46-BSG-1 (1 Wakorintho 1)

Mwongozo wa Biblia
46-BSG-1 (1 Wakorintho 1)
Juni 8, 2018

MASWALI NA MAJIBU.

[1] Je, Paulo alikuwa wapi alipoandika kile tunachokiita sasa waraka wa kwanza kwa Wakorintho? Efeso.

[2] Je, ni mambo gani yalipelekea mtume Paulo kuandika waraka huu?
(a) Fitina, utengano, matabaka.
(b) Zinaa miongoni mwa wakristo.

“Kwa maana, ndugu zangu, nimearifiwa habari zenu na wale walio wa nyumbani mwa Kloe, ya kwamba iko fitina kwenu.” (1 Cor. 1:110

“Yakini habari imeenea ya kuwa kwenu kuna zinaa, na zinaa ya namna isiyokuwako hata katika Mataifa, kwamba mtu awe na mke wa babaye.” (1 Cor 5:1)

[3] Orodhesha mawazo makuu kuu ya sura hii.
(a) Utangulizi (1-9)
(b) Asili ya mgawanyiko katika Korintho (10-17)
(c) Upumbavu wa kujisifu katika hekima ya mwanadamu (18-31)

[4] Nani alijiunga na Paulo katika kushughulikia waraka huu kwa Wakorintho? Sosthenes

[5] Ni jambo lipi moja ambalo Kanisa la Korintho halikupungukiwa? (7) Karama za Roho.

[6] Je, tatizo gani la kwanza kabisa ambalo Paulo anakumbana nalo katika waraka huu? (10) Mgawanyo, matabaka, utengano.

[7] Je, ni nani iliyeripoti tatizo hili kwake? (11) “Wale walio wa nyumbani mwa Kloe.

[8] Je, Paulo alisema nini kuhusu tatizo hili? (12) Alilikemea, akiwakataza wasiwe na matabaka/ vikundi na kuanza kusema: Mimi ni wa Paulo, na, Mimi ni wa Apolo, na, Mimi ni wa Kefa, na, Mimi ni wa Kristo.”

[9] Je, nani alibatizwa na Paulo katika Korintho? (14,16)
(a) Krispo,
(b) Gayo,
(c) Watu wa nyumbani mwa Stefana.

[10] Kwanini Paulo anashukuru kwamba hakubatiza mtu yo yote, mbali na hao waliotajwa? (15) “Mtu asije akasema kwamba mlibatizwa kwa jina langu.”

[11] Taja mitazamo mikuu miwili ya watu kuhusu Injili ya Msalaba? (18)
(a) Upumbavu kwa wale ambao wanaangamia
(b) Nguvu za Mungu kwa wale kuokoka

[12] Je, ni jinsi gani ya mahubiri ya Kristo aliyesulubiwa yalionekana kwa Wayahudi na Wayunani? (23)
(a) Msalaba: Kikwazo kwa Wayahudi
(b) Msalaba: Upumbavu kwa Wayunani

[13] Je, ni kwa jinsi gani Mungu amechagua kuwaaibisha wenye hekima? (27-28) Kwa kutumia yale ambayo mbele ya macho yao ni upumbavu, dhaifu, vitu vinyonge, na kudharauliwa.

[14] Taja faida Nne (4) tunazofurahia kupitia kwa Yesu Kristo (30)
(a) Kristo: Hekima yetu.
(b) Kristo: Haki yetu.
(c) Kristo: Utakatifu wetu.
(d) Kristo: Ukombozi wetu.

[15] Je, twapwaswa kujifia juu ya misingi wa kitu gani pekee? (31) Msalaba wa Kristo. “Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.” (1 Wakorintho 1:31)


 

MWITIKIO WETU.

Nyimbo za Kristo # 134.
Tafuta Daima Utakatifu
(Take Time to be Holy)

1. Tafuta daima utakatifu;
Fanya urafiki na wakristo tu;
Nena siku zote na Bwana wako,
Baraka uombe kwa kila jambo.

2. Tafuta saima utakatifu:
Uwe peke yako ukimwabudu;
Ukimwangalia Mwokozi wako,
Utabadilishwa kama alivyo.

3. Tafuta daima utakatifu;
Kiongozi wako awe Yesu tu;
Katika furaha au huzuni
Dumu kumfuata Yesu Mwokozi.

4.Tafuta daima utakatifu;
Umtawaze Roho moyoni mwako,
Akikuongoza katika haki,
Hufanywa tayari kwa kazi yake.

BWANA AWABARIKI.

Sauti ya Injili SDA © 2018