5/2/17: Jaribio Kali

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA

http://tgvs.org/archives/2684
Robo hii: Lisha Kondoo Zangu
Kitabu: 1 Petro & 2 Petro
Somo la (6/13): Kuteseka kwa ajili ya Kristo

Fungu la Kukariri: “Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.”(1 Petro 2:21).

OMBI: Baba yetu mpendwa, asante kwa nafasi nyingine ya tafakari ya neno Lako. Tunaomba Roho Wako atufundishe saa hii, Bwana. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tuandae kwa ajili ya ufalme Wako. Tunaomba katika Jina la Yesu Kristo, Bwana wetu, Amina!


 

Jumanne: (5/2/17)

JARIBIO KALI (The Fiery Trial)

SWALI # 1: Kwa nini Petro anasema kuwa hawapaswi kuona mateso yao kuwa ni ajabu?

1 Petro 4:12-14

12 Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. 13 Lakini kama mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 14 Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia.

JIBU: (Maelezo Ya Mwandishi)

Petro anaweka wazi kuwa mateso kwa ajili ya kuwa Mkristo ni kushiriki mateso ya Kristo. Si jambo la kutokutegemewa. Kinyume chake, kama Paulo alivyoandika: “Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa.” (2 Timotheo 3:12). Yesu mwenyewe aliwaonya wafuasi wake kuhusu kile ambacho wangekikabili: “Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu. Ndipo wengi watakapojikwaa, nao watasalitiana, na kuchukiana.” (Mathayo 24:9, 10).

Kulingana na Ellen G. White: “Ndivyo itakavyokuwa kwa wale wote wanaoishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu. Mateso na lawama yanawasubiri wote ambao wamejazwa na Roho ya Kristo. Aina ya mateso hubadilika kulingana na wakati, lakini kanuni –roho iliyo chanzo chake- ni ile ile ambayo imewaua wateule wa Bwana tangu zamani za siku za Habili.”—The Acts of the Apostles, uk. 576.

 

ANGALIA MAFUNGU HAYA:

2 Timotheo 3:12
Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya utauwa katika Kristo Yesu wataudhiwa

Yohana 15:18
Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia Mimi kabla ya kuwachukia ninyi.

 

SWALI # 2: Soma Ufunuo 12:17. Inasema nini kuhusu uhalisi wa mateso kwa Wakristo katika siku za mwisho?

Ufunuo 12:17
Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari.

 

SWALI # 3: Tunaweza kufanya kitu gani ili kuwatia moyo, kuwatumainisha, na hata kuwasaidia wale ambao wanateseka kwa sababu ya imani yao?

JIBU: Songa Mbele Kwa Imani.

1 Petro 4:12
Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho.

Hakuna swali, kwa Mkristo mwaminifu, mateso yanaweza kuwa ni ukweli uliopo siku zote, ambacho ndicho kitu Petro anashughulika nacho hapa katika kuwaonya wasomaji wake kuhusu “majaribio makali [kama moto KJV], BHN” waliokabiliwa nayo.

Moto ulikuwa ni sitiari njema kutumika (kama ilivyo katika Biblia ya Kiingereza KJV). Moto unaweza kuwa mharibifu, lakini pia unaweza kusafisha uchafu. Inategemea ni kitu gani kilicho ndani ya moto huo. Nyumba zinaharibiwa na moto; fedha na dhahabu husafishwa nayo. Ingawaje haipasi mtu kuleta mateso kwa makusudi, Mungu anaweza kuleta jambo jema kutokana nayo. Kwa hiyo, Petro anawaambia wasomaji wake (na sisi pia): Ndiyo, mateso ni mabaya, lakini usikatishwe tamaa kutokana nayo kana kwamba ni kitu ambacho hakikutegemewa. SONGA MBELE KWA IMANI.

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO HILI?

1 Petro 1:6
Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali

Yakobo 1:2-3
2 Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; 3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Luka 22:28
Nanyi ndinyi mliodumu pamoja nami katika majaribu yangu.

 

AHADI YA BWANA

Ufunuo 3:10
Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

 

SAUTI YA INJILI

(Hebu sikiliza sauti ya Bwana kwako, tunapofunga kipindi hiki)

Yakobo 1:12
Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


 

WIMBO WA MWISHO

Mbele yetu iko saa,
Ya kuja-a ribiwa;
Ijayo kwa Ulimwengu,
Kuwajaribu wakaao,

Chorus:
Tazama naja upesi;
Ulicho nacho shikeni;
Hata nitakaporudi;
Tazama naja upesi.


WHERE HE MAY LEAD ME I WILL GO

Where He may lead me I will go,
For I have learned to trust Him so,
And I remember ’twas for me,
That He was slain on Calvary.

Refrain

Jesus shall lead me night and day,
Jesus shall lead me all the way,
He is the truest Friend to me,
For I remember Calvary.

O I delight in His command,
Love to be led by His dear hand;
His divine will is sweet to me,
Hallowed by bloodstained Calvary.

Onward I go, nor doubt nor fear,
Happy with Christ my Savior near,
Trusting that I some day shall see,
Jesus my Friend of Calvary.


MWISHO.

Sauti Ya Injili SDA © 2017