ABC’s za Maombi (1/5)

Saa ya Ibada na Maombi
ABC’s za Maombi (1/5)
Mfululizo: 99A. 001-031.

 

MAOMBI YANAAMRIWA KATIKA BIBLIA.
99A-001
Muundo: Sauti

“Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu.” (Isaya 55:6)

“Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; Kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.” (Mathayo 7:7-8)

“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” (Wafilipi 4:6-7)

TUFANYE NINI BASI?
[1] Tutubu dhambi zetu
[2] Tumtafute Bwana
[3] Tuliite Jina Lake
[4] Tuombee wengine
[5] Weka ombi lako hapo chini.

 

SAUTI YA INJILI
{Hebu sikia sauti ya Bwana ikinena nasi tunapoanza siku hii}

Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.” (Isaya 55:6-7)

 

BWANA ATUBARIKI SOTE!


 

MAOMBI YAELEKEZWE KWA MUNGU.
99A-002
Muundo: Sauti

“Ee Bwana, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye. Bwana, asubuhi utaisikia sauti yangu, Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.” (Zaburi 5:1-3)

MWITO WA LEO:

“Bwana ametamalaki, mataifa wanatetemeka; Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika. Bwana katika Sayuni ni mkuu, Naye ametukuka juu ya mataifa yote. Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa; Ndiye mtakatifu.” (Zaburi 99:1-3)

 

SAUTI YA INJILI
{Hebu sikia sauti ya Bwana ikinena nasi tunapoanza siku hii}

“Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu Yeye peke yake. Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.” (Mathayo 4:10-11)