135-002: Mawakala

VITA KUU KATI YA KRISTO NA SHETANI

Sehemu ya I: Malaika, Shetani, Mapepo

Mfululizo # 135:001-044

Sehemu ya I: Malaika, Shetani, Mapepo

Mada ya Leo: 135-002

MALAIKA KAMA MAWAKALA WA WOKOVU WA MUNGU

OMBI: Baba yetu mpendwa, asante kwa zawadi ya neno Lako. Tunaalika Roho wako atuongoze katika tafakari ya somo hili. Tusamehe makosa, uovu, na dhambi. Tuandae kwa ajili ya ufalme wako. Tumeomba haya katika jina la Yesu Kristo-Bwana wetu, Amina.


 

Muhtasari wa Mawazo Makuu
(1) Mawakala wa wokovu wa Mungu
(2) Wokovu dhidi ya maadui
(3) Malaika kama mashahidi wa agano
(4) Waelekezaji wa mapenzi ya Mungu
(5) Wawasilishaji wa maelekezo ya Mungu
(6) Hitimisho
(7) Sauti Ya Injili

 

MALAIKA KAMA MAWAKALA WA WOKOVU WA MUNGU

Waebrania 1:14
Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?

Kutoka 23:23
22 Lakini ukiisikiza sauti yake kweli, na kuyatenda yote ninenayo mimi; ndipo mimi nitakuwa ni adui wa adui zako, na mtesi wa hao wakutesao. 23 Kwa kuwa malaika wangu atatangulia mbele yako, na kukufikisha kwenye Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mkanaani, na Mhivi, na Myebusi; nami nitawakatilia mbali.

Kutoka 32:34
Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika Wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.

Kutoka 33: 2
1 Bwana akanena na Musa, Haya, ondokeni, katokeni hapo, wewe na hao watu uliowaleta wakwee kutoka nchi ya Misri, waende nchi hiyo niliyomwapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, niliposema, Nitakipa kizazi chako nchi hii; 2 Nami nitamtuma malaika aende mbele yako; nami nitawafukuza Mkanaani, na Mwamori, na Mhiti, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi;

Hesabu 20:14-16
14 Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata; 15 jinsi baba zetu walivyotelemkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mwingi, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia; 16 tena tulipomlilia Bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho;

Isaya 63:8-9
8 Maana alisema, “Hakika ndio watu Wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.” 9 Katika mateso yao yote Yeye aliteswa, na malaika wa uso Wake akawaokoa; kwa mapenzi Yake, na huruma Zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.

 

 

MALAIKA WANAWAOKOA WATU WA MUNGU DHIDI YA MAADUI ZAO

2 Wafalme19:35
Ikawa usiku uo huo malaika wa Bwana alitoka, akakiingia kituo cha Waashuri, akawapiga watu mia na themanini na tano elfu. Na watu walipoondoka asubuhi na mapema, kumbe! Hao walikuwa maiti wote pia.

2 Nyakati 32: 21
Naye Bwana akatuma malaika aliyewakatia mbali mashujaa wote, na majemadari, na maakida, matuoni mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake mwenye haya ya uso. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, wale waliotoka viunoni mwake mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.

Isaya 37:36
Basi malaika wa Bwana alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.

Matendo 5:19
18 Wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; 19 lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa (cf. Matendo 12:6-11)

 

 

MALAIKA KAMA MASHAHIDI WA AGANO

Matendo 7:53
Ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike.

Matendo 7:38
Yeye ndiye aliyekuwa katika kanisa jangwani pamoja na yule malaika aliyesema naye katika mlima wa Sinai, tena pamoja na baba zetu; ndiye aliyepokea maneno ya uzima atupe sisi.

Wagalatia 3:19
Torati ni nini basi? Iliingizwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi; iliamriwa kwa utumishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe.

ANAGLIZO:
“Ilikuwa Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye aliyetoa sheria kwenye mlima Sinai (soma Kutoka 20:2). Pia alikuwa Malaika wa agano (soma Kutoka 23:20). Lakini malaika wengi sana walikuwa na Bwana katika mlima wa Sinai wakishuhudia” (cf. Torati 33: 2; Zaburi 68:17; Gal 3:19; Waebrania 2:2).” SDA BC Vol. 6

 

 

MALAIKA KAMA WAELEKEZAJI WA MAPENZI YA MUNGU

Zekaria 1:8-10
8 Naliona wakati wa usiku, na tazama, mtu amepanda farasi mwekundu, akasimama kati ya mihadasi iliyokuwa mahali penye uvuli; na nyuma yake walikuwapo farasi wengine wekundu, na wa rangi ya kijivujivu, na weupe. 9 Ndipo nikasema, Ee Bwana wangu, ni nini hawa? Basi yule malaika aliyesema nami akaniambia, Nitakuonyesha ni nini hawa. 10 Na yule mtu aliyesimama kati ya mihadasi akajibu, akasema, Hawa ndio Bwana aliowatuma, waende huko na huko duniani.

Danieli 7:15-16
15 Basi, mimi Danielii, roho yangu ilihuzunika mwilini mwangu, na hayo maono ya kichwa changu yakanifadhaisha. 16 Nikamkaribia mmoja wa hao waliosimama karibu, nikamwuliza maana ya kweli ya hayo yote. Basi akaniambia, akanijulisha tafsiri ya mambo hayo.
Ufunuo 17:1
Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi.

Ufunuo 21:9
Akaja mmoja wa wale malaika saba waliokuwa na vile vitasa saba vilivyojaa yale mapigo saba ya mwisho, naye akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo.

 

MALAIKA HUWASILISHA MAELEKEZO YA MUNGU

Zekaria 3:4
Naye huyo akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi zenye uchafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani nyingi.
Hesabu 22:21-35

Zekaria 3:6-7
6 Kisha malaika wa Bwana akamshuhudia Yoshua, akisema, 7 Bwana wa majeshi asema hivi, Kama ukienda katika njia zangu, na kama ukishika maagizo yangu, ndipo utakapoihukumu nyumba yangu, nawe utazilinda nyua zangu, nami nitakupa nafasi ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.

Matayo 2:13
Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.

Wagalatia 1:8
Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe.

 

MALAIKA HUTIMIZA MAELEKEZO YA MUNGU

Ufunuo 7:1-2
2 Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, 3 akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao.
Ufunuo 15:1
Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.

 

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO LA LEO?

Mshukuru Bwana kwa ulinzi wa malaika zake

Zaburi 34:7-9
7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8 Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
9 Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.

 

SAUTI YA INJILI

Waebrania 2:1-3a
1 Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. 2 Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, 3 Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?

 

MWISHO.

Sauti Ya Injili SDA © 2017