Uumbaji Wa Malaika.

UUMBAJI WA MALAIKA.

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Fundisho Kuhusu Malaika/ 76-002 (Waebrania 1:14)/ Andiko Msingi: “Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” (Waebrania 1:13–14)

Maelezo ya Ufunguzi: Malaika waliumbwa lini? Pengine malaika waliumbwa mabilioni ya miaka iliyopita. Waliumbwa kabla ya mbingu na dunia kuumbwa (Ayubu 38:4–11). “Wakati wa kuumbwa kwa malaika ni dhana ambayo Biblia haitaji kwa namna mahususi. Uwepo wa malaika huonekana kabla ya kuumbwa kwa wanadamu. Ni zamani kiasi gani hakuna ajuaye. Huonekana kwamba walikuwepo pale dunia ilipoumbwa. Maandiko huonesha kwamba malaika waliimba na kushangilia wakati Mungu akiumba dunia—pengine kabla ya kitu chochote kuumbwa. Ni bayana kwamba waliumbwa kabla ya jamii ya wanadamu. Zaidi ya hili, hakuna taarifa za kutosha kiasi cha kuwa mahususi.” (Don Stewart)

MASWALI NA MAJIBU.
[1] Nini chimbuko la malaika? Malaika siyo viumbe ambao wamekuwepo tangu milele, bali badala yake, waliumbwa na Mungu. Walikuwa na mwanzo, wala hawawezi kufa (Luka 20:36). Wakati fulani hapo zamani, Mungu alitamka na malaika wakawepo.

[2] Je Agano la Kale hufundisha nini kuhusu vile Mungu alivyowaumba malaika?

 • Katika Zaburi 148:2–5, mtunzi wa Zaburi anatamka: “Msifuni, enyi malaika Wake wote; Msifuni, majeshi Yake yote. Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga. Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.” (Zaburi 148:2–5)
 • Vilevile, katika Isaya 44:24, Mungu alitamka kupitia nabii huyu: “Bwana, mkombozi wako, Yeye aliyekuumba tumboni, asema hivi; Mimi ni Bwana, nifanyaye vitu vyote; nizitandaye mbingu peke Yangu; niienezaye nchi; ni nani aliye pamoja Nami?” (Isaya 44:24)

[3] Je malaika waliumbwa lini? Hapo mwanzo! Aya ya kwanza ya Maandiko hutupatia dokezo kuhusu lini malaika waliumbwa. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” (Mwanzo 1:1)

 • Kirai “mbingu na nchi” hurejelea ulimwengu mzima. Hii hujumuisha sehemu zote tofauti. Uumbaji wa malaika huonekana kujumuisha katika kauli hii.

[4] Je malaika waliumbwa lini? Kabla ya uumbaji wa dunia. Japo hatuambiwi ni wakati gani hasa waliumbwa, huonekana kuwa wakati fulani kabla dunia haijaumbwa.

 • Mungu alizungumza na Ayubu akisema: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.” (Ayubu 38:4) “Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?” (Ayubu 38:7)


[5] Je malaika waliumbwa lini? Kabla ya siku ya saba. Jambo moja tunaloweza kuwa na hakika nalo ni kwamba malaika waliumbwa kabla ya siku ya saba ya uumbaji. Biblia inasema: “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote.” (Mwanzo 2:1). Kirai “jeshi lake lote” hubeba dhana ya ujumuishi ambapo ni bayana kabisa malaika wahusishwa.

 • “Malaika ni ngazi ya viumbe wenye maarifa wenye umri mkubwa kuliko mwanadamu. Mafadha waliweka tukio la uumbaji wa malaika kuwa sadfa na tukio la kuumbwa kwa viasili vya awali, pengine wakijenga msingi wa wazo lao katika kitabu cha Apokrifa, Ecclesiasticus 18:1—“Yeye aishiye milele aliumbwa vitu vyote pamoja.” katika Ayubu 38:7, ushabihiano wa Kiebrania hufanya “nyota za asubuhi” kuwa sawa na “wana wa Mungu,” kiasi kwamba malaika huzungumziwa kuwa walikuwepo katika hatua fulani za kazi ya uumbaji wa Mungu. Kutajwa kwa “nyoka” katika Mwa. 3:1 hudokeza juu ya anguko la Shetani kabla ya anguko la mwanadamu. Tunaweza kupambanua kwamba uumbaji wa malaika ulifanyika kabla ya uumbaji wa mwanadamu… Katika Mwa. 2:1, “jeshi lake lote,” alilokuwa ameumba Mungu, huweza kukusudiwa kujumuisha malaika. Mwanadamu alikuwa upeo wa kazi ya uumbaji, aliyeumbwa baada ya malaika kuumbwa.” [Augustus Hopkins Strong, Systematic Theology, (Philadelphia: American Baptist Publication Society, 1907), 446].

