October 8-14, 2017

WIKI HII KATIKA MAOMBI
October 8-14, 2017

MAHITAJI YETU KWA PAMOJA!
Tumshukuru Mungu kwa:-
[1] Upendo wake kwetu.
[2] Msamaha wa dhambi zetu.
[3] Nafasi nyingine ya Uhai.

USHUHUDA/ SIFA.
[1] Mwanangu leo anaendelea vyema, Mbarikiwe sana. (Mama M.)

CHANGAMOTO ZA WATU BINAFSI
[1] Naomba muiombee familia yetu. (Dada R)

[2] Naomba pia tuombee vijana wanaotafuta wenza wa maisha, Mungu akawapatie ubavu halisi. (Dada R)

[3] Tumwombee Baba yangu mroman ili Mungu aweze kumwonyesha nuru; na asimtazame mtu ye yote zaidi ya YESU pale Kalvari. (Dada R)

[4] Mnisaidie kuiomboa familia yangu, imjue Mungu, na ipate kusonga mbele. (Dada S.)

[5] Ofisi nayofanyia kazi inapitia changamoto nyingi kiasi kwamba hata kulipa wafanyakazi kwa wakati inashindwa. Mungu afanye njia hizi changamoto ziondoke. (ML)

[6] Nahitaji maombi, ndoto mbaya zinanitesa nikiamka nimechoka (Dada H)

[7] Ombea ndoa yangu mume anawanawake nje nyumba ndogo (Dada H)

[8] Mimi naitwa Gift, na mume wangu anaitwa Musa. Muombeeni each,… “Zarau na Kuninyanyasa, .. ana wanawake wengi” (Gift)

[9] Mimi ni Yusta, naomba miombee: Kukua kiroho; Familia yangu; na Malengo yangu binafsi. Mungu anisaidie yatimie (Yusta)

[10] Nahitaji amani ktk moyo wangu, sina kabisa amani. (Dada)

[11] Nahitaji Mume, ila awe Mume mwenye hofu ya Mungu! (Dada)

[13] Nahitaji mafanikio, na nikipata pesa niifanyie jambo la maana. (Dada)

[14] Nahitaji mwanangu ambaye ndio uzao wangu wa kwanza, … Mungu akamfanye kichwa na wala si mkia. Mungu amsimamie maisha yake yote. Asije badilika, akawa mtoto asiyeeleweka. (Dada)

[15] Napenda nimfahamu Mungu zaidi (Dada)

[16] Tumuombee kaka yetu kule Dar Es Salaam, kwa ajili ya Vipimo na Tiba (Kaka S)

 

ONGEZA USHUHUDA/ HITAJI LAKO HAPO CHINI
[17] ……………..
[18] …………….
[19] …………….
[20] …………….

 

AHADI ZA BWANA:
“6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. 7 Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” (Wafilipi 4:6-7)

UKUMBUSHO:
[1] Jumatano: (Maombi na Kufunga)
[2] Tumia “initials” baada ya kuandika ombo lako; Yaani (Herufi ya Kwanza na ya Mwisho). Mfano: Paulo Silas …. (P.S.)
[3] Kipidi cha Maombi ni kila Siku Alfajiri; Lakini hata kama hutakuwa hewani, Timu ya Maombi… itaendelea kuombea changamoto uliyo nayo; Hivyo, usisite kutuma Ombi lako.

OMBI: Ee Bwana, sikia vilio vya watoto Wako, toka mlima wako Mtakatifu. Ukawatendee Bwana, sawasawa na Fadhili Zako. Tusamehe dhambi, uovu na kasoro zetu zote, Bwana. Ukatusafishe na Kututakasa kwa damu Yako – ili tufae kuitwa watoto Wako. Tumeomba haya katika Jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina.

HUDUMA YA MAOMBI
Sauti Ya Injili
Timu Ya Maombi