43-BSG-1 (Yohana 1)

Mwongozo wa Kujifunza Biblia.
Aprili 4, 2018
43-BSG-1 (Yohana 1)

SEHEMU YA I: MASWALI NA MAJIBU

 

[1] Tunaweza kuitaje Yohana 1:1–18? Utangulizi wa Injili ya Yohana.

[2] Hapo mwanzo kulikuwepo nini? “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.” (Yohana 1:1–2)

[3] Kwa nini Yesu anaitwa “Neno”? Kwa sababu Yeye ni ufunuo wa Mungu; Neno Lake humdhihirisha Yeye na tabia Yake.

[4] Ni uthibitisho gani wa uungu Wake unapatika katika Yohana 1:1–3? Anatajwa kuwa “Mungu,” na kwamba alikuwepo “hapo mwanzo” na kwamba “vyote vilifanyika kwa huyo.”

“Katika uwepo Wake kabla tangu milele Neno alikuwa pamoja na Mungu. Tafsiri husika haileti maelezo kamili ya maneno ya Kiyunani (pros ton theon). Kirai hicho hubeba maana ya kina zaidi tu ya kwamba Neno alikuwa pamoja na Mungu; “[huleta] taswira ya nafsi mbili binafsi wakitazamana na kujihusisha katika mazungumzo ya busara” (W. Robert Cook, The Theology of John [Chicago: Moody, 1979], 49). Tangu milele Yesu, kama nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu, alikuwa “pamoja na Baba [pros ton patera]” (1 Yohana 1:2) katika ushirika wa kina na wa karibu sana. Pengine pros ton theon ingeweza kufasiriwa kama “uso-kwa-uso.” Neno ni nafsi, na wala si tabia ya Mungu au mwangaza kutoka Kwake. Naye ni mwenye asili ileile sawa na Baba.” (John MacArthur, The MacArthur New Testament commentary: John 1–11/John 1:1–2)

[5] Je, Yesu anajulikana kwa namna gani pia katika utangulizi wa Yohana? Nuru ya watu.

Uthibitisho wa Biblia:
“Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.” (Yohana 1:4) “Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.” (Yohana 3:19) “Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” (Yohana 8:12)

[5] Tunajuaje injili ni ujumbe wa bure kwa wote? Kwa sababu Yesu Kristo, kama ilivyo nuru, huwafikia wote, “wote wapate kuamini kwa yeye.” Yohana 1:7, 9.

[6] Akina nani hawakumpokea Kristo? Watu Wake Mwenyewe, Wayahudi (1:11). “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.” (Yohana 1:11)

[7] Ni mtu gani aliyetumwa kutoka kwa Mungu? Yohana (Yohana 1:6).

[8] Ni haki wapewayo wale wanaompokea Yesu? (aya ya 12) Ni badiliko gani kuu lifanyikalo ndani yetu tunapoamini kwelikweli? Tunakuwa viumbe vipya katika Kristo, hata “wana wa Mungu.”

“Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake:” (Yohana 1:12)

[9] Nini kinachozungumziwa katika Yohana 1:14? Kufanyika mwili: Mungu katika umbo la mwanadamu, akiishi katika dunia hii, miongoni mwa watu.

“Kristo ni Mungu katika maana kamili na timilifu ya neno husika; Yeye pia ni mwanadamu katika maana hiyohiyo, isipokuwa kwamba “[hakujua] dhambi” (2 Kor. 5:21). Maandiko kwa kurudiarudia na kwa msisitizo hutangaza ukweli huu wa msingi (angalia Luka 1:35; Rum. 1:3; 8:3; Gal. 4:4; Flp. 2:6–8; Kol. 2:9; 1 Tim. 3:16; Ebr. 1:2, 8; 2:14–18; 10:5; 1 Yohana 1:2; nk.; angalia katika Flp. 2:6–8; Kol. 2:9).” (SDA BC 5/ Yohana 1:14)

[10] Yohana anayetajwa katika Yohana 1:15 ni nani? Yohana Mbatizaji.

