Shetani, Utangulizi.

FUNDISHO KUHUSU SHETANI, UTANGULIZI

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Fundisho kuhusu Malaika: Shetani/ 76-009 (Mathayo 4:1, 10)/ Andiko Msingi: “Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.” (Mathayo 4:1)

Kielelezo cha Ufunguzi. Maabadi ya Ibilisi: “Popote Mungu anaposimamisha nyumba ya maombi, Ibilisi daima hujenga maabadi yake hapo; Na itagundulika baada ya uchunguzi kwamba hii yake ina idadi kubwa zaidi ya waumini.” (Daniel Defoe)

MASWALI NA MAJIBU.

[1] Je Shetani ni nani? Hasidi, mshtaki; kiongozi wa malaika walioanguka; kiumbe-nafsi ampingaye Mung na kutafuta kuzuia mipango yake na kuwaongoza watu Wake kwenye uasi/dhambini.

[2] Ni aya gani za Biblia muhimu ambazo unakumbuka kuhusu Shetani? Ayubu 1:6–12; Yn. 8:44; 1 Pet 5:8–9; 1 Yn. 3:8; Mat. 4:1, 10; Rum. 16:20; Ufu. 12:7–10; Ufu. 20:2, 10

[3] Habari gani kuhusu maandiko mengine husiani? 1 Nya. 21:1, Ayubu 2:2–7, Isa 14:12–15, Zek. 3:1–2, Mat 4:1–11, Mat 12:24, Mat 13:19, Mat 13:38–39, Mat 25:41, Luka 10:17–19, Luka 22:31–32, Yn. 12:31, Yn. 13:27, Yn. 14:30–31, Yn. 16:11, Mdo. 5:3, Mdo. 26:17–18, Rum. 16:20, 1 Kor. 7:5, 2 Kor. 2:11, 2 Kor. 4:3–4, 2 Kor. 11:13–15, Efe. 2:2, Efe. 6:11–12, 1 Thes. 2:17–18, 1 Thes. 3:5, Ebr. 2:14–15, Ufu. 2:12–13, Ufu. 20:2–3, Ufu. 20:10

[4] Ni maangiko gani humtaja Shetani kwa jina? 1 Nyak. 21:1; Ayubu 1:6–9, 12; 2:1–4, 6–7; Zek. 3:1–2, Mat 4:1, 3, 5–11; 5:37; 6:13; 12:26; 13:19, 38–39; 16:23; 25:41; Marko 1:13; 3:22–23, 26; 4:15; 8:33; Luka 4:2–9, 12–13; 8:12; 10:18–19; 11:18; 13:16; 22:3, 31; Yn. 8:38, 41, 44; 12:31; 13:2, 27; 14:30; 16:11; 17:15; Mdo. 5:3; 10:38; 13:10; 26:18; Rum. 16:20; 1 Kor. 2:6; 5:5; 7:5; 2 Kor. 2:11; 6:15; 11:3, 14–15; 12:7; Efe. 2:2; 4:27; 6:11, 13, 16; 1 Thes. 2:18; 3:5; 2 Thes. 2:9; 3:3; 1 Tim. 1:20; 3:6–7; 5:14–15; 2 Tim. 2:26; 4:18; Ebr. 2:14; Yak. 4:7, 16; 1 Pet. 5:8–9; 1 Yn. 2:13–14; 3:8, 10, 12; 4:4; 5:18–19; Yuda 9; Ufu. 2:9–10, 13, 24; 3:9; 12:3–4, 7–18; 13:2, 4; 16:13; 20:2–3, 7–10.

[5] Je ni maneno gani mengine yanayohusiana na Shetani? Shetani kutupwa chini, sinagogi la Shetani, ufalme wa Shetani, njama za Shetani, mambo ya kina, vilindi vya Shetani.

WATU KATIKA BIBLIA

[6] Je unaweza kubainisha baadhi ya watu katika Biblia kuhusiana na dhana ya Shetani? Ndiyo.

 1. Yesu alimtaja Beelzebuli (Marko 3:22–30, Luka 11:14-23, Mat. 9:34, 12:22-32)
 2. Watu walikataliwa na Paulo (1 Tim. 1:18–20)
 3. Kushindwa na Shetani (Ufu. 20:7–10)
 4. Waraka wa Pergamo (Ufu. 2:12–17)

MATUKIO YA BIBLIA

[7] Je unaweza kubainisha baadhi ya matukio ya Biblia yanayohusiana na Shetani? Ndiyo.

