Yesu na Sabato, Seh 1.

SABATO KATIKA VITABU VYA INJILI. Yesu na Sabato, Seh 1./ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Sabato katika Agano Jipya: Vitabu vya Injili/ 86-020, (Mathayo 5:17) / Andiko Msingi: “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.” (Mathayo 5:17)

Malengo ya Somo: Kudurusu matukio makuu ambapo Yesu alifundisha kwa mfano, kwa neno, na kupitia miujiza ya uponyaji, kiini cha uadhimishaji Sabato ya kweli. Leo tutajikita kwenye mfano wa Kristo wa kuhudhuria ibada siku ya Sabato.

Maelezo ya Ufunguzi: Akthari ya Wakristo wengi leo hudai kwamba si lazima tena kuishika Sabato ya siku ya saba ya Biblia—kwamba Sabato ilikuwa “kivuli cha mambo yajayo,” na hivyo Kristo alipokufa, Sabato “ikagongomewa msalabani;” kwamba Jumamosi ambapo mwili wa Yesu ulikuwa kaburini ilikuwa “Sabato rasmi ya mwisho” (Kol. 2:16–17); kwamba waumini wote wanapaswa kuishika Jumapili [siku ya kwanza ya juma] katika kuheshimu ufufuo wa Yesu Kristo. Sababu zote hizi husikika kuwa adhimu lakini, hivi ni za kibiblia, au zimetolewa nje ya muktadha? Mara nyingi sana tunasikia Matendo 20:7; 1 Kor. 16:2; Ufu. 1:10, nk., kama uhalalisho wa utakatifu wa Jumapili. Je maandiko haya yanasema, endapo kuna lolote, kwamba Mungu alibadili siku ya ibada kutoka Sabato kwenda Jumapili? Jibu ni “Hapana” thabiti.

Kwa vile wengi humtumia Kristo (mathalani, ufufuo Wake) ili kuhesabiwa hakialalisha dai lao, ni muhimu sana basi kwamba tuwe na somo la kina, tukichunguza mwenendo wa Kristo kuhusu mada ya Sabato. Hata hivyo, Kristo ndiye Mwasisi wa Sabato (Mwa. 2:1-3); Yeye ni “Bwana wa Sabato” (Mat. 12:8). Endapo Yeye ni Bwana wa Sabato, ninahakika atakuwa na kitu fulani cha kusema, na kutufundisha kuhusu mada hii ya maandiko iliyo makini na inayojadiliwa zaidi.

Zingatia: Baadhi ya rejea juu ya Sabato katika vitabu vyetu vinne vya Injili havina utata wowote kati ya Kristo na Marabi/Mafarisayo; wakati ambapo mengine yanao. Tutaanza na “Kristo na Sabato katika Mazingira Yasiyo Utata.” Somo hili hijikita katika mahudhurio ya Yesu kwenye sinagogi. Masomo yajayo yatasisitiza matukio ya Yesu ya awali kabisa kurekodiwa; mashauri ya Kristo kuhusu Sabato katika Mathayo 24:20; na uadhimishaji wa Sabato wakati Yesu akiwa kaburini, Luka 23:54–56.

MASWALI YA MSINGI

[1] Nini chanzo fusili (timilifu) cha kweli?  Nini kiwango fusili cha maadili? Nini utawala fusili wa haki? Jibu ni ‘Sheria ya Mungu.’

Hili ni swali ambalo sisi sote hatuna budi kulijibu, na tunapaswa kulijibu kisahihi. Sheria ya Mungu ni kiwango cha maisha. Sheria ya Mungu ina ufusili wake/mamlaka isiyobadilika—kwa sababu ya asili yake: hutoka katika Chanzo Taabadi—Mungu Mwenyewe.

Kwa mtazamo wa kiteolojia, neno ‘Sheria’ huwa hata muhimu zaidi kwamba sababu linajumuisha Sheria ya Mungu – [Amri Kumi]. Katika Sheria hii, maagizo ya Mungu yamekusudiwa kwa ajili ya wanadamu wote, katika vazazi vyote.  