[11] Nini kilichofanyika mwili? (aya ya 14) Yesu Kristo (angalia “Kufanyika Mwili” hapo juu)

[12] Mungu alileta nini? (aya ya 17) Nini kilichokuja kupitia Yesu Kristo? (aya ya 17) “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.” (Yohana 1:17)

[13] Ni watu gani wawili ambao Yohana alikana kwamba siye? “Naye alikiri, wala hakukana; alikiri kwamba, Mimi siye Kristo. Wakamwuliza, Ni nini basi? U Eliya wewe? Akasema, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.” (Yohana 1:20–21)

[14] Yohana alisemaje juu yake mwenyewe? “Akasema, Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, Inyosheni njia ya Bwana! Kama vile alivyonena nabii Isaya.” (Yohana 1:23)

[15] Mwanakondoo wa Mungu hufanya nini? Huchukua dhambi za ulimwengu (Yohana 1:29).

[16] Yohana alipewa ishara gani ili kumtambua ambaye angebatiza kwa Roho Mtakatifu? (aya ya 33) Mungu wa Mungu katika umbo la hua. “Wala mimi sikumjua; lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyo aliniambia, Yeye ambaye utamwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.” (Yohana 1:33)

[17] Andrea alimleta nani kwa Yesu? (aya ya 40-42)

“Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu. Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo). Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).” (Yohana 1:40–42)

[18] Filipo alishuhudia nini kwa Nathanieli? (aya ya 45)
“Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti.” (Yohana 1:45)

[19] Nini kilichomfanya Nathanieli aamini? (aya ya 48-50)
“Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya.” (Yohana 1:48–50)

[20] Malaika wangekwea na kushuka wapi? (aya ya 51) (Angalia pia Mwa. 28:12)
“Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.” (Yohana 1:51)

[21] Filipo alimpata nani na kumleta kwa Kristo? Nathanaeli.

“Naye Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mwenyeji wa mji wa Andrea na Petro. Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli.” (Yohana 1:44–49)


 

SEHEMU YA II: TAARIFA ZA KUSHANGAZA

Dondoo zifuatazo zimechukuliwa kutoka The Seventh-Day Adventis Bible Commentary, Volume 5/Dondoo ya Ziadaa Juu ya Yohana Sura ya 1 (Mwishoni mwa Sura husika)

1. Utatu Mtakatifu.

Utatu Mtakatifu unaunda na nafasi tatu—Baba wa milele, Bwana Yesu Kristo, Mwana wa Baba wa milele, na Roho Mtakatifu (angalia Mat. 28:19; Yohana 1:1, 2; 6:27; 14:16, 17, 26; Matendo 5:3, 4; Efe. 4:4–6; Ebr. 1:1–3, 8; angalia katika Yohana 1:1–3, 14).

“Kuna nafsi tatu hai katika utatu wa mbinguni…Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu” (Ev 615). Kristo na Baba ni “umoja katika asili, katika tabia, katika kusudi” (PP 34), lakini “si katika nafsi” (8T 269; linganisha 9T 68). Roho Mtakatifu “ni nafsi kama Mungu alivyo nafsi” (Ev 616).

2. Uungu na Uwepo wa Kristo Kabla ya Kuzaliwa.

Kristo ni Mungu katika maana ya juu na kamili ya neno husika—katika asili, katika hekima, katika mamlaka, na katika uwezo (angalia Isa. 9:6; Mika 5:2; Yohana 1:1–3; 8:58; 14:8–11; Kol. 1:15–17; 2:9; Ebr. 1:8; angalia ufafanuzi juu ya Mika 5:2; Mat. 1:1, 23; Luka 1:35; Yohana 1:1–3; 16:28; Flp. 2:6–8; Kol. 2:9).

“Kristo ni Mwana wa Mungu aliyekuwepo kabla hajazaliwa, aishiye kwa uwezo wake mwenyewe… Kamwe hapajawahi kuwepo wakati alipokuwa kwenye ushirika wa karibu pamoja na Mungu wa milele…. Alikuwa sawa na Mungu, asiye na ukomo na mwenye uweza wote” (Ev 615; linganisha DA 469, 470; Ev 614; PP 38, 63).