 1. Majaribu na Anguko la Mwanadamu • Mwa. 3
 2. Kipindi kabla ya mashaibu • Mwa. 1:1–9:27
 3. Kisa cha Ayubu • Ayubu 1:6–42:17
 4. Ayubu apoteza mali zake • Ayubu 1:6–2:10
 5. Mali za Ayubu zatwaliwa • Ayubu 1:6–22
 • Maisha ya Yesu • Mat. 1:18–19:22; 20:17–28:20; Marko 1:2–10:22, 32–16:20; Luka 1:8–3:22; 4:1–9:50; 10:1–24:53; Yn. 1:6–3:36; 4:1–13:38; 15:1–21:23; Mdo. 1:1–19; 1 Kor. 15:6–7
 • Yesu adai kuwa nuru ya ulimwengu • Yn. 8:12–59; Yesu afundisha katikati ya ukinzani huko Yerusalemu • Yn. 7:11–8:59
 • Huduma ya Yesu huko Uyahudi na Perea • Mat. 19:1–22; 20:17–34; 26:6–13; Marko 10:1–22, 32–52; 14:3–9; Luka 13:22–16:31; 17:5–19:28; Yn. 7:11–12:11
 • Huduma ya Yesu • Mat. 3:13–19:22; 20:17–34; 26:6–13; Marko 1:9–10:22, 32–52; 14:3–9; 15:41; Luka 3:19–22; 4:1–9:62; 10:1–16:31; 17:1–19:28; Yn. 1:29–3:36; 4:1–12:11
 1. Kanisa la Awali • Mdo. 1:12–2:41; 3:1–5:11, 17–28:31; 22:17–21; Rum. 16:1, 22; 1 Kor. 16:8–9; 2 Kor. 2:1; 7:13–15; 8:16–24; 9:3–5; 11:8–9; 12:14–18; 13:1–2; Gal. 1:17–24; 2:11–14; Efe. 6:21–22; Filp. 2:25–30; 4:18; Kol. 4:7–9, 16; 1 Thes. 3:1–5; 1 Tim. 1:3; 2 Tim. 1:17; 2:13; 4:9–21; Tt 1:5; Film. 10–12; Ufu. 1:9–22:21
 1. Yohana apata njozi huko Patmo • Ufu. 1:9–22:21; Yohana aona joka na wanyama wawili • Ufu. 12:1–13:18; Vita vya mwanakondoo na wanyama • Ufu. 6:1–18:24

SHETANI: MATUKIO MENGINE HUSIANI KIBIBLIA:

 1. Utajiri wa Ayubu watwaliwa
 2. Zekaria aona njozi ya Yoshua
 3. Ayubu apoteza utajiri wake
 4. Shetani amjaribu Yesu jangwani
 5. Yohana aona njozi huko Patmo
 6. Vitasa saba vya ghadhabu ya Mungu vyamiminiwa
 7. Ushindi wa Mwanakondoo: Lusifa atupwa nje ya mbingu
 8. Ushindi wa Mwanakondoo: Msalaba
 9. Ushindi wa Mwanakondoo: Vita vya Harmagedoni
 10. Ushindi wa Mwanakondoo: Ujio wa Pili
 11. Yohana amwona nyoka na wanyama wawili
 12. Kristo atawala kwa miaka elfu moja
 13. Shetani ashindwa

[8] Je Mada-Masomo gani yatazingatiwa kuhusu Shetani?

 1. Uwepo wa Shetani
 2. Kuumbwa kwa Shetani
 3. Hali ya Asili ya Shetani
 4. Utume/Kazi ya Shetani ya Uovu
 5. Anguko la Shetani
 6. Uangamivu wa Shetani.

[9] Je Dhima-Ibada zipi huweza kuandaliwa kuhusu Shetani?

 1. Shetani Adui wa Mungu
 2. Shetani kama Adui wa Watu wa Mungu
 3. Shetani kama Mjaribu
 4. Shetani kama Mdanganyifu
 5. Ufalme wa Shetani
 6. Mawakala wa Shetani
 7. Upinzani wa Shetani
 8. Kushindwa kwa Shetani

[10] Yapi ni majina ya Shetani katika Biblia?