[2] Je Kristo alifundisha nini kuhusu uendelevu wa Sheria ya Mungu? Ingeendelea bila kubadilika. “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.” (Mathayo 5:17–19) “Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.” (Luka 16:17)

[3] Ni kwa jinsi gani ukweli huo ungeiathiri Sabato? Kwa vile Sheria ya Mungu ingedumu bila kubadilika, basi mtu anaweza kuhitimisha kwamba Sabato (amri ya nne) ingeendelea bila kubadilika vilevile.

[4] Je Sabato ilifanyika kwa ajili ya nani? “And He said to them, “The Sabbath was made for man, and not man for the Sabbath.” (Marko 2:27) Kristo alifundisha kwamba Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, ambapo hujumuisha jamii yote ya wanadamu.

Neno mwanadamu, Kiyunani anthrōpos, kimsingi, “mtu,” istilahi majumui iwahusuyo wanaume, wanawake, na watoto (angalia katika Marko 6:44). “Jamii ya wanadamu” huweza kuakisi maana ya anthrōpos kisahihi zaidi. Sabato ilikusudiwa na kuasisiwa na Muumbaji mwenye upendo kwa ajili ya maslahi bora ya jamii ya wanadamu. Ni kwa njia tu ya kupotosha fikra ndipo mtu anaweza kudhani Sabato iko “dhidi” ya mwanadamu vyovyote vile (angalia katika Kol. 2:14). [SDA BC 5:588].

[5] Jadili jinsi Yesu Kristo alivyofanya kazi na kuishika Sabato. Akiwa huko Nazareti, alikokuwa amelelewa alifanya kazi ya useremala (Marko 6:3; Mat 13:35), lakini katika siku ya saba ya juma [Sabato] alipumzika na kuhudhuria ibada; na hivyo alishika Sabato (Luka 4:1).

[6] Ni siku gani ya juma ambapo Yesu alienda kanisani? Siku ya saba. Yesu alihudhuria sinagogi katika siku ya Sabato. Zingatia maandiko yafuatayo:

 • “Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya Sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.” (Marko 1:21)
 • Na ilipokuwa Sabato, alianza kufundisha katika sinagogi; wengi waliposikia wakashangaa, wakisema, Huyu ameyapata wapi haya? Na, Ni hekima gani hii aliyopewa Huyu? Na, Ni nini miujiza hii mikubwa inayotendeka kwa mikono Yake?” (Marko 6:2)
 • “Hivyo akaja Nazareti, hapo alipolelewa. Na kama ilivyokuwa desturi Yake, akaingia katika sinagogi siku ya Sabato, kisha akasimama ili asome.” (Luka 4:16)
 • “Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya Sabato. (Luka 4:31)
 • Siku ya Sabato alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo.” (Luka 13:10)

Kwa mujibu wa Luka 4:16, “desturi” Yake ilikuwa kwenda kwenye sinagogi siku ya Sabato. Kwa kuhudhuria sinagogi, Yesu alidhihirisha mwenendo Wake chanya kuhusu Sabato kama muda wa kusanyiko takatifu: “Mtafanya kazi siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, kusanyiko takatifu; msifanye kazi ya namna yoyote; ni Sabato kwa Bwana katika makao yenu yote.” (Walawi 23:3)

[7] Je Luka kwa namna mahususi hubainisha Sabato kama siku ya saba ya juma? Ndiyo.  “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.” (Luka 24:1)

“Ufufuo ulitokea siku ya kwanza ya juma katika kutimiza utabiri wa Yesu kwamba angekuwa “siku tatu mchana na usiku katika moyo wa nchi” (Mat. 12:40; linganisha 27:63; Marko 8:31; 9:31; 10:33–34). Wayahudi hawakuwa na majina kwa ajili ya siku za juma, ila walizihesabu kwa uhusiano na Sabato, siku ya saba ya juma. Kwa hiyo, siku ya kwanza, ilikuwa Jumapili, siku baada ya Sabato.” [John MacArthur, Luke 18–24, MacArthur New Testament Commentary, (Chicago, IL: Moody Publishers, 2014), 409].

