Si Mimi Niliyekutuma

SI MIMI NINAYEKUTUMA?
Jumapili
April 30, 2017

Bwana akamtazama,akasema, Enenda kwa uwezo wako huu…..Je! Si Mimi ninayekutuma? {Waamuzi 6:14}

Kwa Gidion ulikuja wito wa kimbingu wa kuwakomboa watu Wake. Kwa wakati huo alikuwa akishughulika na kazi ya kupura ngano. Kiasi kidogo cha nafaka hii kilikuwa kimefichwa na pasipo kuthubutu kuipuria eneo la wazi katika sakafu ya kawaida ya kupuria alikuwa amekwenda kwenye eneo fulani karibu na shinikizo la zabibu :kwa maana msimu wa zabibu mbivu ulikuwa bado ungali mbali, sasa uangalizi mdogo ilikuwa ukifanywa juu ya mashamba ya mizabibu. Wakati Gidion akitenda kazi kwa siri na utulivu ,kwa huzuni alitafakari juu ya hali ya Israel na kufikiria jinsi ambavyo nira ya watesi wao ungeweza kuvunjwa kutoka kwa watu wake.

Kwa ghafla {malaika wa Bwana } akajitokeza na kuzungumza naye akimwambia ( BWANA yu pamoja nawe ,Ee shujaa) (Ee Bwana wangu) ndilo lililokuwa jibu lake, (ikiwa Bwana yu pamoja nasi,mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu,waliyotuhadithia baba zetu wakisema, Je! Siye Bwana aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa ,naye ametutia katika mikono ya Midiani). Yule mjumbe wa Mbinguni akajibu, Enenda kwa uwezo wako huu ,ukawaokoe Israel na mkono wa Midiani . Je si Mimi ninayekutuma?

Gidion aliguswa sana na halo take mwenyewe ya kutotosheleza kwa ajili ya kazi kuu iliyoko mbele yake .. Kwa kawaida Bwana hamchagui kwa ajili ya kazi yake watu wenye uwezo mkubwa sana. Lakin huwachagua wale anaoweza kuwatumia kwa namba bora zaidi .

Watu wanaoweza kufanya kazi njema kwa ajili ya Mungu. Wanaweza kwa wakati fulani kuachwa katika giza , huenda kwa namna fulani pasipo kuonekana wala kutumiwa na Bwana wao . Lakini kama akitenda kwa uaminifu wajibu wa nafsi yao duni waliyonayo wakidumisha utayari wa kutenda kazi na kujitolea kwa ajili yake , katika wakati wake Mwenyewe yeye atawakabidhi wajibu mkubwa zaidi.

Kabla ya heshima kuna unyenyekevu . Bwana anaweza kuwatumia kwa ufanisi zaidi wale walio na utambuzi wa kina zaidi juu ya kutofaa kwako wenyewe na kutotosheleza . Atawafundisha jinsi ya kuenenda kwa ujasiri wa imani . Atawafanya wawe imara kwa kuunganisha udhaifu wao katika nguvu yake . Atawafanya kuwa na hekima kwa kuunganisha kuyokujua kwao pamoja na hekima yake.