 1. Abadoni (Ufu. 9:11)
 2. Mshitaki wa ndugu zetu (1 Petro 5:8)
 3. Malaika wa kuzimu (Ufu. 9:11)
 4. Apolioni (Ufu. 9:11)
 5. Beelzebuli (Mat. 12:24; Marko 3:22; Luka 11:15)
 6. Beliali (2 Kor. 6:15)
 7. Pepo wa uongo (1 Wafalme 22:22)
 8. Ibilisi (Mat. 4:1; Luka 4:2; Ufu. 20:2)
 9. Joka (Ufu. 12:3; 20:2)
 10. Adui (Mat. 13:39)
 11. Mwovu (Mat. 13:19, 38)
 12. Roho mbaya (1 Sam. 16:14)
 13. Ni baba wa uongo (Yohana 8:44)
 14. Ni mungu wa ulimwengu huu (2 Kor. 4:4)
 15. Joka mkubwa mwekundu (Ufu. 12:3)
 16. Mwongo (Yohana 8:44)
 17. Muuaji (Yohana 8:44)
 18. Ni mfalme wa uwezo wa anga (Efe. 2:2)
 19. Ni mtawala wa pepo wachafu (Mat. 12:24; Marko 3:22; Luka 11:15)
 20. Ni mtawala wa ulimwengu huu (Yohana 12:31)
 21. Shetani (Ayubu 1:6; Mat. 4:10)
 22. Nyoka (Mwa. 3:4, 14)
 23. Nyoka wa zamani (Ufu. 12:9; 20:2)
 24. Ni roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi (Efe. 2:2)
 25. Ni Mjaribu (Mat. 4:3; 1 Thes. 3:5)

[11] Je unaweza kuwasilisha muhtasari mfupi kuhusu Shetani pamoja na rejea za Biblia? Ndiyo

 1. Alimwasi Mungu, 2 Pet 2:4; 1 Yohana 3:8.
 2. Alitupwa nje ya mbingu, Luka 10:18.
 3. Alitupwa chini hadi kuzimu, 2 Pet 2:4; Yuda 1:6.
 4. Yeye ni mwasisi wa majaribu, dhambi, na mauti, Mwa. 3:1, 6, 14, 24.
 5. Anakuja ili aibe, aue na kuangamiza, Yn. 10:10.
 6. Alimjaribu Yesu Kristo, Mat 4:3–10.
 7. Hupotosha Maandiko, Mat 4:6; Zab. 91:11, 12.
 8. Hupinga kazi ya Mungu, Zek. 3:1; 1 Thes 2:18.
 9. Huzuia kazi ya injili, Mat 13:19; 2 Kor. 4:4.
 10. Hutenda kazi kwa ishara na ajabu za uongo, 2 Thes 2:9; Ufu. 16:14.
 11. Huigiza umbo la malaika wa nuru, 2 Kor. 11:14
 12. Yeye ni “yule mwasi,” mwasisi wa uasi, 2 Thes 2:9; 2 Tim 4:1.
 13. Atahukumiwa wakati wa mwisho, Yuda 1:6; Ufu. 20:10.
 14. Moto wa milele umeandaliwa kwa ajili yake hasa pamoja na malaika wake, Mat 25:41.

MAANA YA KIIBADA: “Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. Amina.” (Warumi 16:20)

“Paulo huwaakikishia waumini waaminifu kwamba wanaweza kutazamia siku ambapo vita vyao vya kiroho vitakuwa vimeisha. Walikuwa wa uongo na madanganyo ni mawakala wa Ibilisi, nao wataangamizwa wakati ule Mungu wa amani atakapomseta Shetani. Katika Warumi 15:33, Paulo anamzungumzia “Mungu wa amani” katika uhusiano na upaji wa kiungu kwa ajili ya watoto Wake. Hapa Mungu wa amani anazungumziwa katika uhusiano na ushindi Wake dawamu dhidi ya Shetani na utumishi Wake kwa niaba ya watoto Wake. Paulo anatumia taashira ya Mwanzo 3:15, ambapo, baada ya Anguko, Mungu anamtangazia nyoka (Shetani) kwamba “Huo [uzao ambao ni Masihi] utakuponda kichwa,” yaani, kumsababishia jeraha la mauti.

