Kujua Kuhusu Mungu Wa Biblia

Kujua Kuhusu Mungu Wa Biblia/ 72-003 (Kutoka 3:14)/ Fundisho Kuhusu Mungu-Seh 3/ Aya Kuu: “Nami nimemjaza Roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina, Mungu akamwambia Musa, MIMI NIKO AMBAYE NIKO; akasema, Ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli; MIMI NIKO amenituma kwenu.” (Kutoka 3:13–14)

Muhtasari wa Somo: [Vile alivyo].

 1. Yeye ni Mungu mnasifi
 2. Yeye ni Mungu mtakatifu
 3. Yeye ni Mungu mwenye rehema
 4. Yeye ni Mungu mwenye haki
 5. Yeye ni Mungu mwenye wivu
 6. Yeye ni Mungu mwaminifu
 7. Yeye ni Mungu mkweli.

Maswali ya Moyoni: Je Mungu wa Biblia ni nani? Tunapataje maarifa kuhusu Mungu wa Biblia?

YEYE NI MUNGU MNASIFI

Hii si tu kwamba humaanisha anajulikana kinasifi bali pia kwamba Yeye ni nafsi. Hebu tudurusu: mara ya mwisho tuliona kwamba washika wote wa Utatu ni nafsi. Kwa hiyo kamwe Mungu siyo ‘kitu’ bali “Yeye.”

[1] Tunapomtambua Mungu wa Biblia kimsingi tunamtaja kwa namna mbili:

 • Kama Elohimu, ambayo hurejelea uwezo Wake na utaabadi, yaani, kwamba ‘anavuka mipaka ya mafiko yetu (1 Wafalme 8:27).
 • Kama Yehova, ambayo hurejelea uwepo Wake binafsi (‘MIMI NIKO AMBAYO NIKO’) na uenevu, yaani, yuko karibu (Kutoka 3:14). Kipengele hiki cha sifa ya Mungu kilikuwa bayana zaidi pale alipodhihirishwa na Yesu kama Baba (Mathayo 6:9; 11:27).

Katika Kiebrania katika ilivyo katika Kiingereza, jina hili “MIMI NIKO” ’ni aina ya kitenzi cha “kuwa,” na hudokeza kwamba mmiliki wake ni mwishinafsi, wa milele (DA 469). “Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, Mimi Niko.” (Yohana 8:58)

Ufunuo-nafsi wa Mungu kuhusu jina Lake hujikita katika utu na uwepo, siyo sifa fulani mahususi. Kisarufi, kirai husika huweza kufasiriwa katika wakati wa sasa (“Mimi NIKO ambaye NIKO”) pamoja na dhana ya ujeo (“Nitakuwa nitakayekuwa”). Huunganisha kwenye ahadi ya uwepo wa Mungu Kut. 3:12.”

“Uwepo wa kiungu (siyo tu uwepo) huweza kuwa kipengele muhimu zaidi katika muktadha huu maalum. Musa na Israeli wanamtafuta Mungu ambaye—bila shaka—amekuwa kimya kwa kipindi kirefu. Neno “BWANA” limejikita katika herufi Konsonanti nne za Kiebrania, ambazo matamshi yake wezekani yalikuwa “Yehova.” Waandishi wa Kiyahudi walilichukulia kuwa takatifu kiasi kwamba hawakuingiza irabu kwenye neno “BWANA,” ili kuepuka kutamka jina la Mungu. Uhusiano wa karibu upo kati ya herufi hizinne na kitenzo “kuwa.” [Jon L. Dybdahl, Ed., Andrews Study Bible Notes, (Berrien Springs, MI: Andrews University Press, 2010), 77].

[2] Mungu wa Biblia hutazamwa kimsingi katika jinsi ya kiume.

