Asili na Hulka ya Malaika

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Fundisho kuhusu Malaika/ 76-003 (Waebrania 1:13-14)/ Andiko Msingi: “Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” (Waebrania 1:13–14)

Maelezo ya Ufunguzi: Asili ya malaika ni muhimu katika uhusiano na uamiliano na wanadamu. “Kwa sababu malaika hawaonekani, mimi na wewe kijumla hatuelewi shughuli zao nyuma ya jukwaa. Hatuna jinsi ya kuelezea ni mara ngapi malaika wameingilia kati kwa niaba yetu bila sisi kufahamu jambo hilo.”

Malaika wana hulka, lakini pia wana uwezo waliopewa na Mungu. Katika Zaburi 103:20, tunasoma: Mhimidini Bwana, enyi malaika Zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno Lake, Mkiisikiliza sauti ya neno Lake.

Na katika 2 Wathesalonike 1:7, tunasoma kuhusu “malaika wa uweza.” Mara nyingi malaika hutajwa kuwa watakatifu (Ayubu 5:1; 15:15; Zab. 89:7; Dan. 4:13, 17, 23; 8:13; Yuda 14). Ni viumbe wenye upekee wa ajabu aliowaumba Mungu ili kuwahudumia wanadamu. Hili linapaswa kuwa somo kuu na ukumbusho kwa kila mmoja wetu kuhusu upendo wa Mungu kwetu.” [H. Wayne House and Timothy J. Demy, Answers to Common Questions about Angels & Demons, (Grand Rapids, MI: Kregel Publications, 2011), 20].   

MASWALI NA MAJIBU

[1] Je Biblia inasema nini kuhusu ufanidi (ukuu ama ubora wa juu) wa malaika? Wao ni viumbe fanidi— fanidi kuliko mwanadamu katika hali yake kabla ya kutukuzwa, “You have made him a little lower than the angels; You have crowned him with glory and honor, And set him over the works of Your hands.” (Ebr. 2:7).

[2]Hivi siku moja mwanadamu anawahukumu malaika? Ndiyo. Siku inakuja ambapo mwanadamu aliyetukuzwa (baada ya Ujio wa Pili) amefawidhiwa kazi ya kuhukumu (kutekeleza adhabu juu ya) malaika waovu: “Hamjui ya kuwa mtawahukumu malaika, basi si zaidi sana mambo ya maisha haya?” (1 Wakorintho 6:3)

[3] Je siku moja mwanadamu atatawala juu ya malaika? Ndiyo. Siku inakuja ambapo mwanadamu aliyetukuzwa (baada ya Ujio wa Pili) amefawidhiwa kutawala juu ya malaika wema: “Maana hakuuweka chini ya malaika;” “Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake (mwanadamu)” (Ebr. 2:5, 8c, AMP)

Hulka ya malaika ni nini?

[4] Wao ni Viumbe wa Kiroho — (ikiwa na maana kwamba wa ni “roho”) — malaika wema (Ebr. 1:14), na malaika waovu au pepo wachafu (Mat. 8:16; Luka 8:2; 11:24, 26; Matendo 19:12) wanaitwa “pepo,” pepo wachafu. Wana miili halisiri (isoyakinifu), miili junubu (siyo ya kidunia), na miili badiri, isiyo na maumbo.

[5] Wao ni Viumbe Halidifu (Wasiokufa)— hebu tuone kile Biblia isemacho kuhusu uhalidifu wa malaika waovu.

“Na tazama, wakapiga kelele, wakisema, Tuna nini Nawe, Mwana wa Mungu? Je! Umekuja kututesa kabla ya muhula wetu? (Mathayo 8:29)

 • “Pepo wachafu walimtambua Yesu kama Mwana mtakatifu wa Mungu. Ni jambo la kinaya jinsi gani kwamba watu katika siku za Yesu walikuwa na upofu kiasi hicho, wakati pepo wachafu waliweza kuwa na utambuzi bayana kuhusu Yesu. Pepo wachafu waliuliza iwapo Yesu alikuwa amekuja kuwatesa. Neno “tesa” ni taashira na sahihi. Biblia inasema kwamba mwishoni mwa ulimwengu, Ibilisi na pepo wake wachafu watatupwa kwenye ziwa la moto (Ufunuo 20:10). Swali husika la pepo wachafu huonesha kwamba walijua kuhusu mustakabali wao wa mwisho. Pepo hao wachafu walitumaini kwamba Yesu asingewapelekea kwenye hatima yao kabla ya wakati ulioteuliwa. Maandishi ya Kiyahudi yaliyoandikwa kati ya wakati wa Agano la Kale na Agano Jipya yalifundisha kwamba pepo wachafu wana ruhusu ya kupinga jamii ya wanadamu hadi pale tu katika Siku ya Hukumu. Kauli hii kutoka kwa pepo wachafu huonesha uwezo wa Mungu juu ya majeshi ya Shetani.” [Bruce B. Barton, Matthew, Life Application Bible Commentary, (Wheaton, IL: Tyndale House Publishers, 1996), 167].

“Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.” (Yuda 6). “Na yule Ibilisi, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo. Nao watateswa mchana na usiku hata milele na milele.” (Ufunuo 20:10)

[6] Wao ni Viumbe Wasojinsi—“Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini, wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi; wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo.” (Luka 20:34–36)

 • Malaika hawaoi wala kuolewa au kujihusisha katika mahusiano ya kimapenzi, kwa vile kusudi lingine kuu mojawapo la tendo hili ni kuijaza dunia (ambayo wakazi wake hufa) lakini malaika (wakazi wa junubu ya mbinguni) hawafi.
 • “Hakuna ndoa mbinguni. Wana wa ulimwengu huu (msemo wa Kiebrania ambayo ni taashira ya wale wanaoishi katika ulimwengu wa sasa; cf. Luka 16:8) huoa na kuolewa. Lakini kama ilivyo kwa mahusiano mengine ya kifamilia, ndoa ni kwa ajili ya maisha ya sasa tu. Uhalisia ni kwamba wale wanaohesabiwa kustahili kupata uzima wa milele unaofuatia ufufuo kutoka kwa wafu, hawaoi wala hawaolewi; maana hawawezi kufa tena, kwa sababu wao ni kama malaika, na wao ni wana wa Mungu, ilhali wakiwa wana wa ufufuo. Hakutakuwa na haja ya ndoa na familia kwa kusudi la kuongeza idadi ya watu, kwa sababu ya wazi kwamba wale waishio milele katika uwepo wa Mungu hawawezi kufa tena na hivyo hawahitaji kuhawilishwa. Watakuwa kama malaika watakatifu, ambao wao hawatakufa kamwe.” [John MacArthur, Luke 18–24, MacArthur New Testament Commentary, (Chicago, IL: Moody Publishers, 2014), 146].

[7] Wao ni Viumbe Wenye Nguvu

 • “Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize” (1 Nya. 21:15)
 • “Kwa kuwa Bwana atapita ili awapige hao Wamisri; na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo miwili, Bwana atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie nyumbani mwenu kuwapiga ninyi.” (Kutoka 12:23)
 • “Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru.” (2 Nya. 32:21)
 • “Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia.” (Mathayo 28:2)
 • “Wenye ushupavu, wenye kujikinai, hawatetemeki wakiyatukana matukufu; ijapokuwa malaika ambao ni wakuu zaidi kwa uwezo na nguvu, hawaleti mashitaka mabaya juu yao mbele za Bwana.” (2 Petro 2:11)

[8] Wao ni Viumbe Waendao Kasi

 • “Basi hapo nilipokuwa nikisema, na kuomba, na kuiungama dhambi yangu, na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuomba dua yangu mbele za Bwana, Mungu wangu, kwa ajili ya mlima mtakatifu wa Mungu wangu; naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.” (Danieli 9:20–21)
 • “Na tazama, mmoja wao waliokuwa pamoja na Yesu akanyosha mkono wake, akaufuta upanga wake, akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio. Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga. Ama wadhani ya kuwa Mimi siwezi kumsihi Baba Yangu, Naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?” (Mathayo 26:51–53)

[9] Wao ni Viumbe Wengi Sana

 • “Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele Yake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele Yake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.” (Danieli 7:10)
 • “Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu” (Ufunuo 5:11)

[10] Wana Maarifa

 • “Ndipo mimi mjakazi wako nikasema, Neno la bwana wangu mfalme na liwe la kustarehesha; kwa kuwa kama malaika wa Mungu ndivyo alivyo bwana wangu mfalme, kuyapambanua yaliyo mema na yaliyo mabaya; naye Bwana, Mungu wako na awe pamoja nawe.” (2 Samweli 14:17)
 • “Mtumwa wako Yoabu ameyatenda haya ili kubadili uso wa jambo hili; na bwana wangu anayo akili, kama akili ya malaika wa Mungu, hata ajue mambo yote ya duniani.” (2 Samweli 14:20)
 • Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1 Petro 1:12)

[11] Wana Hisia

 • “Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? (Ayubu 38:7)
 • “Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.” (Luka 15:7) Hupenda na kufurahia!
 • “Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi” (Waebrania 12:22)

[12] Wana Utashi wa Kimaadili

 • “Nami Yohana ndimi niliyeyasikia na kuyaona mambo hayo. Na hapo nilipoyasikia na kuyaona nalianguka, ili nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha hayo. Naye akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mjoli wako, na wa ndugu zako manabii, na wa wale wayashikao maneno ya kitabu hiki. Msujudie Mungu.(Ufunuo 22:8–9)