“Kirai en tachei, hapa kimefasiriwa kama upesi, kina maana ya haraka, au tasihili, kama ilivyofasiliwa katika Matendo 12:7 na 22:18, na mara nyingi ilibeba mdokezo naibi wa kutotarajika. Kielezi chenye uhusiano wa karibu tachu hutumiwa mara tatu katika Ufunuo 22 kuhusiana na Kristo “kuja upesi” (vv. 7, 12, 20). Tunajua kutokana na Agano Jipya yenye kwamba Shetani hakusetwa haraka kwa mtazamo wa waumini waliokuwa wakiishi wakati huo. Angali hajatiishwa bado.”

“Inatia moyo kwamba Bwana atamseta Shetani chini ya miguu yako, miguu ya watu wa Mungu, kadiri wanapoungana na Kristo katika ushindi Wake dhidi ya Shetani.” [John F. MacArthur Jr., Romans, MacArthur New Testament Commentary, (Chicago: Moody Press, 1991), 2:377].

SAUTI YA INJILI: Kuepuka Mitego ya Shetani, Sehemu ya 1. Wapendwa, kila siku tunakabiliana na kiumbe mwenye chuki, mwerevu na mjuzi sana aitwaye Ibilisi. Maandiko yanasema hatuna budi “tumzuie Shetani asije akatushinda; maana hatukosi kuzijua hila na makusudi yake.” (2 Wakorintho 2:11, AMP).  Lakini tunawezaje kuepuka hila zake, mitego yake? Jibu linapatikana katika 1 Petro. “Iweni na uwianifu (kiasi, nia makini), kesheni na kuchukua tahadhari nyakati zote; kwa kuwa adui yenu, Ibilisi, huzunguka huku na kule kama simba angurumaye [aliye katika njaa kali], akimtafuta mtu amwakue na kummeza.” (1 Petro 5:8, AMP)

Leo, tutaangalia sehemu ya 1 ya “Jinsi ya Kuepuka Mitego ya Shetani,” ambayo ni, “Usitange Mbali.” Mtunzi wa Zaburi anasema “Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno Lako.” (Zaburi 119:67) “Kabla sijateswa mimi nalitanga mbali, lakini sasa neno Lako nalitii [kulisikia, kulipokea, kulipenda, na kulifuata].” (Zaburi 119:67, AMP).

Hivyo, tunawezaje kukeshi, kuwa waangalifu, daima tukiwa tumejiandaa dhidi ya shambulio la adui? Maneno manne: Kusikia, Kupokea, Kupenda, na Kutii Neno. [1] Kulisikia Neno: Maandiko yanasema – “Basi imani, chanzo chake ni kusikia (kile kinachosemwa); na kusikia huja kwa neno la (kuhubiri ujumbe utokao kwenye midomo ya) Kristo (Masihi Mwenyewe).” (Warumi 10:17, AMP). Kuwa mwangalifu huanza kwa kulisikia neno la Mungu.

[2] Pili, kupitia maombi. Maombi ni ya lazima katika kumshinda Ibilisi. Tunapaswa kuomba, siyo tu kabla hatujala, bali wakati wote. Mungu huwasiliana nasi kupitia Biblia na maombi. maombi ni oksijeni tunayovuta! Wakati mwingine Wakristo hupuuza maisha yao ya maombi, kulisikia Neno, nao wanashindwa kulisoma Neno la Mungu vile wapaswavyo. Wanapoanza kufanya hivi, wanaanza kutanga mbali.