 • Nafsi zote katika Utatu huzungumziwa katika jinsi ya kiume.
 • Mungu alipomwumba Adamu, alikuwa katika ‘sura’ ya Mungu hasa (Mwanzo 1:26), hivyo Adamu alikuwa jinsi ya kiume wala siyo mke.
 • Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume (Mwanzo 2:22–23).
 • Jaribu lolote la kumfanya Mungu awe katika jinsi ya kike ni kinyume na ufunuo bayana wa Biblia.

YEYE NI MUNGU MTAKATIFU

“Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.” (Kutoka 3:5) “Kwa kuwa Mimi ni Bwana, Mungu wenu; takaseni nafsi zenu basi; iweni watakatifu, kwa kuwa Mimi ni Mtakatifu; wala msitie uchafu nafsi zenu kwa kitu kitambaacho cha aina yoyote, kiendacho juu ya nchi.” (Walawi 11:44)

[1] Tabia ya Mungu ni kipimo cha kiwango cha utakatifu Wake. Utakatifu hutoka kwa Mungu. Utakatifu wa Mungu ni nini? Ni usharidi (ubora) wa kimaadili unaounganisha hulka Zake. Utakatifu hubainishwa kupitia matendo Yake, ukimtenga na wengine wote.

Kisawe sahihi kwa ajili ya utakatifu ni ‘hali ya kuwa mwingine,’ na humaanisha:

 • Mungu ni ‘mwingine’ kabisa (Kutoka 9:14).
 • Hakuna yeyote mbali na Mungu afananaye na Yeye (Kutoka 15:11).

[2] “Utakatifu wa Mungu haupaswi kuchukuliwa kama hulka moja miongoni mwa zingine; badala yake ni istalahi ya jumla ikiwakilisha dhana ya utimilifu Wake wote na utukufu kamili. Ni ukamilifu Wake halidi wa kimaadili unaoweka upeo wa maarifa na uwezo Wake halidi…. Ukamilifu halidi wa kimaadili ni upeo wa Utatu. Utakatifu ni utukufu kamili wenye upeo huo” (A. A. Hodge). Katika Maandiko, utakatifu utumikao kwa Mungu, kwanza ni usalidi Wake kimaadili, (Law. 11:44; Zab. 145:17), na pili, usajifu (ukuu) Wake kiungu (Isa. 6:3; Zab. 22:3; Ufu. 4:8). – [Alan Cairns, Dictionary of Theological Terms, 2002, 211–212].

[3] Mungu hana dhambi, kasoro au dosari yoyote (angalia Kumbukumbu 32:4).

 • Huchukia dhambi (Kutoka 20:1–17; Zaburi 7:11).
 • Hawezi kufanya kosa (2 Samweli 22:31; Zaburi 18:30).

[4] Hii ndiyo sababu mwanadamu anahitaji mbadala (Habakuki 1:13).

 • Mfumo wa kafara ulianzishwa ili kuonesha siyo tu Mungu wa rehema bali pia ubaya hasa wa dhambi (Waebrania 10:1).
 • Lazima mbadala asiwe na dosari au ila (Kutoka 12:5; Waebrania 4:15; 1 Petro 2:22).

[5] Hii ndiyo sababu watu Wake hawana budi kuwa watakatifu (1 Petro 1:16).

 • Uongofu hupelekea utakatifu (Waefeso 4:22).
 • Utakaso (mchakato wa kuwa mtakatifu) hudaiwa kwa kila mmoja wetu (1 Thes. 4:3).

[6] Utakatifu wa Mungu hauna kifani! Musa anauliza swali muhimu sana: “Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama Wewe? Ni nani aliye kama Wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa Zako, mfanya maajabu?” (Kutoka 15:11), nabii Samweli anaongeza: “Hakuna aliye mtakatifu kama Bwana; Kwa maana hakuna yeyote ila Wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.” (1 Samweli 2:2).

