Malaika, Muhtasari.

Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Utangulizi Kuhusu Angilolojia: (Mafundisho Makuu kuhusu Malaika) Seh 1/ 76-001 (Waebrania 1:14)/ Andiko Msingi: “Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wowote, Uketi mkono Wangu wa kuume Hata nitakapoweka adui Zako chini ya nyayo Zako? Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?” (Waebrania 1:13–14)

Maelezo ya Ufunguzi: (Kielelezo) — “Nakubali uwepo wa malaika kama kipengele cha uhalisia wa kiroho wa utajiri wa Mungu. Ni bayana, kutokana na wingu la malaika, lazima uumbaji ni tanzifu zaidi, anuwai, na uhalisia mwingi kuliko ambavyo mtu angependa kufikiria. Malaika ni ishara kwamba wema wa Mungu lazima uwe na manufaa kupita kiasi; humiminika maridhawa katika nishati ya uumbaji. Viumbe mbalimbali halidi wanaweza kutegemezwa na kustawishwa katika mfumo huu mwema na maridhawa.” [Sidney Callahan in Commonweal (Dec. 1, 1995). Christianity Today, Vol. 40, no. 2].

MASWALI NA MAJIBU.

[1] Kwa nini tufanye somo la kiteolojia kuhusu malaika: (Angilolojia)? Kwa sababu ni mada ya Biblia, yenye rejea nyingi zaidi katika maandiko kuliko watu wadhanivyo. Pili, ni mada inayonasihi, kwa kiwango cha kusisimua kuliko inavyodhaniwa mara nyingi.

[2] Ni mara ngapi neno malaika huonekana kwenye Biblia? Mara 186 katika Agano Jipya na zaidi ya mara 100 katika Agano la Kale.

[3] Mara nyingi viumbe huonekana ambao kwa kweli ni ‘malaika,’ lakini neno ‘malaika’ halikutumiwa hasa, mfano:

 • ‘mtu’ (Mwanzo 32:24; Yoshua 5:13).
 • ‘mamlaka (Wakolosai 1:16).
 • Makerubi (Mwanzo 3:24).
 • Maserafi (Isaya 6:2).
 • magari ya moto’ (2 Wafalme 6:17).

[4] Malaika ni Nani? “Kiumbe wa kiroho, kimsingi ni mjumbe (Kiebrania malʾāḵ; Kiyunani ángelos) wa Mungu (mfano, Mwa. 16:7, 9; Kut. 3:2; Hes. 22:22–35). Majina mengine ni pamoja na “wana wa Mungu” (Ayubu 1:6; Zab. 29:1), “watakatifu” (mfano, Zab. 89:7; Dan. 8:13, na “mlinzi” (Dan. 4:13, 17, 23 [MT 10, 14, 20]). Wakati mwingine “majeshi ya mbinguni” au “jeshi la mbinguni” pia hurejelea malaika (1 Flm. 22:19 = 2 Nya. 18:18; Zab. 148:2; Neh. 9:6). Kiebrania malʾā pia hutumika kwa ajili ya manabii wanadamu (2 Nya. 36:15–16; Isa. 44:26; Hag. 1:13), makuhani (Mal. 2:7), na pepo (Zab. 104:4); Kiyunani ángelos huweza pia kurejelea wajumbe wanadamu (Luka 9:52; Marko 1:2).” [Edward P. Myers, Eerdmans dictionary of the Bible, 2000, 63].

[5] Nini maana ya neno “malaika.” Kwa mazungumzo ya kawaida, “malaika” humaanisha wajumbe.

 • Neno ‘malaika’ kutoka Kiyunani aggeloi, kimsingi humaanisha “wajumbe,” huweza kuwa kiumbe wa kiroho au mwanadamu. “Aggeloi hutumiwa kwa mwanadamu katika Mat. 11:10; Marko 1:2; Luka 7:24, 27; 9:52; cf. 2 Kor. 12:7. Imependekezwa kwamba “malaika” wa makanisa saba ni viongozi wake husika, au maaskofu, katika wakati wa Yohana, na kwamba Bwana alikuwa akiwawasilishia ujumbe kwao kwa ajili ya kupelekwa kwa makanisa yao.” (SDA BC 7:741)
 • Kwa Usomaji Zaidi–malaika ni rejea juu ya wachungaji wa makanisa (Soma Ufu. 1:20; 2:1, 8, 12, 18; 3:1, 7, 14; Malaika kama rejea kuhusu wajumbe wa kibinadamu (Soma Lk. 7:24; Yakobo 2:25).
 • Katika Ufu. 14:6-12, malaika huonekana “wakiruka katikati ya mbingu” wakitangaza Ujumbe wa Malaika wa Tatu. Kwa kweli hii ni alama ya “watakatifu” wanaowasilisha ujumbe huu, maana hawakupewa malaika ili kwenda na kuhubiri injili, lakini ni wanadamu waliopewa utume huu. Ingawa malaika wana shauku ya kina sana masuala ya wokovu kama roho wahudumuo (Waebrania 1:14) wao hawajapewa wajibu huu.
 • Mara nyingi sana, hata Yesu Kristo anaitwa malaika, “malaika wa Yehova,” (Mwa. 16:7; 22:11; Waamuzi 6:12; 2 Flm. 19:35), nk. — (Tunaona hili baadaye katika mfululizo huu)
 • Lakini kwa kuzungumza kwa dhati “malaika” hubeba rejea ya nyanja tofauti ya viumbe walioumbwa na Mungu kuwa watumishi Wake. Wao ni roho wahudumuo (1 Wafalme 19:5; Zab. 68:17; 104:4; Luka 16:22; Matendo 12:7–11; 27:23; Ebr. 1:7, 14)

[6] Nini hulka ya malaika? Kwa mujibu wa Biblia, siyo tu kwamba malaika wapo ila pia wapo kama nafsi, kama nafsi wenye akili, utambuzi, na utashi. Sifa zote za hulka huelekezwa kwa malaika.

