BABA WA REHEMA (1/2)

Injili Ya Asubuhi
Mwezi: Agosti
Mfululizo: 101A-001-031

 

REHEMA: KARAMA YA UADUI
101A-001
Mwanzo 3:15
“Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino”


 

REHEMA IKAWAFUNIKA
101A-002
Mwanzo 3:20-21
“20 Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai. 21 Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika”


 

REHEMA IKAWAREHEMU
101A-003
Mwanzo 3:22-24
“22 Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; 23 kwa hiyo Bwana Mungu akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa. 24 Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.”


 

REHEMA: ALAMA YA KAINI
101A-004
Mwanzo 4:13 – 15
“13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki. 14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua. 15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.”


 

REHEMA KABLA YA GHARIKA
101A-005
Mwanzo 6:5-8
“5 Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. 6 Bwana akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. 7 Bwana akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya. 8 Lakini Nuhu akapata neema machoni pa Bwana.”


 

REHEMA KWA LUTU
101A-006
Mwanzo 19:15-17
“15 Hata alfajiri ndipo malaika wakamhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. 16 Akakawia-kawia; nao wale watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, na mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyomhurumia, wakamtoa wakamweka nje ya mji. 17 Ikawa walipomtoa nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako usitazame nyuma, wala usisimame katika hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea.”


 

REHEMA KWA YUSUFU
101A-007
Mwanzo 41:37- 41
“37 Neno hilo likawa jema machoni pa Farao, na machoni pa watumwa wake wote. 38 Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu kama huyu, mwenye roho ya Mungu ndani yake? 39 Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe. 40 Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neno lako watu wangu watatawaliwa. Katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. 41 Farao akamwambia Yusufu, Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.”


 

REHEMA KWA WAEBRANIA
101A-008
Kutoka 2:23-25
“23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa. 24 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo. 25 Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.”


 

REHEMA: KUVUKA BAHARI YA SHAMU.
101A-009
Kutoka 14:10-13
“10 Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana. 11 Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? 12 Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani. 13 Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.”


 

KWA REHEMA YAKO UMETUKOMBOA
101A-010
Kutoka 15:11 – 13
“11 Ee Bwana, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? 12 Ulinyosha mkono wako wa kuume, Nchi ikawameza. 13 Wewe kwa rehema zako umewaongoza watu uliowakomboa, Kwa uweza wako uliwaelekeza hata makao yako matakatifu.”


REHEMA: ILI NIPATE KUKAA KATI YAO
Msimbo: 101A-011
Kutoka 25:8 – 9
“8 Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao. 9 Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya.”


KITI CHA REHEMA
101A-012
Kutoka 25:17-22
“17 Nawe fanya kiti cha rehema cha dhahabu safi; urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu. 18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.”


 

NITAMREHEMU YEYE NITAKAYEMREHEMU
101A-013
Kutoka 33: 19
“17 Bwana akamwambia Musa, Nitafanya na neno hili ulilolinena, kwa maana umepata neema mbele zangu, nami nakujua jina lako. 18 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. 19 Akasema, Nitapitisha wema Wangu wote mbele yako, Nami nitalitangaza jina la Bwana mbele yako; Nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.”


 

MWINGI WA REHEMA NA KWELI
101A-014
Kutoka 34: 6 -7
“6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.”


LAKINI WEWE U MWINGI WA REHEMA
101A-015
Nehemia 9:16-17
“16 Lakini wao na baba zetu wakatakabari, wakafanya shingo zao kuwa ngumu, wala hawakuzisikiliza amri zako, 17 ila wakakataa kutii, wala hawakuyakumbuka maajabu yako, uliyoyafanya kati yao; lakini wakafanya shingo zao kuwa ngumu, na katika kuasi kwao wakaweka jemadari, ili wairudie hali ya utumwa; lakini wewe u Mungu, uliye tayari kusamehe, mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, basi hukuwaacha.”


BABA WA REHEMA
101A-016
2 Wakorintho 1:3
“3 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote; 4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.”


REHEMA NA MSAMAHA
101A-017
Danieli 9:9-10
“9 Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi; 10 wala hatukuitii sauti ya Bwana, Mungu wetu, kwa kwenda katika sheria zake, alizoziweka mbele yetu kwa kinywa cha watumishi wake, manabii.”


KWA KUWA REHEMA ZAKE NI NYINGI
101A-018
2 Samweli 24:14
“Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na tuanguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu.”


REHEMA KWA ISRAELI
101A-019
Nehemia 9:30-31
“30 Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza; kwa hiyo ukawatia katika mikono ya watu wa nchi. 31 Ila kwa rehema zako nyingi hukuwakomesha kabisa, wala kuwaacha; kwa maana wewe u Mungu mwenye neema, mwenye rehema.”


 

KWA WINGI WA FADHILI ZAKO
101A-020
Zaburi 5:7
“Bali mimi, kwa wingi wa fadhili Zako, Nitaingia nyumbani Mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu Lako takatifu.”


 

REHEMA KWA ISRAELI MUASI
101A-021
Yeremia 3:12
“Enenda, ukatangaze maneno haya kuelekea upande wa kaskazini, ukaseme, Rudi, Ee Israeli mwenye kuasi, asema Bwana; sitakutazama kwa hasira; maana Mimi ni mwenye rehema, asema Bwana, sitashika hasira hata milele.”


