98:001-030 [Injili Ya Asubuhi]

INJILI YA ASUBUHI
Mfululizo # 98:001-030
Mwezi: June
Kitengo: Vishazi katika Biblia (part 1)

 


98-001 ABBA BABA
Warumi 8:15
14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. 15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. 16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; 17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.

 


98-002 KUKAA NDANI YAKE
1 Yohana 2:6
Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani Yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama Yeye alivyoenenda.


 

98-003 KUKAA NDANI YANGU
Yohan 15:5-5
4 Kaeni ndani Yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. 5 Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani Yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo Mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.


 

98-004 KAENI KATIKA PENDO LANGU
Yohana 15:9-10
9 Kama vile Baba alivyonipenda Mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo Langu. 10 Mkizishika amri Zangu, mtakaa katika pendo Langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba Yangu na kukaa katika pendo Lake.


98-005 KAENI KATIKA NENO LANGU
Yohana 8:29-32
29 Naye aliyenipeleka Yu pamoja Nami, hakuniacha peke Yangu; kwa sababu nafanya sikuzote yale yampendezayo. 30 Naye alipokuwa akisema hayo, wengi walimwamini. 31 Basi Yesu akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno Langu, mmekuwa wanafunzi Wangu kweli kweli; 32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.


98-006 KAENI NDANI YA MWANA
1 Yohana 2:23-25
23 Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia. 24 Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba. 25 Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.


 

98-007 ILI AKAE NANYI HATA MILELE
Yohana 14:16-18
16 Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu. 18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu.


98-008 WAKAA MILELE
Zaburi 9:7
Bali Bwana atakaa milele, Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.

Zaburi 125:1-2
1 Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. 2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo Bwana anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.


98-009 AKAAYE NDANI YAKE
Yohana 3:6,9
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. 9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.


98-010 AKAAYE KATIKA PENDO
1 Yohana 4:16-21

16 Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

17 Katika hili pendo limekamilishwa kwetu, ili tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.

18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo. 19 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza.

20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.21 Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.


98-011 HUKAA NDANI YANGU
Yohana 6:55-58
55 Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56 Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. 57 Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. 58 Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.


98-012 AWEZA KUTUOKOA
Danieli 3:16-18
16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili. 17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. 18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.


98-013 AWEZAYE KUFANYA VITA NAYE?
Ufunuo 13:4
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?


 

98-014 LIWEZALO KUZIOKOA ROHO ZENU.

Yakobo 1:21-22
21 Kwa hiyo wekeeni mbali uchafu wote na ubaya uzidio, na kupokea kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. 22 Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

Waebrania 7:24-25 [Aweza Kuwaokoa Kabisa]
24 Bali Yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani Wake usioondoka. 25 Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa Yeye; maana Yu hai sikuzote ili awaombee.


98-015 NANI ANGESIMAMA?
Zaburi 130:3-4
3 Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? 4 Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.

Zaburi 1:5-6
5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki. 6 Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea.


98-016 CHUKIZO LA UHARIBIFU
Danieli 9:24-27
24 Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.
26 Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.
27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.


 

98-017 CHUKIZO KWA BWANA
Mithali 15:8
Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.


 

98-018 MWINGI WA FADHILI NA KWELI
Zaburi 86:12-17
12 Nitakusifu Wewe, Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.
13 Maana fadhili zako kwangu ni nyingi sana; Umeiopoa nafsi yangu na kuzimu.
14 Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Mkutano wa wakatili wamenitafuta roho. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.
15 Lakini Wewe, Bwana, U Mungu wa rehema na neema, Mvumilivu, mwingi wa fadhili na kweli.
16 Unielekee na kunifadhili mimi; Mpe mtumishi wako nguvu zako, Umwokoe mwana wa mjakazi wako.
17 Unifanyie ishara ya wema, Wanichukiao waione na kuaibishwa. Kwa kuwa Wewe, Bwana, Umenisaidia na kunifariji.


98-019 KWA MAPENZI YAKE MAKUU ALIYOTUPENDA
Waefeso 2:4-5
4 Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; 5 hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.

Warumi 8:37-39
37 Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda.

38 Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, 39 wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.