[6] Nani aliyewaumba malaika? Yesu Kristo—

 • “Kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia Yake, na kwa ajili Yake. (Wakolosai 1:16)
 • “Haleluya. Msifuni Bwana kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu. Msifuni, enyi malaika Wake wote; Msifuni, majeshi Yake yote. Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga. Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu. Na vilisifu jina la Bwana, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.” (Zaburi 148:1–5) 

[7] Je lini Mungu aliwaumba malaika? Wakati fulani kabla ulimwengu haujaumbwa (Mwa. 1:1).

 • “Kujaribu kubaini wakati gani Mungu aliwaumba malaika kwa namna fulani ni zoezi tata kwa sababu chochote alichofanya Mungu “kabla ya msingi wa ulimwengu, huweka tukio hilo nje ya wakati. Muda na shuhuba (space) ni sifa za ulimwengu wetu, siyo ule wa Mungu. Yeye hafungwi na saa, siku na miaka kama tulivyo sisi. Kwa kweli, Biblia hutuambia kwamba “kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.” (2 Petro 3:8).”
 • “Tunajua kwamba Mungu aliwaumba malaika kabla hajaumba ulimwengu halisi. Kitabu cha Ayubu huwabainisha malaika wakimwabudu Mungu wakati akiumba ulimwengu: “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?” (Ayubu 38:4–7).
 • “Kama tukizingatia kazi ya malaika, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu aliwaumba malaika muda kabla ya uumbaji wa jamii ya wanadamu kwa sababu mojawapo ya wajibu wao ni kuwa “roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu” (Waebrania 1:14). Tunajua pia kwamba walikuwepo kabla ya Bustani ya Edeni, kwa sababu Shetani, ambaye hapo awali alikuwa malaika Lusifa, tayari alikuwemo bustanini katika hali yake ya anguko. Hata hivyo, kwa sababu kazi nyingine ya malaika ni kumwabudu Mungu karibu na enzi Yake (Ufunuo 5:11–14), huenda wamekuwepo tangu mamilioni ya miaka—kabla Mungu hajaumba ulimwengu, wakimwabudu na kumtumikia.”
 • “Hivyo, ingawa Biblia haisemi kwa namna mahususi lini Mungu aliwaumba malaika, tukio hili lilifanyika wakati fulani kabla ulimwengu haujaumbwa; hatuwezi kuwa na hakika ni lini hasa.” [Got Questions Ministries, Got Questions? Bible Questions Answered, (Bellingham, WA: Logos Bible Software, 2002–2013)].

[8] Nini kingine ambacho Biblia husema kuhusu malaika?

 1. Waliumbwa binafsi—hakuna “mailaka papa” ambapo malaika wengine wote walitokea kwake. Malaika siyo jamaa ila kundi (Ebr. 12:22) maana kila mmoja aliumbwa binafsi—(angalia hapa chini kwa ajili ya maelezo zaidi)
 • Waliumbwa watakatifu—Kwa vile Mungu ni mtakatifu (1 Petro 1:16), hawezi kuumba malaika wasio watakatifu. Yuda 6 hutupatia maelezo kuhusu seti nyingi ya malaika—malaika waovu/waasi. Hawa ni wale “wasioilinda enzi yao wenyewe na kumtukuza Mungu, lakini hawakudumisha nafasi yao, bali waliyaacha makao yao yaliyowahusu. Wakati fulani walikuwa salidi, watakatifu, na wakiishi katika uwepo wa Mungu, waliruhusu kiburi na kujiunga na Shetani wakamwasi Mungu.” [Bruce B. Barton, 1 Peter, 2 Peter, Jude, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Pub., 1995), 244].

[9] Ipi mifanano na tofauti kati ya malaika na wanadamu?

 • “Mungu aliwaumba malaika na wanadamu kama viumbe tofauti, nao waliumbwa katika nyakati tofauti. Malaika siyo za wanadamu waliokufa. Malaika hawawi wanadamu, na wanadamu hawawi malaika. Tofauti yao hudumu milele. Wote (malaika na wanadamu) ni waliumbwa, viumbe haladi (hawaishi milele), na ni viumbe wenye ukomo, wanaomtegemea Mungu kwa ajili ya kuendelea kuwepo kwao. Makundi haya mawili huwajibika kwa Mungu kwa matendo yao, na wana ukomo katika uwezo na nafasi zao (Mat. 24:36; Yohana 16:11; 1 Kor. 6:3; Ebr. 9:27). Makundi yote yana hulka kamili ikiwa ni pamoja na akili, utashi, na mhemko; na wote wana uwezo wa kudumisha uhusiano wa mchaa na Mungu. Lakini malaika ni tofauti na wanadamu.”
 • “Malaika wana asili tofauti na wao ni viumbe wa ngazi tofauti (Ebr. 2:5–7). Malaika hawaonekani na wala hawaoi/hawaolewi, hawazaliani, wala kufa (Mat. 22:28–30; Luka 20:36). Malaika ni roho (Ebr. 1:14), na wala hawana miili, mbari, au jinsi (japo katika mionekano yao kwa wanadamu, huonekana kuwa na jinsi zote mbili). Wanadamu ni roho na mwili (Yakobo 2:26). Malaika pia wana uwezo mkuu zaidi wa maarifa, nguvu, na wepesi (2 Petro 2:11). Ni muhimu kukumbuka mifanano na tofauti, hususan wakati wa kuzingatia picha za malaika katika sanaa, tamaduni mashuhuri, na harakati mbalimbali za kidini. Mitazamo haipaswi kamwe kuutwaa ukweli wa Maandiko!” [H. Wayne House and Timothy J. Demy, Answers to Common Questions about Angels & Demons, (Grand Rapids, MI: Kregel Publications, 2011), 20–21].

