Roho Mtakatifu

Mahubiri Mafupi: Roho Mtakatifu katika kurasa za Biblia.

137-001: “JUU YA USO WA VILINDI VYA MAJI”

Mwanzo 1:1-3
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi. 2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji. 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.


137-002: “NA TUMFANYE MTU KWA MFANO WETU”

Mwanzo 1:26-27

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. 27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.