NEEMA, REHEMA, NA AMANI
101A-022
1 Timotheo 1:1-2
“1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa amri ya Mungu Mwokozi wetu na Kristo Yesu, taraja letu; 2 kwa Timotheo, mwanangu hasa katika imani. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.”


BWANA NI MWINGI WA REHEMA NA HURUMA
101A-023
Yakobo 5:11
“Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”


AMBAYE KWA REHEMA ZAKE NYINGI
101A-024
1 Petro 1:3-5
“3 Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu; 4 tupate na urithi usioharibika, usio na uchafu, usionyauka, uliotunzwa mbinguni kwa ajili yenu. 5 Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.”


REHEMA KWA YONA
101A-025
Yona 1:14-17
“14 Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. 15 Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. 16 Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri. 17 Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku.”


REHEMA KWA WATU WA NINAWI.
101A-026
Yona 3:1-3, 10
1 Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, 2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru. 3 Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. 10 Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya. Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.”

Zaburi 86:15
“Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.”

Zaburi 103:8
“Bwana amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.”


REHEMA: YONA NA MTANGO
101A-027
Yona 4:1-3
“1 Lakini jambo hili lilimchukiza Yona sana, naye akakasirika. 2 Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. 3 Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.”


 

REHEMA YAKE NI KUBWA
101A-028
Hesabu 14:18-19
“18 Bwana ni mpole wa hasira, mwingi wa rehema, mwenye kusamehe uovu na makosa, naye hatamfanya mwenye hatia kuwa hana makosa kwa njia yo yote; mwenye kuwapatiliza wana kwa uovu wa baba zao, katika kizazi cha tatu na cha nne. 19 Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa. 20 Bwana akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa”


 

MUNGU: UTAJIRI WA REHEMA
101A-029
Waefeso 2:4-9
“4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi Yake makuu aliyotupenda; 5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. 6 Akatufufua pamoja Naye, akatuketisha pamoja Naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; 7 ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema Yake upitao kiasi kwa wema Wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. 8 Kwa maana mmeokolewa kwa Neema, kwa njia ya Imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.”


 

REHEMA: UKAWAPA WAOKOZI WALIOWAOKOA
101A-030
Nehemia 9:27
“26 Walakini hawakukutii, wakakuasi, wakaitupa sheria Yako nyuma yao, wakawaua manabii Wako walioshuhudu juu yao wapate kuwarejeza Kwako; wakatenda machukizo makuu. 27 Kwa sababu hiyo ukawatia katika mikono ya adui zao, waliowasumbua; na wakati wa shida yao, walipokulilia, uliwasikia kutoka mbinguni; na kwa wingi wa rehema zako ukawapa waokozi waliowaokoa katika mikono ya adui zao.”


REHEMA NA HAKI MSALABANI
101A-031

Zaburi 85:10
“Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana.”

Psalm 85:10 (NKJV)
“Mercy and truth have met together; Righteousness and peace have kissed.”

 

Haki na Huruma wakasimama mbali, wakipingana kila mmoja, wakitenganishwa na Ghuba pana. {Sons and Daughters of God, uk. 243}

Pale msalabani tunaona Rehema na Haki ya Mungu.

[a] HAKI (Mungu anahukumu kwa Haki):

“Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23); na Kristo lazima afe msalabani. Tukumbuke ombi la Kristo Gethsemane: “Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nitakavyo Mimi, bali kama utakavyo Wewe.” (Mathayo 26:39b).

Pale msalabani tunaona jinsi Kristo alivyochukua nafasi yetu, akawa Mbadala wetu, akakinywea kikombe, akafa kwa ajili yetu.

[b] REHEMA (Mungu ni Mwenye Rehema):

Mfano: Umepanda basi, mmefika mbali nje ya mji (porini), kuna wanyama wakali, n.k; kondakta ananza kukusanya nauli za abiria; anafika kwenye kiti chako na unajikuta huna hela za kulipa. Swali muhimu: Je, asimamishe gari, akutoe nje na kukuacha pale, au atoe sehemu ya mshahara wake, kulipa fidia kwa ajili ya nauli yako? Kumbuka: Lazima hatoe hesabu sahihi kwa mwenye mali (tajiri wake). Kwa huruma kuu, kondakta anaamua kukulipia nauli. Wapendwa hii ni Rehema.

Rehema ya Mungu kwetu ilidhihirishwa dhahiri msalabani, Rehema hii kuu, si kwa ajili ya Kristo, la hasha!; ni kwa ajili yetu; kwa sababu tusamehewa, tukapatanishwa na Mungu wetu.

Warumi 5:8-11
“8 Bali Mungu aonyesha pendo lake Yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.”

“9 Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa Yeye. 10 Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake.”

11 Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.


 

MWITIKIO WETU

MSALABA WA YESU
Nyimbo Za Kristo # 120:

[1] Msalaba wa Yesu, Nikae karibu;
Pale pana chemichemi Ya kuponya dhambi.

Pale msalaba Msalaba wake,
Huo Ni sifa yangu, Kwa maisha yote.

[2] Karibu msalaba Nalitetemeka,
Pendo likaniona Likanirehemu.

[3] Unikumbushe Yesu, Nikuone pale;
Niupate upendo Na kuvutwa nao.

[4] Karibu msalaba, Kwa kutegemea,
Kukesha na kungoja, Nitaka pale.

 

Sauti Ya Injili SDA © 2017