“Kimsingi Kristo alikuwa Mungu, na katika maana ya juu kabisa. Alikuwa pamoja na Mungu tangu milele zote, Mungu juu ya yote, mbarikiwa milele na milele. Bwana Yesu Kristo, Mwana mtakatifu wa Mungu, alikuwa akiishi tangu milele, nafsi tofauti, hata hivyo mmoja na Baba” (EGW RH April 5, 1906; cf. DA 19).

Angalia Maelezo ya Ziada ya EGW juu ya Yohana 1:1–3, 14; COL 2:9; 3:10.

3. Ubinadamu wa Kristo.

Bwana Yesu Kristo alikuwa mwanadamu halisi na kamili, kama walivyo wanadamu wengine katika hali zote isipokuwa hakutenda dhambi (2 Kor. 5:21; angalia Luka 24:39; Yohana 1:14; Rum. 1:3, 4; 5:15; Gal. 4:4; Flp. 2:7; 1 Tim. 2:5; Ebr. 2:14, 17; 1 Yohana 1:1; 4:2; 2 Yohana 7; angalia ufafanuzi juu ya Mat. 1:23; Yohana 1:14; Flp. 2:6–8).

“Kristo alikuwa mwanadamu halisi” (EGW YI Okt. 13, 1898), “mwanadamu kamili” (EGW ST Juni 17, 1897), “mshirika wa tabia yetu” (EGW RH Feb 18, 1890). “Alikuja kama kitoto kisichojiweza, akibeba ubinadamu tuubebao” (EGW MS 21, 1895), na “na akiwa mshirika wa familia ya mwanadamu alikuwa na uwezo wa kupatwa na mauti” (EGW RH Sept 4, 1900). “Aliwaombea wanafunzi Wake na kwa ajili Yake Mwenyewe, kwa namna hiyo akijihusianisha na mahitaji yetu, madhaifu yetu, kushindwa kwetu” (2T 508; cf. MH 422).

Angalia Maelezo ya Ziada ya EGW juu ya Yohana 1:1–3, 14; Kol. 1:26, 27; Ebr. 2:14–18.

4. Kristo Kufanyika Mwili.

Kufanyika mwili ni muunganiko halisi, kamili, na usiotanguka wa asili ya kiungu na kibinadamu katika nafsi moja, Yesu Kristo, kila asili, hata hivyo, ikidumu bila kubadilika na ikiwa tofauti na nyingine (angalia Mat. 1:20; Luka 1:35; Yn 1:14; Flp. 2:5–8; 1 Tim. 3:16; 1 Yoh 4:2, 3; angalia ufafanuzi wa Mat. 1:18; Yohana 1:14; 16:28; Flp. 2:6–8).
“Kristo alikuwa mwanadamu halisi. … Hata hivyo alikuwa Mungu katika mwili” (EGW YI Okt. 13, 1898). “Uungu Wake ulifichwa katika ubinadamu,—utukufus usioonekana katika umbo la mwanadamu linaloonekana” (DA 23). “Ana asili mbili, kwa pamoja, ya kibinadamu na kiungu” (EGW MS 76, 1903).

“Je, asili ya kibinadamu ya Mwana wa Mariamu ilibadilishwa kuwa asili ya Mwana wa Mungu? Hapana; asili hizo mbili ziliungana kwa namna isiyokuwa ya kawaida katika nafsi moja—Mwanadamu Kristo Yesu” (EGW Letter 280, 1904). “Asili ya ubinadamu haikuchukua nafasi ya ile ya kiungu, wala ya kiungu haikuchukua ile ya kibinadamu” (EGW ST Mei 10, 1899). “Uungu haukushuka hadhi kuwa ubinadamu; uungu ulidumisha mahali pake” (EGW RH Feb 18, 1890).

“Alidhihirisha ubinadamu kamilifu, ukiunganika uungu; … huku akidumisha kila asili ikiwa tofauti” (EGW GCB robo ya 4, 1899, uk. 102).