MAANA YA KIIBADA: Katika Wakolosai 1:16, mtume Paulo anaandika kuhusu Kristo kama Bwana wa uumbaji akifanya vyote vijulikanavyo viweze kuwepo. Kama nafsi ya pili ya Uungu, Kristo kama Mungu alikuwa wakala wa uumbaji wa malaika:Kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia Yake, na kwa ajili Yake.” Waraka wa Paulp kwa Wakristo huko Kolosai, Uturuki ya sasa, uliandikwa sehemu ya madhumuni husika yakiwa kukabiliana na utahafakishaji (fanyia maridhiano, maafikiano) wa teolojia ya Ukristo na dhana za kipagani na upotofu uliotishia uhali wa Ukristo kwenye mji huo. Sehemu ya kosa la kiteolojia lililoenezwa lilikuwa kuwaabudu malaika (2:18), ikiwa ni pamoja na imani kwamba malaika walikuwa dhariri (minunurisho) kutoka kwa Mungu. Sambamba na dhana hii ilikuwa imani kwamba Yesu Kristo hakuwa zaidi ya mpatanishi. Dhana hizi zilikana uungu fanidi wa Kristo. Ilhali akipinga msingi huu wa kizushi, Paulo alihimiza uungu wa Kristo, akimtangaza Yeye kuwa Mungu Muumbaji. Kristo aliumba na kuutegemeza ulimwengu na vyote vilivyomo (Yohana 1:3; Ebr. 1:2, 10), ikiwa ni pamoja na malaika.

Kwa kuwa katika Yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia Yake, na kwa ajili Yake.

Ni muhimu kukumbuka virai vitatu hivi katika Wakolosai 1:16— “katika Yeye … kwa njia Yake … na kwa ajili Yake.” Malaika siyo “mawakala huru” ulimwenguni katika uwepo au utendaji wao. Wanaabudu, wanatumika, na kumtukuza Mungu, nasi pia tunapaswa kufanya vivyo hivyo.” [H. Wayne House and Timothy J. Demy, Answers to Common Questions about Angels & Demons, (Grand Rapids, MI: Kregel Publications, 2011), 17–18].

SAUTI YA INJILI: “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi” (Waebrania 12:22).

“Naamini katika kusanyiko kuu (panēguris, “mjumuiko kwa ajili ya sherehe ya hadhara”) hurejelea jeshi kuu la malaika, badala ya kanisa la uzalio wa kwanza. Fasiri ingeweza kuwa, “Bali ninyi mmekuja kwenye… umati usiohesabika wa malaika katika kusanyiko la karamu.” Tunapokuja Mlima Sayuni katika Yesu Kristo, tunakuja katika kusanyiko kuu la malaika washerehekeao, tunaoungana nao katika kumsifu Mungu. Danieli hutupatia wa idadi ya malaika tutakaoungana nao mbinguni: “maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake” (Dan. 7:10; cf. Ufu. 5:11).”

“Malaika wasiohesabika walikuwepo pia huko Sinai, kama wapatanishi wa agano la Musa (Gal. 3:19), agano la sheria na hukumu. Lakini wanadamu wasingemsogelea hapo. Kama alivyokuwa Mungu waliyemtumikia, huko Sinai haikuwezekana kuwakaribia. Malaika hawakuwa wakisherehekea pale Sinai; walikuwa wakipaza sauti za tarumbeta za hukumu.”

“Kinyume na vile yafundishavyo baadhi ya makanisa, hatupaswi kuwaabudu malaika. Tunajumuika nao katika kumwabudu Mungu, na Mungu pekee. “Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu,” Paulo anaonya, “kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika” (Kol. 2:18). Wakati wa njozi yake huko Patmo, wakati mmoja Yohana alistaajabu sana kiasi kwamba alianguka mbele ya miguu ya malaika kana kwamba kutaka kumwabudu. Lakini malaika huyo akamkataza, akisema, “Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu.” (Ufu. 19:10). Huko mbinguni, hatutawaabudu malaika, bali tutaabudu pamoja na malaika. Tutajumuika nao katika sherehe na sifa ya milele kwa Mungu.” [John F. MacArthur Jr., Hebrews, MacArthur New Testament Commentary, (Chicago: Moody Press, 1983), 414–415].

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Dibaji ya Angilolojia: (Fundisho kuhusu malaika) Somo # 2