Mithali 27: Mwongozo wa Biblia.

20-BSG-27J: MASWALI NA MAJIBU.

KUONA KILICHOPO.

[1] Nini maudhui makuu ya sura hii? Wajibu unayoongoza Tabia.

  • Jihadharini na dhambi nne (1-4).
  • Kuza urafiki (5-10).
  • Fuata ushauri wa mzazi wako (11-22).
  • Kuwa na bidii sana katika kulinda mapato na rasilimali zako (23-27).

[2] Sura hii inasema nini juu ya Mungu? Mungu anatutaka tumtegemee kikamilifu. Tunapaswa kuongelea kesho kama wale waliowasilisha mapenzi yao kwa Mungu. Ni lazima kutumia muda wa sasa (leo) kwa bidii na hekima kwa sababu hakuna ajuaye ya kesho.

PATA KIINI.

[3] Ni kitu gani ambacho hupaswi kujisifu kwacho? (27:1) Kesho. Lazima tujihadhari na ujasiri kuhusu kesho: kesho haijulikani! Mwenyezi Mungu pekee ndiye ajuaye yajayo!

[4] Badala ya kujivunia kesho, Je, tunapaswa kufanya nini? Tunahitaji kujifunza umuhimu wa maisha ya imani na utegemezi kwa Mungu. Haikukusudiwa kabisa kwa mwanadamu kujitegemea (pasipo Mungu). Ni lazima tujifunze kukuza roho ya unyenyekevu, na utegemezi wa mapenzi ya Mungu kwetu.

[5] Kwa nini ni afadhali kuruhusu mtu mwingine akusifu? (27:2) “Kama unastahili sifa, mtu mwingine atabaini na atakusifu. Lakini kama unajisifu, na kutenda kwa kiburi yawezekana ukawachosha wengine. Mbali na hilo, sifa za wengine hubeba uzito zaidi, kwa kuwa watabaini ukweli wa mafanikio, tabia na maadili yako” (NIV Quest Study Bible)

[6] Ni kitu gani kilicho bora kuliko busu la adui? (27:5-6) Karipio/ maonyo ya wazi; Majeraha ya rafiki.

[7] Tunawezaje kuwa na Imani kuhusu majeraha kutoka kwa rafiki? (27:6) Majeraha kutoka kwa rafiki ni ‘makaripio’ au ukosoaji wenye nia ya kuturekebisha sisi. – “Kipuli cha dhahabu, na pambo la dhahabu safi; Ndivyo alivyo mwonyaji mwenye hekima kwa sikio lisikialo.” (Mithali 25:12). Hata kama yanaweza kuwa machungu, maonyo hayo ni faida zaidi kwetu kuliko udanganyifu au (kupakwa mafuta) na adui.

[8] Tutawezaje kubaini marafiki wa kweli? (17:17). “Rafiki wa kweli atatupenda wakati wa tabu na raha. Kwa kweli, rangi za kweli za rafiki ni mara nyingi hujidhihirisha tunapopitia changamoto ngumu na chungu katika maisha …. Marafiki wa kweli wakati mwingine hututupa. Watakuwa radhi kutuambia ukweli ngumu, hata kama ni machungu kiasi gani. Tunaweza kuamini maoni yao ya uaminifu, lakini adui huleta busu (27:6). Jihadhari sana na mtu ambaye hana ujasiri wa kukabiliana nawe (kukukaripia) hususan pale unapokosea” (NIV Quest Study Bible)

[9] Nani hupaswi kumsahau? (27:10) Rafiki yako; au rafiki wa baba yako.

[10] Nini unatakiwa kuwa na bidii ya kujua? (27:23) Jua hali ya mifugo yako; Hudumia mifugo yako

[11] Ni kitu gani kisicho na ukomo? (27:24) Utajiri; pia, kumbuka kuwa “Taji” (ukubwa, cheo, umashuhuri) hautadumu vizazi vyote. Hebu kuwa mnyenyekevu kwa Mungu na kwa wanadamu wenzako.