Methali 28: Mwongozo wa Biblia.

20-BSG-28A: MWONGOZO WA IBADA.

Mwongozo wa Ibada unaoshabihiana na “Mpango wa Usomaji wa Biblia” wa leo: Mithali 28/ Dhima: Haki/ 20-BSG-28A, (Mithali 28:1-28)/ Wimbo: “Yesu, wewe ndiwe Haki Yangu” [Mtunzi: Charles Wesley]

UCHUNGUZI: Mungu anahitaji watu Wake wawe wenye Haki—(Isa 1:16-17; 56:1; Yer 22:3; Hos 10:12; Zef 2:3; Mt 5:6; Mt 6:33; Efe 6:14; 1 Tim 6:11; 2 Tim 2:22)

TAFAKARI: Sehemu ya kwanza ya sura hii (aya. 1-12) inaonesha sifa za wenye haki na waovu. Hakika wacha Mungu ni wenye hekima, bidii, na wanyofu. Waovu ni wapumbavu, wavivu, au wenye udanganyifu. Tutajadili zaidi juu ya waovu katika kipengele kitakachofuata.

Hebu tujikite katika kundi la wenye Haki. Menye haki ni kama simba (28:1); anaelewa uasi na hudumisha utaratibu (28:2); huishika sheria ya Mungu na hupinga waovu (28:4); humtafuta Bwana na kudumisha haki (28:5); huchagua uadilifu na umaskini dhidi ya faida ya kipato chahila (28:6); ni mtambuzi na mtiifu wa sheria ya Mungu (28:7); hana lawama –atakuwa na urithi mzuri (28:10); ni masikini lakini mwenye hekima—ana ufahamu kwa sababu anamtegemea Mungu (28:11); yeye hushinda na kutawala kwa haki (28:11).

MAANA YA KIIBADA: Wapendwa, hekima ni “kumcha Bwana!” (Mithali 9:10). Kwa kuwa Bwana ndiye “Mwenye Haki” (Zab. 145:17), mtu mwenye hekima ataifanya haki [au utakatifu] kuwa lengo lake kuu katika maisha ya binafsi na ya umma. Mtu mwenye hekima atakuwa mwangalifu kutoivunja sheria ya Yehova. Endapo atajikwaa na kuanguka; ataungama, ataachana na dhambi zake – toba — na atapata huruma na rehema kutoka kwa Bwana (Mithali 28:13).

SAUTI YA INJILI: Kipengele hiki kimeandikwa kana kwamba Mungu anaongea nawe moja kwa moja –kwa sababu hufanya hivyo. Je Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, kuna makundi mawili katika sura hii, njia mbili: Haki na Uovu. Asubuhi ya leo ninakualika kuchagua kundi la wenye haki. Je, uko tayari kushika Sheria Zangu? Sikiliza: Sheria Yangu ni kamilifu — huiburudisha nafsi; Ushuhuda Wangu ni amini,– Humtia mjinga hekima; Maagizo Yangu ni ya adili –Huufurahisha moyo; Amri Zangu ni safi –Huyatia macho nuru. (Zaburi 19:7-8). Jitahidi basi kuwa mwenye haki, mtakatifu. Tii Amri Zangu nawe utabarikiwa na hatimaye utaurithi Uzima wa Milele ninaoandaa kwa ajili yako.

SHAUKU YANGU: Kwa neema ya Mungu, ninakata shauri kutii sheria ya Mungu na kuenenda kwa haki katika maisha ya kibinafsi na ya umma. Ee Bwana nisaidie kuwa mtiifu Kwako. Amina.

Iweni na Alfajiri Njema: “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.” (Ufunuo 22:14)

MASWALI NA MAJIBU.

[1] Ni ujasiri upi walionao wenye haki? (28:1) Wao ni kama kama simba.

[2] Nani anasifu waovu? (28:4) Wale walioweka sheria ya Mungu kando.

[3] “Watu wabaya hawaelewi haki/ Hukumu.” Je, waumini wanawezakuwa wanasiasa bora? (28:5) Ndiyo/ Hapana. Yusufu na Danieli, kwa mfano, walifanya kazi katika serikali za wapagani, lakini walisimamia haki na sheria ya Mungu.

[4] Sala ya nani ni chukizo? (28:9) Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria ya Mungu. – Linganisha Maandiko haya: “Tazama, mkono wa Bwana haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia; lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.” (Isaya 59:1-2)

[5] Nini kitatokea kwa yule amsababishiaye mwenye haki kupotea? (28:10) Ataanguka katika shimo lake mwenyewe.

[6] Njia gani ni bora Zaidi kuhusu kutubu dhambi? (28:13) “Watu wa Mungu wanapaswa kukubali na kukiri dhambi zao kwa uwazi. Ingawa Mungu anajua pale wanapokosa, anawataka waweze kukiri dhambi hizo. Sala za Daudi katika Zaburi 32 na 51 zinatoa mfano mzuri wa kuungama dhambi kwa Mungu. Zaburi hizi, pamoja na 1 Yohana 1:6-9, zinaonesha thamani ya kutambua dhambi zetu: tunapokiri mapema, mapema twaweza kupata uzoefu wa msamaha wa Mungu.” (NIV Quest Study Bible)

[7] Nani hawatafanikiwa? (28:13) Yeye aliyeficha dhambi zake. “Kukiri na kuachana na dhambi ndio ufafanuzi wa toba. Mtu ambaye hupata ‘rehema’ atafanikiwa katika hali halisi ya mwisho katika umilele.” [David K. Stabnow, CSB Study Bible: Notes, 2017, 997].

[8] Inamaana gani kufanya mgumu moyo? (28:14) Ni pale tunapoazimia kupingana na njia za Mungu na Neno, Amri Zake; Tunapofanya udhuru dhidi ya dhambi zetu; Ni pale tunapopinga kazi ya usadikisho ya Roho Mtakatifu (Yohana 16:8-11), na pale ambapo hatuna hamu tena ya haki [utakatifu] katika mioyo yetu, au msukumo wa kutubu.

[9] Mtawala mwovu anafananishwa na nini? (28:15) Simba angurumaye; dubu mwenye njaa… kwa watu masikini.

[10] Nani atakuwa na mkate mwingi? (28:19) Yeye alimaye shamba lake. (Hatupaswi kuwa wavivu; tunapaswa kuwa na juhudi katika kazi ya mikono yetu)

[11] Kitu gani si kizuri? (28:21) Upendeleo: Kupendelea watu si kwema!

[12] Nini kitatokea kwa yule afanyaye upesi kuwa tajiri? (28:22) Umaskini utakuja juu yake.

[13] Nani anaelezwa kuwa mwenzi wa mwangamizi? (28:24) Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa.

[14] Kwa nini kujiamini sana ni upumbavu? (28:26) Kwa sababu hakuna mtu ye yote ajuaye ya kesho –(rejea somo la jana, “Wazo la Usiku”). Ni lazima tujifunze kumtegemea Mungu. “Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.” (Mithali 28:26)

[15] Nani ambaye hatapungukiwa? (28:27) Yeye ampaye maskini. “Amhurumiaye maskini humkopesha Bwana; Naye atamlipa kwa tendo lake jema.” (Mithali 19:17)