5/3/17: Hukumu na watu wa Mungu

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA

http://tgvs.org/archives/2695
Robo hii: Lisha Kondoo Zangu
Kitabu: 1 Petro & 2 Petro
Somo la (6/13): Kuteseka kwa ajili ya Kristo

Fungu la Kukariri: “Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.”(1 Petro 2:21).

OMBI: Baba yetu mpendwa, asante kwa nafasi nyingine ya tafakari ya neno Lako. Tunaomba Roho Wako atufundishe saa hii, Bwana. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tuandae kwa ajili ya ufalme Wako. Tunaomba katika Jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina!


 

Jumatano: (5/3/17)

HUKUMU NA WATU WA MUNGU

SWALI # 1: Linganisha 1 Petro 4:17-19 na Isaya 10:11, 12 na Malaki 3:1-6. Ni kitu gani aya hizi zinakisema kwa pamoja?

1 Petro 4:17-19
17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje?

18 Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?

19 Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.
Isaya 10:11, 12
11 je! Sitautenda Yerusalemu na sanamu zake vile vile kama nilivyoutenda Samaria na sanamu zake?

12 Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Malaki 3:1-6
1 Angalieni, namtuma mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia, angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi.

2 Lakini ni nani atakayestahimili siku ya kuja kwake? Au ni nani atakayesimama atakapoonekana yeye? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo;

3 naye ataketi kama asafishaye fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na fedha; nao watamtolea Bwana dhabihu katika haki.

4 Wakati ule ndipo dhabihu za Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na kama katika miaka ya zamani.

5 Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.

6 Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.

 

JIBU: [Maelezo ya Mwandishi]

Katika aya hizi zote, mchakato wa hukumu unaelezwa kuwa unaanza na watu wa Mungu. Petro anahusisha mateso ya wasomaji wake na hukumu ya Mungu. Kwake, mateso ambayo wasomaji wake Wakristo wanapitia yanaweza yasiwe kitu zaidi ya hukumu ya Mungu, ambayo huanza katika nyumba ya Mungu. “Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, kama kwa Muumba mwaminifu.” (1 Petro 4:19).

 
SWALI #2: Soma Luka 18:1-8. Hili hutusaidiaje kufahamu hukumu ya Mungu?

Luka 18:1-8.
1 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.

2 Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu.

3 Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu.

4 Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu,

5 lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima.

6 Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.

7 Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?

8 Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?

 

Katika nyakati za kibiblia, hukumu kwa kawaida ilikuwa ni kitu kinachotakiwa sana. Taswira ya mjane maskini katika Luka 18:1-8 huvutia fikra pana kuelekea katika hukumu. Mjane anafahamu kuwa atashinda katika daawa yake iwapo tu atampata hakimu ambaye atachukua kesi yake. Ana pesa kidogo na hadhi ndogo kuweza kusukuma mbele kesi yake, lakini hatimaye anamsihi hakimu apate kusikiliza kesi yake na kumpatia kilicho stahili yake. Kama Yesu anavyosema, “Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao?” (Luka 18:7). Dhambi imeleta uovu duniani, na watu wa Mungu katika zama zote wamesubiri kwa muda mrefu ili Mungu afanye tena mambo kuwa mema.

Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina Lako? Kwa kuwa Wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele Zako; kwa kuwa matendo Yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.” (Ufunuo 15:4).

 
MASWALI YA KUFIKIRIA ZAIDI

SWALI # 3: Fikiri juu ya uovu wote katika ulimwengu ambao umepita na bado unaendelea bila kuadhibiwa. Kwa nini, basi, dhana ya haki, na hukumu ya haki ya Mungu ni ya muhimu kiasi hicho kwetu kama Wakristo?

SWALI # 4: Unapata tumaini gani kutoka katika ahadi kwamba haki itatendeka?
MWISHO.