5/8/17: Maombi

CHUMBA CHA MAOMBI
http://tgvs.org/archives/2702

Zaburi 25:4-5
4 Ee Bwana, unijulishe njia Zako, Unifundishe mapito Yako, 5 Uniongoze katika kweli Yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.

 

CHANGAMOTO ZA KUOMBEA LEO:
Jumatatu
May 8, 2017

 

(Uongozi) Ombea watahiniwa/ mitiani ya kidato cha Sita inayoendelea sasa hivi.

(Uongozi) Ombea faraja kwa familia zote ambazo watoto wao walipata ajali Juzi huko Arusha.

(Uongozi) Tuombe uinjilisti wa TMI (Total Member Involvement)

(Hyansita) “Niombeeni kwa habar ya madeni nina madeni mengi yananikosesha amani”

(Lawrence) “Naomba mniombe niwe na moyo mwepesi wa kumtolea Bwana Mungu wetu zaka na sadaka”

(Lawrence) “Mniombee kwa ajiri ya changamoto za maisha, na kujazwa na Roho Mtakatifu”

(Elda) Wapendwa mama angu anaumwa tumuombee

(Hawa) “Naomba Roho Mtakatifu anitie nguvu niweze kuomba na mimi”

(Mavanza) “Mungu anipe kibari cha kutumika mbele zake”; pia “Afya njema”

(Eliot) “Nina Dada yangu anaitwa Rahel ni mgonjwa wa mda mrefu anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa na ngozi yake kuwa na ukurutu wakati mwingine mwili wote unageuka kuwa kijivu”

(Ivasam) “Najiandaa na mitihani ya kumaliza chuo lkn kichwa kimekuwa kizito kuelewa na usiku usingizi unanielemea ninapo panga kuamka na kusoma”

(Violeth) “Maombi yenu wapendwa nasumbuliwa na macho”

(Simon) “Ada ya Simon bado haijapatikana na deadline imepita; Tafadhali niombeen wapendwa nahitaj kumaliza chuo mwaka huu kwa Neema ya Mungu”.

(Leah) “Mama yangu ni mgonjwa naomba tumwombee majina Juliana Erasto

(Leah) “Nami mnikumbuke napitia changamoto nzito sana Bwana anitie nguvu”

(Joseph) “Naomba Mungu anifungulie mibaraka Yake, anipe akili, hekima pamoja na Upendo katika yote”

(Rachel) “Nina mgonjwa yuko muhimbili alipata ajali tumkumbuke kwa maombi”

(Toni) “Tuombee wanafunzi ambao wako kwenye changamoto za ada na vitu vingine”

(Esrom) “Tuombee Mahubiri ya TMI yatakayorindima June 2017”

(Utume Gerezani) Tunahitaji fedha kwa ajili ya kusaidia wenzetu waliofungwa ili nao wapate Injili, waokolewe, waupate uzima wa milele.

(Echelesi) Ombea huyu mpendwa ili bosi wake ampatie ruhusa ya kwenda Ibada, siku ya Sabato.

(Bundara) “Nahitaji mwenzi wangu wa maisha, Bwana akapate kunitendea sawa sawa Na niombavyo”

(Bundara) Fedha kwa ajili ya kutoa kitabu cha Geography anachokiandaa kichapishwe by mwezi November, 2017; “ili kitoke, kikawasaidie wengine ambao nao wana hitaji la kupata elimu”

(David) “Niombeeni wapendwa nipate nyumba fulani itakayouzwa mwezi July, 2017. Kama ni mapenzi ya Mungu, nifanikiwe kupata hicho kibanda”

(Bundara) Tuombe Kwa ajili ya wangonjwa Pande nne za Dunia Bwana akawaponye maana Yeye ni mponyaji: “Walio kifoni nenda waponyeni”

(Ley) Tumuombee kwa “changamoto ya kutumia madawa ya kulevya na kufunguliwa macho ya kiroho.”

(Joseph) “Naomba kuomba baraka za Mungu ziwe pamoja nami kwa kila kazi/ biashara nitakayo shika na ikafanikiwe mara dufu kwa Utukufu Wake.”

(Joseph) “Niwatakie uponyaji wa haraka wote wenye kukata tamaa kwa matatizo ya kiafya”


 

USHUHUDA/ SHUKRANI:

(Joseph) “Naomba kumshukuru Mungu kwa kuniokoa kwenye ajali ya Pikipiki niliyo pata juzi.”

(Oliver) “Namshukuru Mungu amejibu maombi ndugu yangu anaendeleaje vizuri

(Oliver) “Na Mimi presha imeshuka Bwana Yesu apewe Sifa”

(Yuster) “Namshukuru Mungu kwa afya njema kwa cku nzima jina Lake litukuzwe”


 

AGIZO LA KUOMBEA WENGINE

Waefeso 6:18
Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote

 

 

TUNAALIKWA KUFANYA YAFUATAYO:
[1] Ombea wapendwa hawa
[2] Weka Ombi (Text/Audio)
[3] Weka Ushuhuda wako
[4] Weka hitaji lako
[5] Weka nyimbo za Sifa
[6] Jikabidhi kwa Mungu wako sasa

KUMBUKA: Kutoa taarifa Ombi lako linapokuwa limejibiwa, ili tuliondoe katika list hii.
Ee Bwana twaomba usikie sala zetu toka mlima Wako mtakatifu, na ukatutendee sisi watoto Wako, sawasawa na fadhili Zako. Tunaomba haya katika jina la Kristo Yesu, Bwana wetu, Amina.
CHUMBA CHA MAOMBI

Sauti Ya Injili SDA © 2017