Aprili 1, 2018

Saa ya Ibada na Maombi
Aprili 1, 2018

AHADI ZA BWANA
[Ondoleo la Dhambi]

“Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina Lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya.” (Luka 24:46-48)

Sifa/ Shukrani:
[1] Ushindi: Ameshinda Kaburi.
[2] Uhai: Uzima wa Milele.

Maombi ya Jumla:
[1] Wagonjwa kati yetu
[2] Familia zetu.

Maombi Maalum:
[1] Mama anayesumbuliwa na mgongo.
[2] Watoto yatima Tanzania.
[3] Programu ya Kufunga (J5)

Ongeza Jambo Lako Hapa:
[1] ……………..
[2] …………….
[3] …………….

OMBI: Baba, tunalisifu jila Lako kwa ajili ya nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa Yesu Kristo na ushindi aliotupatia pale msalabani. Asante kwa ushindi Wake wa dhambi; kwa maana “uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.” Hivyo Bwana, asubuhi ya leo, tusaidie, tuimarike, tusitikisike, tukazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa twajua ya kwamba taabu yetu siyo bure katika Bwana.” (1 Kor 15:56-58). Tukumbushe kweli hizi za Neno Lako siku zote za maisha yetu…. hadi siku ile Kuu utakaporejea. Asante Bwana, ni katika Jina la Yesu Kristo, tumeomba, Amina.

TIMU YA MAOMBI
(Sauti Ya Injili)