[7] Utakatifu wa Mungu huoneshwa katika tabia Yake (Zab. 22:3; Yn.17:11); jina Lake (Isa 57:15; Luka 1:49); maneno Yake (Zab. 60:6; Yer. 23:9); matendo Yake (Zab. 145:17); na ufalme Wake (Zab. 47:8; Mat 13:41; Ufu. 21:27; 1 Kor. 6:9, 10)

YEYE NI MUNGU MWENYE REHEMA.

[1] Mungu husamehe udhalimu na makosa na dhambi

[2] Ka vile Mungu “husamehe udhalimu na makosa na dhambi,” humaanisha kwamba amechagua kutoadhibu dhambi ajilani.

 • “Akasema, Nitapitisha wema Wangu wote mbele yako, Nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; Nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.” (Kutoka 33:19)
 • “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba.” (2 Petro 3:9)

[3] Yesu Kristo ni Mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu–“bali kwa damu ya thamani, kama ya mwanakondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo. Naye amejulikana kweli tangu zamani, kabla haijawekwa misingi ya dunia; lakini alifunuliwa mwisho wa zamani kwa ajili yenu” (1 Petro 1:19–20)

 • Katika umilele kadimu, kabla Adamu na Hawa kutenda dhambi, Mungu alipanga ukombozi wa wadhambi kupitia Yesu Kristo (cf. Matendo 2:23; 4:27, 28; 2 Tim. 1:9).
 • Mungu ni upendo, Mungu ni uzima. Ni haki ya Mungu kukomboa, kuunda upya, na kurejesha. Kabla ya kuwekwa msingi wa ulimwengu, Mwana wa Mungu alijitoa kufa, na ukombozi ni siri “iliyositirika tangu zamani za milele” (Warumi 16:25). [In Heavenly Places, uk. 291].
 • “Mungu alijua matukio ya ujeo, hata kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Hakufanya makusudi Yake yaendane na mazingira, bali aliruhusu mambo yaendelee na kutendeka. Hakutenda kazi ya kuibua hali fulani ya mambo, bali alijua kwamba hali hizo zingekuwepo.” (SDA BC 6:1082).

[4] Mpango wa ukombozi ulifunuliwa katika Mwanzo 3 — “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na Uzao wake; Huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” (Mwanzo 3:15)

 • “Baada ya kumlaani nyoka halisi, Mungu alirejea kwa nyoka wa kiroho, mshawishi mdanganyifu, Shetani, akamlaani. Utakuponda kichwa … utamjeruhi kisigino. “Injili hii ya kwanza” ni ya kinabii kuhusu pambano na matokeo husika kati ya “uzao wako” (Shetani na wasioamini, waitwao watoto wa Ibilisi katika Yohana 8:44) na Uzao wake (Kristo, mzao wa Hawa, na wale walio ndani Yake), lililoanzisha pale bustanini. Katikati ya andiko hili la laana, ujumbe wa tumaini umebainishwa—uzao wa mwanamume ni Kristo, ambaye siku moja atamshinda Joka. Shetani angeweza tu “kumjeruhi” Kristo kisigino (kumsababishia mateso), ilhali Kristo atakiponda kichwa cha Shetani (atamwangamiza kwa pigo la mauti). Paulo, katika andiko lake akidokeza kwa kina kuhusu Mwa. 3, aliwatia moyo waumini huko Rumi, “Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.” (Rum. 16:20). Waumini wanapaswa kutambua kwamba wanashiriki katika kumseta Shetani kwa sababu, pamoja na Mwokozi wao na wa sababu ya kazi Yake iliyokamilika tayari pale msalabani, wao pia ni uzao wa mwanamke. Kwa maelezo zaidi kuhusu uangamivu wa Shetani, angalia Ebr. 2:14, 15; Ufu. 20:10.” [John MacArthur Jr., Ed., The MacArthur Study Bible, electronic ed., (Nashville, TN: Word Pub., 1997), 20–21].

