Tunda la Roho na Uaminifu

TUNDA LA ROHO/ Ibada Ya Usiku/ Uaminifu/ 200F-001 (Gal. 5:22)/ Somo la # 1/ Aya Kuu: “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu.” (Wagalatia 5:22).

Maswali Ya Moyoni: [1] Uaminifu ni nini? [2] Je uaminifu ni tabia muhimu kwa watu wa Mungu? [3] Je tunawezaje kuwa waaminifu?

Uaminifu unafafanuliwa kama “ubora wa kuwa mwaminifu; udilifu.” Uaminifu wa Mungu na neno lake ni mada pana sana katika Bibilia. Lakini tutaangalia uaminifu wa Mungu ‘kama mada’ tegemezi katika masomo ya huko mbeleni. Mtazamo wetu katika mfululizo huu ni kuzingatia matumizi ya uaminifu kwa waumini, yaani — Dhihirisho la uaminifu; Mifano ya kibibilia ya uaminifu; na Uaminifu katika mahusiano ya binadamu.

Somo letu la leo lina kichwa kinachosema “Tunda la Roho ni Uaminifu.” Uaminifu, bila shaka, linatokana na neno “imani.” Imani hutoka kwa Mungu. Wakati fulani wanafunzi walimsihi Bwana wao kuwaongezea imani — (tumaini na imani ambalo chimbuko lake hutokana na imani yetu katika Mungu) (Luka 17:5, AMP). Mtume Paulo anatukumbusha kwamba kila mmoja wetu amepewa “kipimo cha imani” (Rum 12:3). Uaminifu hupinga ‘uzushi” au mafundisho ya uongo. Uaminifu “huamini vitu vyote” (1 Kor 13:7).

Uaminifu ni “ubora wa tabia ambayo humaanisha kusimama kidete katika ahadi ya/ na mtu mwingine au kikundi cha watu, ….  hata katika nyakati za dhiki, upinzani au ukosefu wa uaminifu toka kwa mtu wa upande wa pili au kikundi. Uthabiti huo, kwa upande wake, huzaa matokeo kwa mtu mwaminifu kustahili kuaminiwa.” [Stanley J. Grenz and Jay T. Smith, Pocket Dictionary of Ethics, 2003, 39–40].

Wapendwa, kama tuna Roho wa Mungu, tutakuwa na Matunda ya Roho Mtakatifu katika maisha yetu. Tutakuwa waaminifu – uaminifu kwa Mungu na kwa mwanadamu. Tutakuwa waaminifu kwa maneno yetu na ahadi tunazoweka kwa wengine. Tutaaminiwa au kusadikiwa kwa haraka na wengine. Roho Mtakatifu ataongoza na atashawishi matendo yetu, mitazamo, mawazo, n.k. Tutakuwa waaminifu kwa majirani zetu, marafiki, familia, wazazi, wenzi, watoto, n.k. Tutakuwa waaminifu kwa kazi zetu, mikataba yetu, ajira zetu, majukumu yetu kwa Mungu, talanta zetu, wito wetu wa kuwa “nuru ya ulimwengu” (Mt 5:14). Sikiliza dondoo hii: “Hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa Mkristo ambaye siyo mwaminifu, na madai yote ya kuwa chini ya ushawishi wa Roho wakati uaminifu huo haupo, ni udanganyifu na wa kazi bure.” (Albert Barnes)

Hatua Ya Maamuzi: Ni mwitikio gani unaodhani somo hili lingepaswa kutuhimiza kufanya? Wapendwa — [1] Lazima tuwe waaminifu kwa Mungu; [2] Lazima tuwe waaminifu kwa binadamu mwenzetu; [3] Lazima tuwe waaminifu kwetu wenyewe. Muumini mwaminifu lazima awe tayari kuchunguza hali yake mwenyewe; Lazima awe na hisia ya kina dhidi ya udanganyifu na hatari ya dhambi; Lazima awe na hisia ya utegemezi juu ya Mungu: Kukesha, kuomba na kutafakari Neno Lake wakati wote.

Usiku Mwema:Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana Yeye aliyeahidi ni mwaminifu” (Ebr 10:23).

Sauti ya Injili/ Dhima za Kiibada/ Uaminifu — Dhihirisho la Imani katika Maisha ya kila siku/ Wazo # 1.