5/15/17: Maombi

CHUMBA CHA MAOMBI

 

CHANGAMOTO ZA KUOMBEA LEO:
Jumatatu
May 15, 2017

(Uongozi) Tuombe uinjilisti wa TMI (Total Member Involvement)

(Uongozi) Ombea uinjilisti kwa njia hii ya mtandao, ili watu wapate Injili, waokolewe, waingie mbinguni.

(Uongozi) Ombea Vipindi vya wiki hii, na maandalizi ya kina ya masomo yaliyo katika ratiba wiki hii.

(Uongozi) Ombea mwamko wa Ibada na Maombi kila siku katika huduma hii.

(Zern) “Naombeni maombeni yenu napitia changamoto za kiuchumi”

(David) “Naomba mniombee kuna nyumba fulani naifuatilia, kama ni mapenzi ya Mungu, niipate”

(Utume Gerezani) Tumuombee mtumishi wa Bwana, Mr. Eliot Kisagwa anapoendelea kusimamia huduma hii. Bwana amtangulie katika huduma hii njema na takatifu mbele Zake.


 

USHUHUDA/ SHUKRANI:

(Sote) Tumshukuru Mungu kwa msamaha wa dhambi zetu, kwani sisi sote tu wenye dhambi, tunaohitaji msamaha Wake.  Tukumbuke wapendwa: “Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno Lake halimo mwetu.” (1 Yohana 1:10)

(Sote) Tunamshukuru Mungu kwa nafasi nyingine ya uhai leo.

(Bundara) Kitabu chake cha Geography kitakaguliwa kesho kama “kimekidhi vigezo”; Bwana asifiwe kwa hatua hii.

 

AGIZO LA KUOMBEA WENGINE

Waefeso 6:18
Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”


 

TUNAALIKWA KUFANYA YAFUATAYO:

[1] Ombea wapendwa hawa
[2] Weka Ombi (Text/Audio)
[3] Weka Ushuhuda wako
[4] Weka hitaji lako
[5] Weka nyimbo za Sifa
[6] Jikabidhi kwa Mungu wako sasa

 

KUMBUKA: Kutoa taarifa Ombi lako linapokuwa limejibiwa, ili tuliondoe katika list hii.

Ee Bwana twaomba usikie sala zetu toka mlima Wako mtakatifu, na ukatutendee sisi watoto Wako, sawasawa na fadhili Zako. Tunaomba haya katika jina la Kristo Yesu, Bwana wetu, Amina.

CHUMBA CHA MAOMBI

Sauti Ya Injili SDA © 2017