Zaburi 90: Mwongozo wa Biblia.

19-BSG-90A: MWONGOZO WA IBADA.

Ibada Ya Alfajiri/ “Mwongozo wa Ibada” unaoshabihiana na Mpango wa Usomaji wa Biblia wa Leo: Zaburi 90/ Somo: “Utujulishe Kuzihesabu Siku Zetu”/ 19-BSG-90A: (Zaburi 90:1-17)/  Wimbo: Niwe nao Uzuri wa Mwokozi (Let the Beauty of Jesus) # 123.

UCHUNGUZI: Basi, Utujulishe Kuzihesabu Siku Zetu (Mh. 9:10; Mt 24:44; Lk 12:35-37; 1 Kor. 1:7-8; 2 Kor. 4:18; Philp. 3:20; Tim 2:11-13; 1 Pet. 4:7; 2 Pet. 3:11)

TAFAKARI: Zaburi hii ni mwanzo wa Kitabu cha Nne. “Zab. 90 imeelezewa kama muziki wa nguvu na wa madhumuni ya Mungu, ikinon’goneza udhaifu na ufupi wa maisha ya mwanadamu. Pengine ni shairi la ajabu zaidi ambalo limeandikwa kwenye majivuno ya maisha ya binadamu, kwa kuzingatia imani ya mtuzi katika ahadi za Mungu” (SDABC 3:841). Mungu ni wa milele lakini binadamu ni wa kupita na kufa (aya aya 1-4). Sisi tunateketezwa na hasira ya Mungu kwa sababu ya dhambi zetu. Maisha yetu ni kama majani: kijani kibichi jua linapochomoza; halafu hukauka na hunyauka katika machweo ya jua (aya  ya 5-6). Siku zetu zimehesabiwa; tumepewa wastani wa miaka sabini tu (aya ya 10). Mungu huona maovu yetu yote, ya siri na ya wazi (aya ya 7-8); siku zetu zimejaa maumivu na shida tele (aya ya 9-11).

MAANA YA KIIBADA: Sura hii inamalizika kwa maneo saba ya sala. Mpendwa nakualika tuzingatie mabo haya saba, nayo ni haya — kufundisha, kurudi (kubatilisha hukumu Yake), kuridhisha, kufurahisa, kudhihirisha, kuuona uzuri wa Bwana, na kuthibitisha. Ninakualika tuyatafakari pamoja hapa chini:

(Zaburi 90:12-17) — 12 Basi, utujulishe (utufundishe) kuzihesabu siku zetu, Tujipatie moyo wa hekima 13 Ee Bwana urudi, hata lini? Uwahurumie watumishi wako, 14 Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako, Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote 15 Utufurahishe kwa kadiri ya siku ulizotutesa, Kama miaka ile tuliyoona mabaya 16 Matendo yako na yaonekane kwa watumishi wako, Na adhama yako kwa watoto wao 17 Na uzuri wa Bwana, Mungu wetu, uwe juu yetu, Na kazi ya mikono yetu utufanyie thabiti, Naam, kazi ya mikono yetu uithibitishe.

HATUA YA MAAMUZI: Ni mwitikio gani unaodhani sura hii ingepaswa kutuhimiza kufanya? [1] Kukiri upendo na utunzaji wa Mungu: Yeye ndiye makao yetu, kimbilio letu, nyumba yetu, na usalama wetu (Zab 90:1); [2] Kukiri kwamba Yeye ndiye Muumba (Zab. 90:2); [3] Kuwa mnyenyekevu! Tambua matatizo ya maisha ya mwanadamu, na utegemezi wako Kwake (Zab. 90:3-11); [4] Kata rufaa kwa Bwana (omba) ili akuhurumie na kukusaidia (Zab. 90:12-17).

SAUTI YA INJILI: Kipengele hiki kimeandikwa kana kwamba Mungu ndiye anaongea nawe, moja kwa moja, kwa sababu hufanya hivyo. Je, Bwana ananiambia nini asubuhi ya leo? Mwanangu, nakupenda sana! Mimi ni BWANA MUNGU. Mimi ni Muumba wako. “Kabla haijazaliwa milima, wala haijaumbwa dunia” Nilikuwepo! “Na tangu milele hata milele” Mimi ndimi MUNGU (Zaburi 90:2). “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa” (Yer. 1:5). Je, tatizo lako ni lipi leo? Je, una mzigo mzito kiasi kwamba hakuna ye yote anayeweza kukusaidia kuutua? Je umechoka? Je, umekata tamaa? Nakualika uulete Kwangu, njoo sasa, Nami nitakusaidia.

MAAMUZI YA LEO: Nitamlilia Bwana—Kunifundisha; Kurudi (kubatilisha Hukumu Yake); Kunishibisha kila asubuhi kwa fadhili Zake; Kudhihirisah uwezo Wake kwangu; Kuuona uzuri wa Bwana; na kuthibitisha kazi ya mikono yangu. Amina.

Uwe Na Siku Yenye Baraka: “Niwe nao uzuri wa Mwokozi, Nazo huruma Zake na usafi; Roho Mtakatifu, anibadilishe; Aonekane Yesu ndani yangu.”[Mtunzi: Albert Orsborn]