Hali ya Mwanadamu ya Asili

MWANADAMU ALIUMBWA NA MUNGU

75M-001 (Mwanzo 1:27)/ Hali ya Mwanadamu ya Asili/ Andiko Kuu: “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano Wetu, kwa sura Yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” (Mwanzo 1:26) “Mungu akaumba mtu kwa mfano Wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:27)

Maswali ya Moyoni: [1] Ina maana gani kwamba mwanadamu aliumbwa katika sura ya Mungu? [2] Dhana ya uibukaji hufundishwa kwa watoto katika shule za umma! Je wahimizaji wa dhana ya uibukaji ni kosa? [3] Mungu anasema nini kuhusu mahusiano ya jinsi moja, au ushoga? [4] Je mwanadamu aliumbwa kwa kusudi gani, miongoni mwa mambo mengine? [5] Ipi kanuni ya Mungu ya ndoa? Upi mpango wa kiungu wa ndoa leo?

Haya hapa mazingatio mafupi kutoka kwenye Andiko letu Kuu — [1] Mwanadamu aliumbwa katika sura ya Mungu. Neno “sura’ huelekeza katika kipawa cha kimwili, kiakili, kijamii, na kiroho ambacho kingehitajika kwa ajili ya jamii ya mwanadamu kutimiza kusudi la Mungu kwa ajili yao. Wanadamu waumbwa katika sura ya Mungu na huakisi sifa za kiungu (kama vile maadili na uwezo wa kuchagua), lakini wao hawana uungu kiasili.” [Jon L. Dybdahl, Ed., Andrews Study Bible Notes, (Berrien Springs, MI: Andrews University Press, 2010), 7].

[2] Nadharia ya Uibukaji: Mwanadamu hakuumbwa katika sura ya sokwe, bali katika sura ya Mungu. Mojawapo ya kweli msingi zitokanazo na maandiko haya ni uhalisia kwamba mwanadamu ni matokeo ya uwezo wa Mungu wa uumbaji na wala siyo matokeo ya uibukaji nasibu. Mwanadamu hakuibuka kutoka kwenye kiumbe-seli kwa kipindi cha mamilio ya miaka; yeye ni uumbaji maalum wa Mungu. 

Hapa kuna hatari kuu zaidi katika mfumo mzima wa uibukaji, kama unavyofundishwa kwa watoto wetu katika shule za umma. Unaona, kama mwanadamu aliibuka tu, basi hana tofauti na mbwa au paka. Unamwua, naye hukoma kuishi. Kusingekuwepo ufufuo wa wafu (1 Kor. 15). Hakuna tumaini (Yohana 14:1-3). Hakuna Mungu (Yn. 3:16). Hakuna mbingu ya kupaendea, au hakuna jehanamu ya kuepuka.

“Hakuna msingi wowote wa kudhani kwamba mwanadamu aliibuka kwa viwango vya taratibu vya maendeleo kutoka viumbe wanyama au mimea wa hali ya chini zaidi. Fundisho hilo huhafifisha kazi kuu ya Muumbaji hadi kufikia kiwando cha dhana finyu, za kidunia za mwanadamu. Wanadamu wamekusudia sana kumwondoa Mungu kwenye ujalali wa ulimwengu kiasi kwamba hudhilisha mwanadamu na kumwibia utu wa asili yake.” (Patriarchs and Prophets, uk. 45).

[3] Kutawala—Mwanadamu aliumbwa katika kiwango cha juu zaidi kuliko wanyama. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa katika sura ya Mungu, anaweza kufanya ushirika na Mungu. (Tutazingatia wazo hili katika masomo yajayo)

[4] Kanuni ya Mungu ya Ndoa: —Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke. Ndoa ya jinsi moja (ushoga), pale watu wawili wa jinsi moja wanapofunga ndoa siyo dhana ya Biblia. Ni chukizo kwa Mungu. NI dhambi. Wapendwa, ndoa ilianzishwa kabla ya serikali yoyote, shule, au kanisa. Serikali inaweza kuhalalisha ndoa za namna hiyo, lakini kumbuka kwamba hao SIYO Mungu. Neno la Mungu halina budi kuwa mamlaka fusili (kamili), na siyo serikali. Wapendwa, Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke kwa kusudi la mmoja kwa mwingine. Kanuni ya kiungu ni mwanamume 1 kwa mwanamke 1.

Je Mungu anasema nini kuhusu mahusiano ya ndoa ya jinsi moja, au ushoga? Tangu mwanzo kabisa, tunaona kwamba Mungu anashutumu mwenendo wa jinsi hiyo. Makatazo yafuatayo dhidi ya desturi ya ushoga yameandikwa bayana kwenye Biblia: “Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.” (Walawi 18:22) “Tena mtu mume akilala pamoja na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.” (Walawi 20:13)

Sodoma na Gomora ni majiji makuu ya wakati huo yanayoonesha jinsi Mungu anavyotazama ushoga: “Hata kabla hawajalala, watu wa mji, wenyeji wa Sodoma, wakaizunguka nyumba, vijana kwa wazee, watu wote waliotoka pande zote. Wakamwita Lutu, wakamwambia, Wa wapi wale watu waliokuja kwako usiku huu? Uwatoe kwetu, tupate kuwajua.” (Mwanzo 19:4–5) Mungu aliiadhibuje miji hii? “lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote.” (Luka 17:29)

Sasa kama Mungu aliiadhibu Sodoma, nini kinachokufanya udhani kwamba atakusame (atakuwa na simile kwako)? Kwa kweli, Yuda 7 inasema kwamba hukumu ya Sodoma na Gomora hutumika kama “mfano” wa kila kitakachowapata wote wanaofanya mapenzi ya jinsi moja, au ushoga: “[Wadhalimu wanahukumu kuteseka] kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa [bayana kabisa] kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. (Yuda 7, AMP). Maneno haya hujitosheleza kabisa kuelezea kile kilichotokea. Wapendwa, kama unatenda mambo hayo, tubu dhambi hii mara moja. Yesu anakupenda!

[5] Mwisho, desturi ya ushoga haipatani na ufalme wa Mungu: “Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi. (1 Wakorintho 6:9–10)

SAUTI YA INJILI: Nini mpango wa Mungu kwa ajili ya ndoa? “Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; Naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili Wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.” (Waefeso 5:22–29)

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya?  [1] Usiamini fundisho la uongo kuhusu Uibukaji; [2] Kuhimidi: Msifu Mungu kwa kukuumba katika sura Yake Mwenyewe: “Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo Yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana.” (Zaburi 139:14); [3] Ibada: Kuwa na ushirika pamoja na Mungu. Kumbuka, wewe ni wa pekee, umeumbwa katika sura ya Mungu. [4] Kuwa kama Yesu: “Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa.”

Iweni na Siku Yenye Baraka: “Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.” (Waefeso 2:9–10)

Sauti ya Injili/ Dhima/ Dondoo za Ibada Kuhusu Fundisho la Mwanadamu/ Wazo # 1.