[13] Wanawasiliana kwa Maarifa kupitia usemi —

 • “Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.” (Mathayo 28:5)
 • “Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana.” (Luka 1:13)

[14] Wana Shauku

 • “Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia. (1 Petro 1:12)
 • Wanashindana ama Kuhojiana: “Lakini Mikaeli, malaika mkuu, aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee.” (Yuda 9)

[15] Nadhari na Utambuzi

 • Wakamsihi asiwaamuru watoke kwenda shimoni.” (Luka 8:31)
 • “Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. Nawe utakuwa na furaha na shangwe, na watu wengi watakufurahia kuzaliwa kwake. Kwa sababu atakuwa mkuu mbele za Bwana; hatakunywa divai wala kileo; naye atajazwa Roho Mtakatifu hata tangu tumboni mwa mamaye. Na wengi katika Waisraeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao.” (Luka 1:13–16)

[15] Wanajongea— “Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” (Yohana 1:51)

[16] Wanaelewa Ufunuo wa Kiungu — “Na yule malaika niliyemwona, akisimama juu ya bahari na juu ya nchi, akainua mkono wake wa kuume kuelekea mbinguni, akaapa kwa Yeye aliye hai hata milele na milele, Yeye aliyeziumba mbingu na vitu vilivyomo, na nchi na vitu vilivyomo, na bahari na vitu vilivyomo, ya kwamba hapatakuwa na wakati baada ya haya” (Ufunuo 10:5–6).

[17] Wanaelewa Uungu na Uwezo wa Yesu

 • “Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti, akisema, Tuna nini Nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza? Najua Wewe ni nani—Mtakatifu wa Mungu!” (Marko 1:23–24, NKJV)
 • “Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua. (Marko 1:34)

[18] Wanaabudu — “Hata tena, amletapo mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, asema, Na wamsujudu malaika wote wa Mungu.” (Waebrania 1:6)

MAANA YA KIIBADA: Wapendwa, malaika hujua huwa na shauku na hupendezwa na injili ya Kristo — “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.” (1 Timotheo 3:16) “Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1 Petro 1:12)

SAUTI YA INJILI: Nini kinachomfanya malaika atabasamu? [1] Katika Asubuhi ya Uumbaji: “Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?” (Ayubu 38:7)

[2] Wakati wa Ujio wa Kwanza Wakristo Kristo: “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” (Luka 2:13–14)

[3] Pale Mdhambi Anapoongoka: “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye (akibadili nia yake kuwa njema, akigeuza mienendo yake kwa dhati, huku akichukia dhambi zake za zamani).” (Luka 15:10, AMP)

 • “Toba ya nafsi moja hupeleka furaha isiyoelezeka kwa jeshi lote la mbinguni. Lahani hufanywa kutoka kila kinubi na kila sauti katika nyimbo tukufu kwamba jina lingine limeandikwa katika kitabu cha uzima, nuru nyingine huwashwa ili kuangaza katikati ya giza la kimaadili la ulimwengu huu mpotofu. Tukio hilohilo hueneza hofu kuu miongoni mwa malaika wapotofu na humfadhaisha kiongozi mkuu katika uasi dhidi ya sheria ya Mungu. Mfalme wa giza, ilhali akiona nafsi ambayo ameihesabu kuwa yake ikiponyaka kwenye utawala wake kama ndege kutoka katika mtego wa mwindaji, na kumfanya Kristo kimbilio, hutenda kazi kwa jitihada za kuzimu ili kumnasa tena yule aliyemponyoka.” [Ellen Gould White, Our High Calling, (Review and Herald Publishing Association, 1961), 89].

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? Shukrani kwa Mungu kutupatia malaika Wake watakatifu ili watulinde.

Malaika huwasimamia watoto wa Mungu (Zab. 34:7; 91:11- 12). Hutulinda, hutukirimia mahitaji, lakini muhimu zaidi hutamani kwamba tuokolewe na kwenda mbinguni kuwa pamoja na Muumbaji wetu. Unajua wapo pale juu, hivyo, wanajua jinsi mbingu ilivyo. Sikiliza nukuu hii: “Bwana amempatia kila mtu kazi yake, na malaika watakatifu hutaka tuwe tunaifanya kazi hiyo. Kadiri ambavyo utakesha na kuomba na kufanya kazi, wanakuwa tayari kushirikiana pamoja nawe.” (Testimonies for the Church, 6:481).

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Kwa kuwa atakuagizia malaika Zake waambatane nawe na kukulinda na kukuhifadhi katika njia zako zote [za utii na huduma]. Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.” (Zaburi 91:11–12, AMP)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Dibaji ya Angilolojia: (Fundisho Kuhusu Malaika) Somo # 3