Mungu ni Nani katika Biblia?

Mungu ni Nani katika Biblia?/ 2-001 (Kumb. 6:4)/ Fundisho Kuhusu Mungu-Seh 1/ Aya Kuu: “Sikiza, Ee Israeli; Bwana, Mungu wetu, Bwana ndiye mmoja.” (Kumbukumbu 6:4)

KUMTAMBULISHA MUNGU WA BIBLIA

Warumi 1:19–20 huonesha kwamba kwa asili mwanadamu huamini kuwa Mungu yupo. Katika andiko hili kuna rejea kuhusu dhamiri ya mwanadamu— “Kwa kuwa yale yajulikanayo kuhusu Mungu ni dhahiri kwao na yamebainishwa katika ufahamu wao wa ndani, kwa sababu Mungu Mwenyewe amewadhihirishia hilo. Maana tangu uumbaji wa ulimwengu, asili na hulka Yake isiyoonekana, yaani, uwezo na uungu Wake wa milele, vimefafanuliwa na kutambulishwa wazi katika na kupitia vitu vilivyoumbwa ambavyo ni kazi za mikono Yake. Hivyo wanadamu hawana udhuru wala utetezi au simile yoyote.” (Warumi 1:19–20, AMP)

Yohana 1:9 huonesha kwamba hatua pekee ya kubadili moyo wa kila mwanadamu ni Yesu Kristo: “Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.” (Yohana 1:9). Namna tunavyomwamini Mungu ni kupitia Yesu Kristo (1 Petro 1:21). Tena: haukuwepo msingi kuhusu Mungu huko Korintho (1 Wakorintho 2:2); haukuwepo msingi kuhusu Mungu huko Efeso (Waefeso 4:20–21).

Kifupi: Imani katika Mungu huja kwa ufunuo. [1] Kiwango cha kwanza cha ufunuo ni kwa njia ya dhamiri (Warumi 1:20). Dhamiri pekee haitoshi kuokoa (Warumi 2:12); bali inatosha kuhukumu (Warumi 2:15); [2] Kiwango cha pili cha ufunuo ni kwa njia ya Roho Mtakatifu: “Naye akiisha kuja, Huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki (unyofu wa moyo na msimamo sahihi kwa Mungu), na hukumu:” (Yohana 16:8, AMP)

MUNGU NI NANI KATIKA BIBLIA?

[1] Hakuna jaribu lolote la kuthibitisha uwepo wa Mungu kwenye Biblia. Biblia huamini katika uwepo wa Mungu: “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” (Mwanzo 1:1). Tangu mwanzo kabisa, waandishi wa Biblia hawakufanya jaribu lolote la kutetea uwepo wa Mungu, au kuelezea jinsi alivyofanana. Ufahamu wetu kuhusu Mungu lazima “uaminiwe.” Sikiza kile asemacho Yehova kuhusu uumbaji: “Ninyi ni mashahidi Wangu, asema Bwana, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa Mimi ndiye; kabla Yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada Yangu Mimi hatakuwapo mwingine.” (Isaya 43:10)

[2] Njia pekee salama ya kumsadiki Mungu ni kwa imani. Ndiyo, sayansi inaweza kuthibitisha uumbaji siku moja, lakini sayansi haiwezi kamwe kuiruka (kuikwepa) imani kama njia salama. Fundisho kuhusu Mungu na uumbaji hukubaliwa kwa imani: “Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.” (Waebrania 11:3) “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba Yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.” (Waebrania 11:6)

[3] Je tunaweza kuthibitisha Mungu ni nani? Changamoto katika Malaki 3:10 pengine ndiyo ya kina zaidi miongoni mwa waandishi wowote wa Biblia inapokukuja suala la kuthibitisha uwepo wa Mungu. “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba Yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.” (Malaki 3:10)

ZINGATIA: Imani tu katika Mungu kwa namna fulani haithibitishi chochote kwa sababu hata mashetani huamini katika uwepo wa Mungu (Yakobo 2:19); anajua uangamivu wake wa mwisho (Mathayo 8:29); anajua kwamba muda wake ni mfupi (Ufunuo 12:12).

[4] Ni mambo gani mawili huchochea imani? Kulihubiri neno ~ injili ya Yesu Kristo (Warumi 10:14; 1 Wakorintho 1:21); na huduma ya Roho Mtakatifu (Yohana 16:8).

ZINGATIA: Imani huja kwa mapenzi ya Mungu. Mtume Yako anasema –Kwa kupenda Kwake Mwenyewe [utashi wa Mungu Mwenyewe] alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe Vyake (sampuli ya vile alivyoumba ili viwakifishwe Kwake).” (Yakobo 1:18, AMP). Imani, kwa kweli, ni karama ya Mungu kwa mujibu wa Yohana 6:44, 65. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu” (Waefeso 2:8)

Sauti ya Injili/ Mwongozo wa Kujifunza Biblia/ Mafundisho Makuu/ Utatu/ Somo # 2