 

98-020 JUU YA MIUNGU YOTE
Kutoka 18:8-11
8 Musa akamwambia mkwewe mambo hayo yote Bwana aliyomtenda Farao na Wamisri kwa ajili ya Israeli, na mambo mazito yote yaliyowapata njiani, na jinsi Bwana alivyowaokoa. 9 Yethro alifurahi kwa ajili ya wema wote Bwana aliowatendea Israeli, kwa alivyo waokoa mikononi mwa Wamisri.

10 Kisha Yethro akasema, Na ahimidiwe Bwana aliyewaokoa na mikono ya Wamisri, na mkono wa Farao; aliyewaokoa watu hao watoke mikononi mwa Wamisri. 11 Sasa najua ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa unyeti.


98-021 IBRAHIMU, RAFIKI YANGU.
Isaya 41:8-10
8 Nawe, Israeli, mtumishi wangu; Yakobo, niliyekuchagua; mzao wa Ibrahimu, rafiki yangu; 9 wewe niliyekushika toka miisho ya dunia, na kukuita toka pembe zake, nikikuambia, Wewe u mtumishi wangu; nimekuchagua wala sikukutupa;

10 Usiogope, kwa maana Mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana Mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki Yangu.


98-022 IBRAHIMU BABA YENU
Mwanzo 26:3, 24; 28:13
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.

24 Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.

13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.

Isaya 51:2
Mwangalieni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa; kwa maana alipokuwa mmoja tu nalimwita, nikambariki, nikamfanya kuwa wengi.

Yohana 8:56
Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi.


 

98-023 TUNAKAA MBALI NA BWANA. [absent from the Lord]

2 Wakorintho 5:5-9
5 Basi Yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho.
6 Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana.
7 (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.)

8 Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.
9 Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza Yeye.

10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.


98-024 JITENGENI NA UBAYA WA KILA NAMNA

Mambo Saba Ya Kujitenga Nayo:
(a) Unajisi wa sanamu (Matendo 15:20)
(b) Uasherati (Matendo 15:20,29; 1 Thessalonians 4:2-3)
(c) Nyama zilizosongolewa (Matendo 15:20)
(d) Damu [Eating blood] (Matendo 15:20)
(e) Nyama; au ‘Vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu’ (Matendo 15:29)
(f) Ubaya wa kila namna (1 Wathesalonike 5:22)
(g) Tamaa za mwili zipiganazo na roho (1 Petro 2:11)

 

1 Wathesalonike 5:15-22

15 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.
16 Furahini siku zote;
17 Ombeni bila kukoma;
18 Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.
19 Msimzimishe Roho;
20 Msitweze unabii;
21 Jaribuni mambo yote; lishikeni lililo jema;
22 Jitengeni na ubaya wa kila namna.


 

98-025 KWA WINGI WA AMANI.
Zaburi 37:11
Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.


 

98-026 YAUJAZAYO MOYO (Abundance of the Heart)
Mathayo 12:34
Enyi wazao wa nyoka, mwawezaje kunena mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


 

98-027 MWINGI WA REHEMA

Kutoka 34:5-6
5 Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana.

6 Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli; 7 mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne.


98-028 WINGI WA MAFANIKIO
Msisitizo: “Abundant Prosperity” = Prosperity Gospel
Injili ya Mafanikio/ ufanisi wa maisha.
Je Biblia inasema nini kuhusu mada hii?

Zaburi 37:11
11 Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.


98-029 KUKUBALI MANENO YANGU
Yohana 12:44-48
44 Naye Yesu akapaza sauti, akasema, Yeye aniaminiye Mimi, haniamini Mimi bali Yeye aliyenipeleka.
45 Naye anitazamaye Mimi amtazama Yeye aliyenipeleka.
46 Mimi nimekuja ili niwe nuru ya ulimwengu, ili kila mtu aniaminiye Mimi asikae gizani.
47 Na mtu akiyasikia maneno Yangu, asiyashike, Mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, ila niuokoe ulimwengu.

48 Yeye anikataaye Mimi, asiyeyakubali maneno Yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


98-030 MWAKA WA BWANA ULIOKUBALIWA
Isaya 61:1-2
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. 2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao.

Luka 4:15-20
15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.

16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. 17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, 19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.


 

Sauti Ya Injili SDA © 2017