[7] Malaika waliwatokea nani katika Agano la Kale?

 • Ibrahimu (Mwa. 18:2–15)
 • Hajiri (Mwa. 16:7–14)
 • Lutu (Mwa. 19:1–22)
 • Yakobo (Mwa. 28:10–12)
 • Musa (Kut. 3:1, 2)
 • Balaamu (Hes. 22:31–35)
 • Yoshua (Yos. 5:13–15)
 • Israeli (Amu. 2:1–4)
 • Gideoni (Amu. 6:11–24)
 • Manoa (Amu. 13:6–21)
 • Daudi (2 Sam. 24:16, 17)
 • Eliya (1 Flm. 19:2–8)
 • Danieli (Dan. 6:21, 22)
 • Zekaria (Zek. 2:3)

[8] Habari gani kuhusu kutokea kwao katika Agano Jipya?

 • Zakaria (Luka 1:11–20
 • Mariamu (Luka 1:26–38)
 • Yusufu (Mat. 1:20–25)
 • Wachungaji (Luka 2:8–15)
 • Wanawake kadhaa (Mat. 28:1–7)
 • Mariamu Magdalene (Yohana 20:11–13)
 • Mitume (Matendo 1:10-11)
 • Petro (Matendo 5:19-20)
 • Filipo (Matendo 8:26)
 • Kornelio (Matendo 10:3–32)
 • Paulo (Acts 27:23, 24)
 • Yohana (Ufu. 1:1)
 • Makanisa saba (Ufu. 1:20)

[9] Bainisha huduma ya malaika katika nyakati maalum?

 • Wakati wa uumbaji wa ulimwengu (Ayubu 38:7)
 • Sinai (Matendo 7:38, 53)
 • Kufungwa kwa Shetani (Ufu. 20:1–3)
 • Kurudi kwa Kristo (Mat. 13:41, 49; 1 Thes. 4:16)

ZINGATIA: Tutaangalia huduma ya malaika kwa waumini, wasioamini, na Yesu Kristo wakati ujao.

MAANA YA KIIBADA: Wapendwa, malaika hujua huwa na shauku na hupendezwa na injili ya Kristo — “Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu. Mungu alidhihirishwa katika mwili, Akajulika kuwa na haki katika roho, Akaonekana na malaika, Akahubiriwa katika mataifa, Akaaminiwa katika ulimwengu, Akachukuliwa juu katika utukufu.” (1 Timotheo 3:16) “Wakafunuliwa ya kuwa si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu walihudumu katika mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi Injili kwa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Mambo hayo malaika wanatamani kuyachungulia.” (1 Petro 1:12)

SAUTI YA INJILI: Nini kinachomfanya malaika atabasamu? [1] Katika Asubuhi ya Uumbaji: “Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?” (Ayubu 38:7)

[2] Wakati wa Ujio wa Kwanza Wakristo Kristo: “Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.” (Luka 2:13–14)

[3] Pale Mdhambi Anapoongoka: “Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye (akibadili nia yake kuwa njema, akigeuza mienendo yake kwa dhati, huku akichukia dhambi zake za zamani).” (Luka 15:10, AMP)

WIMBO WA TAFAKARI: “Ndipo Malaika Hufurahia! kutoka “Gaither Vocal Band”

Wakati wa ukamilishwaji wa Lango la Dhahabu; Hapana, malaika hawakusherehekea; Na pale akina Wright waliporusha ndege yao; Hakuna kelele za malaika zilizosikika.

Kuna jambo moja tu ambalo tuna hakika nalo; Ambalo litawafanya malaika hao waruke na kupaza sauti: Ni pale mdhambi anapomfanya Bwana kuwa chaguo lake; Hapo ndipo malaika wanafurahia!

Sasa, pale taa ya umeme ilipowashwa mjini; Hapana, hakuna malaika aliyerukaruka hapo; Na pale mwanadamu alipokanyaga mwezini; Hawakuimba lahani wa ushindi.

Kuna jambo moja tu ambalo tuna hakika nalo; Ambalo litawafanya malaika hao waruke na kupaza sauti: Ni pale mdhambi anapomfanya Bwana kuwa chaguo lake; Hapo ndipo malaika wanafurahia!

Sasa, Mbingu haipazi sauti za bendi; Kwa ajili ya tukio lolote la zamani; Lazima liwe jambo maalum; Ili kuwafanya malaika hao waimbe.

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? Shukrani kwa Mungu kwa kutupatia malaika Wake watakatifu ili watulinde.

Malaika huwasimamia watoto wa Mungu (Zab. 34:7; 91:11- 12). Hutulinda, hutukirimia mahitaji, lakini muhimu zaidi hutamani kwamba tuokolewe na kwenda mbinguni kuwa pamoja na Muumbaji wetu. Unajua wapo pale juu, hivyo, wanajua jinsi mbingu ilivyo. Sikiliza nukuu hii: “Bwana amempatia kila mtu kazi yake, na malaika watakatifu hutaka tuwe tunaifanya kazi hiyo. Kadiri ambavyo utakesha na kuomba na kufanya kazi, wanakuwa tayari kushirikiana pamoja nawe.” (Testimonies for the Church, 6:481).

Uwe na Siku Yenye Baraka: “Kwa kuwa atakuagizia malaika Zake waambatane nawe na kukulinda na kukuhifadhi katika njia zako zote [za utii na huduma]. Mikononi mwao watakuchukua, Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.” (Zaburi 91:11–12, AMP)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Utangulizi kuhusu Angilolojia: (Fundisho kuhusu Malaika) Somo # 1