[5] Rehema ya Mungu ilielekezwa kwa watu Wake, waitwao ‘waliochaguliwa’ au ‘wateule’ (Zaburi 33:12; Warumi 8:33). Walijulikana tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu (Matendo 13:48; Waefeso 1:4). Walichaguliwa kwa neema tu na wala siyo matendo (Warumi 9:11–15; 2 Timotheo 1:9).

[6] Rehema ya Mungu hufunuliwa katika injili –“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda na kuuthamini sana ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye [anayemtumaini, na kudumu Kwake na kumtegemea] asipotee [asipatwe na uangamivu], bali awe na uzima wa milele.” (Yohana 3:16, AMP)

Rehema ya Mungu inaitwa “haki iliyodhihirishwa” (Warumi 1:17). Rehema ya Mungu imehakikishwa kwetu kwa imani pekee (Warumi 4:5).

YEYE NI MUNGU MWENYE HAKI.

Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.” (Kutoka 34:7)

[1] Hii humaanisha haki au usawa–“Haki na hukumu ndio msingi wa kiti Chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso Wako.” (Zaburi 89:14)

 • Huu siyo mtazamo wa mwanadamu kuhusu haki (Isaya 55:8–9).
 • Bali kile ambacho Mungu huita kuwa haki (Zaburi 9:8).

[2] Hii humaanisha lazima aadhibu dhambi (Kutoka 34:7).

 • Hatamsafisha mwenye hatia (Hesabu 14:18).
 • Ulimwengu unahatia mbele ya Mungu (Warumi 3:19).

[3] Mungu huadhibu dhambi kwa njia kadhaa, mfano:

 • Kwa kumruhusu mwanadamua endelee katika dhambi (Warumi 1:26ff.).
 • Kwa kutuma janga fulani (Kumbukumbu 32:35).

[4] Ahadi ya Mungu ajilani kuadhibu dhambi kwa mauti.

 • Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” (Mwanzo 2:17)
 • Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.” (Warumi 6:23)

[5] Adhabu kuu ya dhambi hufanywa kwa njia mbili:

 • Kwa kafara ya damu (Kutoka 12:13).
 • Kwa jehanamu ya moto (Mathayo 25:41).
 • ZINGATIA: “Moto wa milele” umeelezewa kwingineko kama “moto usiozimika” (Mat 3:12) na “moto wa jehanamu.” Maneno haya yote huzungumzia mioto ya siku ya mwisho itakayowaangamiza waovu na matendo yao yote (2 Petro 3:10–12; Ufu. 20:10, 14, 15).

[6] Adhabu ya Mungu duniani huitwa marudi, au kunidhamisha — “Maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye.” (Waebrania 12:6, AMP)

 • Haimpati asiye Mkristo (1 Wakorintho 11:32).
 • Ni kwa Wakristo halisi tu (Waebrania 12:7–11).

YEYE NI MUNGU MWENYE WIVU.

Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa Mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao” (Kutoka 20:5). “Mimi ni Bwana; ndilo jina Langu; na utukufu Wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa Zangu.” (Isaya 42:8)

Dondoo 3 za Haraka:

 • Hatamvumilia hasimu yeyote (Kutoka 34:14).
 • Huchukia aina yoyote ya sanamu (Kumbukumbu 4:23–24; 6:14ff.).
 • Ni mwenye wivu kwa ajili ya watu Wake (Zekaria 1:14; Yakobo 4:5).

YEYE NI MUNGU MWAMINIFU.

Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu Wako ni mkuu.” (Maombolezo 3:23) “Mungu ni mwaminifu (anaweza kutegemewa, kutumainiwa, hivyo ni mkweli daima kwa ahadi Yake, na anaweza kumtarajia) ambaye mliitwa na Yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.” (1 Wakorintho 1:9, AMP)

Dondoo 3 za Haraka:

 • Kamwe hatatuacha wala kututelekeza (Mat. 28:20; Ebr. 13:5).
 • Atatukirimia mahitaji yetu (Filp. 4:19).
 • Atafanya njia ya kutokea katika jaribu au dhiki (1 Kor. 10:13; 2 Pet. 2:9).