Kwa namna mahususi Luka hutaja Ijumaa, siku ya “maandalio” (Luka 23:54), siku ya Sabato (Luka 23:54, 56), na “siku ya kwanza ya juma” (Luka 24:1). Hapawezi kuwepo swali kuhusu mpangilio wa siku hizi au utambulisho wao. Kristo alisulubiwa Ijumaa, akapumzika kaburini Sabato yote, baada ya kukamilisha kazi ya ukombozi (angalia katika Mwa. 2:2, 3; Eze. 20:20), na kufufuka siku iliyofuata, siku ya kwanza ya juma.

[8] Je Yesu alifanya nini alipoingia kwenye sinagogi? Alisimama ili asome (Luka 4:16)

“Ilitarajiwa kwamba Yesu angeombwa kusoma Maandiko na kuhubiri pale ambapo angerejea Nazareti, jukumu ambalo Mwisraeli yeyote mwenye sifa, hata wale walio chini ya umri, angeitwa kufanya. Mara nyingi alikuwa ameombwa kufanya hivyo akiwa Mtoto (DA 74), na sifa Yake kama mhubiri huko Uyahudi (angalia Yohana 3:26; DA 181) sasa iliwafanya watu wa mji Wake wawe na shauku ya kusikiza alichotaka kusema. Yule aliyesoma maandiko teule kutoka kwa Manabii alitarajiwa pia kuwasilisha hubiri.” (SDA BC 5:727).

[9] Kwa nini Yesu alisimama ili asome (Marko 4:16)? Watu walisimama ili kusoma Maandiko ili kuonesha ustahivu wao kwayo. Ustahivu kwa Neno lililoandikwa huhitaji kwamba yule alisomaye hadharani asimame. Lakini waliketi ili kufundisha, hii ikitofautisha maelezo yao na Maandiko yenyewe.

[10] Upi ulikuwa mtazamo wa wanafunzi, na wanawake kuhusu Sabato hata siku ile Yesu alipokufa? Walifanya nini? “[Wanawake hao] Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya Sabato walistarehe kama ilivyoamriwa. (Luka 23:56) “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari.” (Luka 24:1)

“Fasiri hii huweka bayana sana utauwa wa waumini Wakristo hawa wa awali kuhusu Sabato ya siku ya saba. Tendo lao la mwisho Ijumaa ilikuwa kuandaa “manukato na marhamu” (sura ya 23:56). Kisha wakaacha kila kitu “kama ilivyoamriwa (katika Sabato)” (angalia katika Kut. 20:8–11), nao hawakurejea kazi yao ya upendo hadi alfajiri Jumapili. Tofauti kubwa kati ya utakatifu wa Sabato na hali ya kilimwengu ya Jumapili ambayo imeoneshwa kwenye maelezo ya injili hunena kifasaha kwa Wakristo leo.” [Francis D. Nichol, Ed., The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, (Review and Herald Publishing Association, 1980), 5:880–881].

