4-30-17

CHUMBA CHA MAOMBI

Mathayo 18:19
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba Yangu aliye mbinguni.

 

CHANGAMOTO ZA KUOMBEA LEO:
Jumapili
Aprili 30, 2017

(Uongozi) Ombea umoja na mshikamano katika kazi ya Bwana

(Uongozi) Ombea huduma ya Sauti ya Injili/ The Gospel’s Voice.

(Uongozi) Ombea utayarishaji wa masomo ya Biblia.

(Joseph) “Naomba Mungu anifungulie mibaraka Yake, anipe akili, hekima pamoja na Upendo katika yote”

(Rachel) “Nina mgonjwa yuko muhimbili alipata ajali tumkumbuke kwa maombi”

(Toni) “Tuombee wanafunzi ambao wako kwenye changamoto za ada na vitu vingine”

(Esrom) “Tuombee Mahubiri ya TMI yatakayorindima June 2017”

(Utume Kwa Wafungwa) “Tunahitaji VOP Course 500 @ 1500 Tsh; Vitabu 500 vya kugawa Kwa wafungwa @ 2000 Tsh. Tunahitaji fedha kwa ajili ya kusaidia wenzetu waliofungwa ili nao wapate Injili, waokolewe, waupate uzima wa milele.

(Joseph) “Nahitaji maombi kwa jamii yetu kwa ujumla dhidi ya changamoto mbalimbali kuhusu: Mali mzazi aliyoacha ghafula baada ya kifo, inaaingiliwa pasipo kufuatwa sheria za Umiliki, na mzigo imebaki kwangu kulitwaa ili ziwe salama kwa wadogo wangu, Lakini vikwazo vipo, [Nahitaji Ujasiri na hekima kuzinasua kwa Amani!]

(Echelesi) Ombea huyu mpendwa ili bosi wake ampatie ruhusa ya kwenda Ibada, siku ya Sabato.

(Bundara) “Nahitaji mwenzi wangu wa maisha, Bwana akapate kunitendea sawa sawa Na niombavyo”

(Bundara) Fedha kwa ajili ya kutoa kitabu cha Geography anachokiandaa kichapishwe by mwezi November, 2017; “ili kitoke, kikawasaidie wengine ambao nao wana hitaji la kupata elimu”

(Emma) Tumuombee anapokuwa safarini leo kutoka Musoma kuelekea Dar.

 

AGIZO LA KUOMBEA WENGINE
Waefeso 6:18
“Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote”

 

TUNAALIKWA KUFANYA YAFUATAYO:
[1] Ombea wapendwa hawa
[2] Weka Ombi (Text/Audio)
[3] Weka Ushuhuda wako
[4] Weka hitaji lako
[5] Weka nyimbo za Sifa
[6] Jikabidhi kwa Mungu wako sasa

Ee Bwana ukasikie sala zetu toka mlima Wako mtakatifu, na ukatutendee sisi watoto Wako sawasawa na fadhili Zako. Tunaomba haya katika jina la Kristo Yesu, Bwana wetu, Amina.


 

Simon Lukas

Mtakatifu, Mtakatifu,Mtakatifu….Mungu baba uketie mahali pajuu sana Mbinguni, Jina lako takatfu litukuzwe

Baba, ni saa na wakati tena tunawiwa kusalimisha maisha yetu kwako, kwa kuwa wewe ndiwe Mungu upasaye kuabudiwa kwa haki..Ahsante sana kwa namna hii ya pekee,

Baba wakati huu tunaposalimisha maisha yetu kwako,, wapo wana na binti zako wanachangamoto mbalimbali na asbh ya leo hawana pakupeleka changamoto zao zaid yako baba🙏🏻

Baba mwema yupo mmoja anahitaji kupata mwezi wa maisha yake,, lakin yupo anayehitaji kupata karo na michango mbalimbali kwa ajili ya elimu yake,, lakini tunaye mmoja anahitaji fedha kwa ajili ya uchapishaji wa kitabu, baba mwngine anahitaji kupata uhuru wa kukuabud kwa roho na kweli,, lakin baba Mjori wako Joseph anahitaji ombi kwa ajili changamoto za mali(mirathi) baba mwongoze mwanao awe na hekima na busara anaposhughulikia hili jambo.

Baba tunaomba kwa ajili ya utume&unjilisti magerezani, uongozi katika group hili tunaukabidhi mikonon mwako,, lakin hatutawasahau wagonjwa, tunaowafaham na wale tusiowafahamu,, wote wapate uponyi na jina lako takatifu litukuzwe
Tunaomba haya yote tukiamin ktk jina la Yesu, amen