YEYE NI MUNGU MKWELI.

Ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika [ahadi na kiapo Chake], ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo wala kutudanganya, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu.” (Waebrania 6:18, AMP)

Dondoo 4 za Haraka:

 • Hudai ukweli tunapojihusisha Naye (Zaburi 51:6).
 • Mwanawe ni Kweli (Yohana 14:6).
 • Roho Wake ni Kweli (Yohana 14:16–17).
 • Maneno Yake ni kweli (Yohana 17:17).

MAANA YA KIIBADA:“Mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.(Kutoka 34:7)

Swali la Moyoni: Je kuna viwango vya dhambi? Je Mungu huona dhambi zote kuwa sawa? Kwa maneno mengine, dhambi moja siyo mbaya zaidi kuliko nyingine, ndivyo? Andiko hili hutufundisha nini kuhusu Mungu rahimu?

Kiwango #1 (DHAMBI): Dhambi humaanisha “kukosa lengo” na ni lugha ya jumla kwa ajili ya kutofikia kiwango cha Mungu. Warumi 3:23 inasema, “wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Dhambi inaweza kuwa ya makusudi au siyo ya makusudi (Hesabu 15:27). Dhambi siyo tu kufanya kitu fulani kibaya, bali pia ni kushindwa kufanya jambo sahihi (Yakobo 4:17).

Kiwango #2 (MAKOSA): Makosa humaanisha kukaidi kwa kusudi au kukiuka amri kwa kudhamiria. Daudi alilkuwa akizungumzia aina hii ya dhambi alipoandika, “Heri aliyesamehewa dhambi, Na kusitiriwa makosa yake.” (Zaburi 32:1). Makosa yanahusiana na ukiukaji, ikiwa na maana uhalifu wa sheria kwa makusudi. Tumepewa sheria ili kutuonesha kosa lilivyo (Wagalatia 3:19).

Baada ya Daudi kutenda dhambi, aliomba, “Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili Zako. Kiasi cha wingi wa rehema Zako, Uyafute makosa yangu.” (Zaburi 51:1) na “Uzifute hatia zangu zote” (Zaburi 51:9). “Kufuta” humaanisha kutowesha au kupangusa herufi na maneno kwa wino au kuyafanya yasionekane au kutambulika.

Wazo ni kufuata makosa yaliyoandikwa kwenye kitabu cha Mungu cha madeni ya dhambi. Kupitia kifo cha Yesu msalabani, alifuta makosa yetu. Wakolosai 2:14 inasema, “akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu Zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani.”

Kiwango #3 (UDHALIMU):  Udhalimu ni upotoshaji wa kweli na mwenendo pindifu unaofikiria na kupanga kutenda dhambi. Udhalimu ni mienendo ya asili inayotusukuma kurudia kutenda dhambi na kunajisi tabia. Mienendo hii potofu bila shaka huweza kurithishwa kizazi hadi kizazi.

Kutoka 20:5 inasema, “Mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.”

Mika 2:1 inasema, “Ole wao wakusudiao mambo maovu, na kutenda mabaya vitandani mwao!” Daudi alipanga kuzini na Bathsheba na kukusudia kumwua Uria mumewe. Baada ya kutubu, Daudi alimlilia Mungu, “Unioshe kabisa na uovu wangu, Unitakase dhambi zangu.” (Zaburi 51:2).

Usengenyaji, umbeya, kulaani, na ukosoaji ni udhalimu. Yakobo 3:6 inasema, “Nao ulimi ni moto; ule ulimwengu wa uovu, ule ulimi, umewekwa katika viungo vyetu, nao ndio uutiao mwili wote unajisi.” Maneno mengi tuyanenayo huweza kusababisha mizizi ya udhalimu kustawi.

