makundi makundi. Nafasi mashuhuri ya Mlima Sayuni huvutia mataifa mengine. Wamaifa watabubuja kwenda kwenye mlima huo mtakatifu, kama ambavyo walimiminika kwenda Babali katika siku za Yeremia (Yer. 51:44). Kitenzi husika hudokeza kutiririka kwa mto mkuu. Mto huo, hata hivyo, unakwea mlimani. Haitakuwa pasi ugumu kwamba Wamataifa watampokea Mungu wa Biblia. Manabii waliwamithilisha na mito mikuu watesi jahili wa Yerusalemu za AK (cf. 8:6-8). Hapa mto utiririkao kuingia Yerusalemu ni mkondo wa Mataifa waongofu.

MVUTO WA SAYUNI: [1] Ari (2:3a): Watu wengi watakuja na kusema, “Njoni, twende juu mlimani kwa Bwana.” Lugha hii inawasilisha dhana ya ari. Watu wengi—mataifa na lugha mbalimbali—kwa shauku watahamasishana kuja katika mlima wa Yehova (Mlima Sayuni), nyumba (hekalu) la Mungu. Rejea husika ni ya Mlima Sayuni wa kimasihi (Ebr. 12:22) na kwa hekalu la AJ, kanisa la Kristo.

[2] Maelezo (2:3b): Naye atatufundisha njia Zake, nasi tutakwenda katika mapito Yake. Katika nyakati za AK, kawaida wageni walikaribia Yerusalemu wakiwa na nia ya kunyang’anya na kuteka. Isaya huwatazama wakija katika zama za Masihi kwa sababu wanajua kwamba Mlimani Sayuni njaa yao ya kiroho itatoshelezwa. Andiko hili halisemi chochote kuhusu Mfalme wa kimasihi, lakini mafunuo ya awali ya unabii yalizungumzia uwalishwaji Wake kwenye Mlima Sayuni (Zab. 2:6). Sayuni ni chanzo cha ukweli wa kiroho. Wamaifa wana njaa ya kujua hata baadhi ya njia za Mungu wa Israeli. Wanatamani kutembea katika njia Zake, yaani, kuishi maisha yao kadiri ya maagizo Yake. Katika 1:10 Israeli inaliasi neno la Yehova; hapa Wamataifa wanalitafuta.

UTUME WA SAYUNI (2:3b): Maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la Bwana katika Yerusalemu. Shauku ya Wamataifa ya kuja Sayuni huchochewa kwa huduma ya kiinjilisti ya wale ambao tayari wanakaa humo. Sayuni itakuwa kiini cha mafundisho ya kidini kwa ulimwengu wote. Katika Sayuni ya kimasihi itatoka sheria (torah) na neno la Yehova litaondoka. Lazima mtu fulani apeleke ujumbe huo. Rejea husika ni kwa wahubiri wale wanaowasilisha ujumbe wa injili ulimwenguni.

MAANA YA KIIBADA: Mlima wa nyumba ya Yehova (ASV), Isa 2:2 ni “Mlima Moria (uliokuja kuitwa Sayuni), ambapo Hekalu la Sulemani lilijengwa. Lakini Hekalu halisi lilikuwa mfano wa hekalu la kiroho—Kanisa la AJ, au mwili wa Kristo (Efe. 2:21), mnara wa nuru ya ushuhuda wa kiungu kwa ulimwengu. Kwa hiyo ukusanywaji wa mataifa kwenda Yerusalemu katika imani yenye shauku huashiria uongofu wa mataifa. Lakini kwa vile tukio hutajwa kutokea katika siku za mwisho, na kwa vile tunafundishwa na Maandiko mengine kwamba Ufalme wa Mungu hatimaye utashinda falme zote za ulimwengu huu, lazima basi tutazamie wakati wa marejeo ya Kristo, mwisho wa zama za sasa, kwa ajili ya utimilizwaji mkuu wa unabii huu. Katika andiko hili tunapewa kidokezo cha lengo kuu la mwisho la Mungu kwa Israeli na kwa ajili ya jamii ya wanadamu. Ufalme wa Mungu utatukuzwa juu ya ufalme vilima vya ulimwengu huu (Dan 2:35).” [Charles F. Pfeiffer, The Wycliffe Bible Commentary: Old Testament, (Chicago: Moody Press, 1962), Is 2:2].

Kutoka wakati ujao mtukufu wa Sayuni, Isaya anarejea kwenye wakati dhalili wa Sayuni wa sasa. Nasihi: (2:5): Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana. Isaya alitumia taswira za kusisimua kuhusu mvuto wa Sayuni ujao ili kuwahimiza watu wa wakati wake kuenenda katika nuru ya Yehova. Watu wa Mungu walikuwa wakienenda gizani, yaani, walikuwa wakilipuuza neno la Mungu. Ikiwa wakati ujao Wamataifa wanakuja kwa Yehova, ni mara ngapi zaidi Israeli wanapaswa kuenenda katika nuru hiyo ambayo ni urithi wake.

Iweni na Usiku Mwema: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.” (Ufunuo 18:1)