5/3/17

CHUMBA CHA MAOMBI
http://tgvs.org/archives/2688

Zaburi 119:10-11
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo Yako.

11 Moyoni mwangu nimeliweka neno Lako, Nisije nikakutenda dhambi.


 

CHANGAMOTO ZA KUOMBEA LEO:
Jumatano
May 3, 2017
(Uongozi) Ombea watahiniwa/ mitiani ya kidato cha Sita inayoendelea sasa hivi.

(Uongozi) Ombea serikali ya Tanzania, Kenya, Uganda – “Bwana awape hekima viongozi wetu”

(Olivaladis) “Nauguliwa na ndugu yangu; na Mimi mwenyewe presha inapanda sana.”

(Hawa) “Naomba Roho Mtakatifu anitie nguvu niweze kuomba na mimi”

(Mavanza) “Mungu anipe kibari cha kutumika mbele zake”; pia “Afya njema”

(Eliot) “Nina Dada yangu anaitwa Rahel ni mgonjwa wa mda mrefu anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa na ngozi yake kuwa na ukurutu wakati mwingine mwili wote unageuka kuwa kijivu”

(Ivasam) “Najiandaa na mitihani ya kumaliza chuo lkn kichwa kimekuwa kizito kuelewa na usiku usingizi unanielemea ninapo panga kuamka na kusoma”

(Violeth) “Maombi yenu wapendwa nasumbuliwa na macho”

(Simon) “Ada ya Simon bado haijapatikana na deadline imepita; Tafadhali niombeen wapendwa nahitaj kumaliza chuo mwaka huu kwa Neema ya Mungu”.

(Leah) “Mama yangu ni mgonjwa naomba tumwombee majina Juliana Erasto

(Leah) “Nami mnikumbuke napitia changamoto nzito sana Bwana anitie nguvu”

(Joseph) “Naomba Mungu anifungulie mibaraka Yake, anipe akili, hekima pamoja na Upendo katika yote”

(Rachel) “Nina mgonjwa yuko muhimbili alipata ajali tumkumbuke kwa maombi”

(Toni) “Tuombee wanafunzi ambao wako kwenye changamoto za ada na vitu vingine”

(Esrom) “Tuombee Mahubiri ya TMI yatakayorindima June 2017”

(Utume Gerezani) Tunahitaji fedha kwa ajili ya kusaidia wenzetu waliofungwa ili nao wapate Injili, waokolewe, waupate uzima wa milele.

(Echelesi) Ombea huyu mpendwa ili bosi wake ampatie ruhusa ya kwenda Ibada, siku ya Sabato.

(Bundara) “Nahitaji mwenzi wangu wa maisha, Bwana akapate kunitendea sawa sawa Na niombavyo”

(Bundara) Fedha kwa ajili ya kutoa kitabu cha Geography anachokiandaa kichapishwe by mwezi November, 2017; “ili kitoke, kikawasaidie wengine ambao nao wana hitaji la kupata elimu”

(David) “Niombeeni wapendwa nipate nyumba fulani itakayouzwa mwezi July, 2017. Kama ni mapenzi ya Mungu, nifanikiwe kupata hicho kibanda”

SHUKRANI:
(Emma) Tulimwombea juzi, na aamefika salama salamini DAR; Jina la Bwana lihimidiwe!

(Joseph) Ametatua migogoro ya kifamilia iliyokuwa inamkabili.


 

AGIZO LA KUOMBEA WENGINE

Waefeso 6:18
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”
TUNAALIKWA KUFANYA YAFUATAYO:
[1] Ombea wapendwa hawa
[2] Weka Ombi (Text/Audio)
[3] Weka Ushuhuda wako
[4] Weka hitaji lako
[5] Weka nyimbo za Sifa
[6] Jikabidhi kwa Mungu wako sasa

KUMBUKA: Kutoa taarifa Ombi lako linapokuwa limejibiwa, ili tuliondoe katika list hii.
Ee Bwana twaomba usikie sala zetu toka mlima Wako mtakatifu, na ukatutendee sisi watoto Wako, sawasawa na fadhili Zako. Tunaomba haya katika jina la Kristo Yesu, Bwana wetu, Amina.

CHUMBA CHA MAOMBI
Sauti Ya Injili SDA © 2017