Udhalimu hupelekea uasi, kukosa hofu ya Mungu, mihemko isiyo ya asili, na akili potofu (Warumi 1:28-32). “Kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago” (1 Sam. 15:23).

Uasi dhidi ya mamlaka ya kiungu ni udhalimu unaomchukiza Mungu. Machukizo ni aina mbaya kabisa ya udhalimu. Neno hili hutumiwa kipekee kuelezea mambo yanayochukiza, yanayokirihi na yasiyovumilika kabisa—mambo yasiyokubalika kwa Mungu. Baadhi ya machukizo yanayojulikana yameorodheshwa katika Mithali 6:16-19, 12:22, 16:5, Walawi 18:22, 26-27, Kumbukumbu 7:25, 25:16, 27:15.

John Gill akifafanua kuhusu Kut. 34:7 — “mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi” — anasema hivi:

 • “Neno lililotumiwa humaanisha kuinua, na kuondoa: hivyo Yehova ameondoa kutoka kwa mdhambi, na kuweka juu ya Mwanawe, ambaye amebeba, na kuridhika nayo; na kwa kufanya hivyo amepeleka mbali kiasi kwamba haionekani tena; na, kupitia damu Yake kwenye dhamiri ya mdhambi, huondolewa humo, na kupelekwa mbali kama mashariki ilivyo mbali na magharibi; kutoka mahali inakoonekana, kwamba iko katika Kristo, na kwa ajili Yake, kwamba Mungu husamehe dhambi, hata kwa damu yake, haki, na kafara, na utakaso; na msamaha huu ni kwa ajili ya dhambi zote, aina zote za dhambi, dhambi ya asili au halisi, kubwa au ndogo, hadharani au faragha, wazi au siri, ya kutotenda au kutenda, ya moyoni, kwenye ulimi, na maishani.” (John Gill’s Exposition of the Whole Bible)

SAUTI YA INJILI: Wapendwa, hizi hapa habari njema. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zote, makosa yote, udhalimu wote.

Yesu alitoa kafara maisha Yake ili kusamehe dhambi zetu, makosa yetu na udhalimu wetu. “Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu Yake, Na kwa kupigwa Kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu Yake Maovu yetu sisi sote.” (Isaya 53:5–6)

Kwenye msalaba wa Kalvari, Kristo “alitazamwa kama mhalifu” “alihesabiwa pamoja na hao wakosao. Walakini alichukua dhambi za watu wengi, Na kuwaombea wakosaji.” (Isaya 53:12, AMP)

Sisi sote ni “wakosaji” na tunapaswa kuharakisha kumwendea Mungu. Bwana asifiwe kwa sababu ya rehema Yake, aliunda mpango kabla ya msingi wa ulimwengu ili kutufikia sisi, na kutuokoa. “Bali Mungu aonyesha pendo Lake Yeye Mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” (Warumi 5:8)

Wapendwa, licha ya vile moyo wako ulivyopotoka leo, licha ya idadi ya dhambi unazoweza kuwa nao, kifo cha Yesu msalabani kilitosha kabisa kufuta dhambi zako zote. Je utasikiza wito Wake sasa? Anasema –“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.” (Isaya 1:18, AMP)

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya?  [1] Mkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi, kama Mwanakondoo pekee wa Mungu (Yohana 1:29); [2] Tubu matendo/mawazo ya uovu: —udhalimu, makosa na dhambi; [3]Mwombe Bwana akutakase na kukuponya.

Kumbuka: dhambi pekee asiyoweza kuisamehe Mungu ni hatua ya kumkataa Roho Mtakatifu anapokuvuta katika toba (Mathayo 12:32). Bwana akubariki, Amina.

Iweni na Siku Njema: “Alikuja Kwake, wala walio Wake hawakumpokea. Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina Lake” (Yohana 1:11–12)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Utatu/ Somo # 3