MAANA YA KIIBADA: “Ukweli kwamba, alipokuwa hapa duniani, Yeye binafsi aliadhimisha siku husika ya juma kama walivyofanya Wahudi, pia ni ushahidi kwamba wakati haukuwa umepotezwa tangu uwasilishwaji wa sheria pale Sinai, au kwa suala hilo tangu uumbaji. Kristo ndiye “Bwana wa Sabato pia” (Marko 2:28); kwamba ndiye aliyeiumba (Mwa. 2:1–3; cf. Marko 2:27) na huidai kama siku Yake. Mfano Wake katika kuiadhimisha kwa kweli ni kielelezo timilifu kwa ajili ya Mkristo kufuata, kuhusu wakati na kama namna ya uadhimishaji husika. Zaidi ya hapo, hapawezi kuwepo swali lolote ila kwamba juma kama tulilo nalo sasa limetufikia katika mfululizo usiovunjika tangu wakati wa Kristo, na uadhimishaji wa siku ya saba ya juma leo ni uadhimishaji wa Sabato kama alivyoishika Kristo. Tangu wakati huo hadi leo wamekuwepo mamilioni ya Wayahudi waliotawanyika katika ulimwengu uliostaarabika, na isingewezekana kwa wote pamoja kufanya kosa lilelile la kushindwa kutambua siku ya saba ya juma.” [Francis D. Nichol, Ed., The Seventh-Day Adventist Bible Commentary, (Review and Herald Publishing Association, 1980), 5:727].

SAUTI YA INJILI: Je Bwana ananiambia nini leo? Kristo anasema: “Kama (kweli)mnanipenda, mtazishika (tii)amri Zangu.” (Yohana 14:15, AMP). Wapendwa, endapo tunampenda Yesu hakika, hatutajihusisha kwenye mijadala isiyokoma kuhusu Sheria Yake, badala yake, tutajitahidi kudumisha, kutii na kushika Sheria Yake (ambayo hujumuisha Sabato ya siku ya saba).

Hebu tukumbuke kitu fulani hapa … “Sheria haikutamkwa … kwa manufaa tu ya Waebrania. Mungu aliwasharifu kama walinzi na watunzaji wa sheria Yake, lakini ilikusudiwa kudumishwa kama amana takatifu kwa ajili ya ulimwengu wote. Kanuni za Dekalojia zimenasibishwa kwa jamii yote ya wanadamu, na zimedhihirishwa kwa ajili ya maelekezo na utawala wa wote. Kanuni kumi, fupi, za kina, na zenye mamlaka, zinahusu wajibu wa mwanadamu kwa Mungu na kwa mwanadamu mwenzake; na zote zimejengwa kwenye kanuni kuu ya msingi ya upendo.” [Ellen Gould White, The Faith I Live By, (Review and Herald Publishing Association, 1958), 86].

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? Mtii Mungu kwa kuzishika amri Zake.

“Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” (Kutoka 20:8–10)

Dokezo Moja la Mwisho: Kauli rahisi ya Luka kwamba kwa desturi Yesu alihudhuria huduma za sinagogi takatifu siku ya Sabato, ambapo huibainisha kwa namna mahususi kama siku ya saba ya juma (Luka 23:56; 24:1), huweka wazi wajibu wa Mkristo ampendaye Muumbaji wake na ambaye angependa kufuata hatua Zake. “Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo Zake” (1 Petro 2:21). Mpendwa, hivi utafuata hatua Zake leo? Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana. Heri wazitiio shuhuda Zake, Wamtafutao kwa moyo wote (Zab. 119:1-2).

SHAUKU YANGU LEO. Chagua Kisanduku kinachoakiasi uamuzi wako leo:

 • Nataka kufuata nyayo za Kristo kwa kuishika Sabato
 • Nataka kumwomba Bwana anisamehe kwa kuivunja Sabato
 • Nataka kujifunza zaidi kuhusu Sabato
 •  Nataka kuwashirikisha wengine ukweli kuhus Sabato
 • Nataka kushika amri zote za Mungu, ikiwa ni pamoja na Sabato
 • Ni shauku yangu ya kumtii Bwana kwa kuidumisha Siku Yake (Sabato ya siku ya saba) kuwa takatifu, Kut. 20:8.

“Tena naliwapa Sabato Zangu, ziwe ishara kati ya Mimi na wao, wapate kujua ya kuwa Mimi, Bwana, Ndimi niwatakasaye [niwatengaye na kuwaweka kando].” (Ezekieli 20:12, AMP)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Sabato: Sabato katika Historia na Maandiko Matakatifu/ Somo # 20.