[3] Kulipokea Neno: “Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.” (1 Wathesalonike 2:13) “Paulo alimshukuru Mungu jinsi Wathesalonike walivyokuwa wameupokea ujumbe. Wakati ule Paulo na Sila walipokuwa wamemaliza kuhubiri, watu walitambua maneno husika kuwa siyo mawazo ya mwanadamu, nao walikubali ujumbe wa injili kuwa neno hasa la Mungu. Ujumbe wa injili hufunua asili na uwezo wake wa kiungu kadiri unavyobadilisha maisha ya watu. Wathesalonike walikuwa wakishuhudia jinsi neno hili linavyoendelea kutenda kazi ndani ya wale waaminio. Kupitia neno Lake, Mungu hutenda kazi maishani mwa waumini, akiwabadilisha, akiwaongoza, akiwatakasa. Kama ambavyo ilikuwa sahihi kwa waumini wa Thesalonike, ndivyo ilivyo kweli kwa wote waaminio—kwa wale wanapokea ujumbe wa injili na kumtumaini Kristo kama Mwokozi. Ujumbe huo ungali “neno hasa la Mungu”—hakuna hata neno moja ambalo limebadilika. Bado linabadilisha maisha (Luka 8:11, 15; Waebrania 4:12).” [Bruce B. Barton and Grant R. Osborne, 1 & 2 Thessalonians: Life Application Commentary, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1999), 41].

[4] Kulipenda Neno: Kwa sababu Neno ndiyo njia ambayo kwayo Mungu hutumia kuzungumza nasi, tunahitaji kulipenda na kulitumia. Lakini kwa namna gani? Kwa kulisoma. Wapendwa, tunapaswa kumpenda Mungu “kwa kulitenda Neno Lake.” Ni wajibu wetu kulisoma. Maandiko hueleza kwamba tunalifanya hili kwa njia tatu– (a) Kwa Kuisoma Biblia Hadharani. Hii ilifanyika kwenye sinagogi la Wayahudi zamani, kama inavyothibitishwa na Yesu akiingia humo na kutekeleza usomaji uliochaguliwa kutoka kwa nabii Isaya (Luka 4:16–24). Hili lilifanyika katika kanisa la zamani la Kikristo, kama inavyothibitishwa kwa maneno ya Paulo (1 Thes. 5:27; Kol. 4:16). — (b) Kwa Kuisoma kama Familia. Musa aliwanasihi Waisraeli akisema, “Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako; nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.” (Kumbukumbu 6:6–7). Usomaji wa Biblia kwenye familia ni muhimu sana ili kudumisha dini ya Ukristo kwa watoto wetu (angalia 2 Tim. 3:14–15). Tunahitaji kuweka msisitizo mkubwa katika mpango wa Kusoma Biblia Kila Siku. — (c) Kwa Kuisoma kwa Faragha. Zaburi 119 pia ni tafakari ya muumini binafsi: “Sheria Yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa.” (Zaburi 119:97). Kutafakari Neno humfanya mtu husika apate hekima (v. 98), humfanya mtauwa (v. 101), na kutupatia kupenda mambo ya kiroho kwa vile maneno Yake ni “matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu.” (v. 103). Usomaji na tafakari ya Neno humfanya mtu afanane na mti uliomwagiliwa vyema uzaao matunda (Zab. 1:1-3).

[5] Kulitii Neno: “Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu…. Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.” (Yakobo 1:22, 25)

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? Kujiandaa vizuri zaidi kukabilia shambulio la Ibilisi, lazima–[1] Tulisikie Neno (angalia Mfano wa Mpanzi, Mat 13:18-23); [2] Tuombe Daima; [3] Tulipokee Neno; [4] Tulipenda Neno; na [5] Tulitii Neno.

Wapendwa, Neno la Mungu linafananishwa na upanga unalotulinda dhidi ya maadui wa kiroho (Efe. 6:17). Ni taa inayotuongoza (Zab. 119:105). Linalinganishwa na maziwa yanayostawisha nafsi (1 Petro 2:2).

Utii wa Neno hujumuisha kuepuka mionekano yote ya uovu. Baadhi yetu hukosa ujasiri wa kusema “Hapana” kwa marafiki zetu wasio Wakristo. Tunaposhindwa kufanya hivyo tunavuruga maadili yetu, tunajisalimisha kwa maisha ya zamani na kuwa wahanga wa mitego ya Shetani. Wapendwa, lazima tutunze kwa juhudi maisha yetu ya maombi, tukimkaribia Mungu kila siku. Lazima tuchukue msimamo wetu kwa uthabiti kwa ajili ya Mungu, tukikaa mbali na janibu ya Shetani.

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.” (Yakobo 4:7–8)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Fundisho kuhusu Malaika: Shetani—mpinzani mkuu wa Mungu/ Somo # 9.