“Ubinadamu wa Kristo usingeweza kutenganishwa na uungu Wake” (EGW MS 106, 1897).

Angalia Maelezo ya Ziada ya EGW juu ya Yohana 1:1–3, 14; Efe. 3:8; Flp. 2:6–8; Kol. 2:9.

5. Kujisalimisha kwa Kristo.

Kwa hiari akitwaa mipaka ya asili ya kibinadamu wakati wa kufanyika mwili, Bwana Yesu Kristo kwa jinsi hiyo alijisalimisha chini ya Baba kwa kipindi cha huduma Yake duniani (angalia Zab. 40:8; Mat. 26:39; Yohana 3:16; 4:34; 5:19, 30; 12:49; 14:10; 17:4, 8; 2 Kor. 8:9; Flp. 2:7, 8; Ebr. 2:9; anagalia ufafanuzi wa Luka 1:35; 2:49; Yohana 3:16; 4:34; Flp. 2:7, 8).

“Huku akiweka kando vazi Lake la kitawala na taji yake ya kifalme” (9T 68), Mwana wa Mungu “alichagua kurejesha fimbo mikononi mwa Baba, na kushuka kutoka kiti cha enzi cha ulimwengu” (DA 22, 23). “Kwa hiari alijitwalia asili ya kibinadamu. Lilikuwa tendo Lake Mwenyewe, na kwa ridhaa Yake Mwenyewe” (EGW RH Sept 4, 1900). “Yesu alijishusha ili kujinyenyekesha, ili kujitwalia asili ya kibinadamu” (EGW ST Jan. 20, 1890; linganisha 5T 702). “Alijinyenyekesha, na kujitwalia hali ya mauti” (EGW RH Sept 4, 1900).

“Mwana wa Mungu alikuwa amejisalimisha chini ya mapenzi ya Mungu, na alikuwa akitegemea uwezo Wake. Kristo alikuwa amejivua nafsi kabisa kiasi kwamba hakufanya mipango yoyote kwa ajili Yake Mwenyewe. Alikubali mipango ya Mungu kwa ajili Yake, na siku kwa siku Baba alifunua mipango Yake” (DA 208; linganisha 664). “Wakati akibeba asili ya kibinadamu, alikuwa akimtegemea Mungu Mwenyezi kwa ajili ya maisha Yake. Katika ubinadamu Wake, aliushikilia uungu wa Mungu” (EGW ST Juni 17, 1897).

 

HITIMISHO.

“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.” (Yohana 1:14)

Ingawa hapo awali Kristo walikuwa ‘yuna namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu,’ tena ‘[baada ya kuzaliwa katika] mfano wa wanadamu,’ ‘[alionekana] ana umbo kama mwanadamu’ (Flp. 2:6–8). Katika Yeye ‘unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili” (Kol. 2:9); licha ya hayo, ‘ilimpasa kufananishwa na ndugu zake’ (Ebr. 2:17). “Tangu siku za milele Bwana Yesu Kristo alikuwa mmoja na Baba,” lakini “alichagua kurejesha fimbo ya utawala mikononi mwa Baba, na kushuka chini kutoka katika kiti cha enzi cha ulimwengu,” ili “aweze kuishi miongoni mwetu, na kutusaidia tufahamu tabia na maisha Yake ya kiungu” (DA 19, 22, 23).

“Asili mbili, ya kiungu na ubinadamu, ziliunganishwa kwa namna isiyokuwa ya kawaida na kuunda nafsi moja. Uungu ulivishwa ubinadamu, wala haukubadilishwa nao. Kwa namna yoyote ile Kristo hakukoma kuwa Mungu alipokuwa mwanadamu. Asili hizo mbili zilikaribiana na kuwa moja kwa namna isiyoweza kutenganishwa, hata hivyo kila mmoja ilibaki kuwa tofauti. Asili ya kibinadamu haikubadilishwa kuwa asili ya kiungu, wala asili ya kiungu haikubadilishwa kuwa asili ya kibinadamu.” (SDA BC 5/ Yohana 1:14)