123: 008-014: Injili Ya Asubuhi

123-008: USINITUPE WAKATI WA UZEE

Zaburi 71:9
Usinitupe wakati wa uzee, Nguvu zangu zipungukapo usiniache.


123-009: ALIVYOKUWA KATIKA DHIKI

Luka 22:40-44
40 Alipofika mahali pale aliwaambia, Ombeni kwamba msiingie majaribuni. 41 Mwenyewe akajitenga nao kama kiasi cha kutupa jiwe, akapiga magoti akaomba, 42 akisema, Ee Baba, ikiwa ni mapenzi Yako, uniondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi Yangu, bali Yako yatendeke. 43 Malaika kutoka mbinguni akamtokea akamtia nguvu. 44 Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; hari yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini


123-010: WATAKAPOPATANA DUNIANI

 

Matayo 18:19-20
19 Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba Yangu aliye mbinguni. 20 Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina Langu, Nami nipo papo hapo katikati yao.


123-011: USINIACHE NIPOTEE

 

Zaburi 119:10-11
Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo Yako. 11 Moyoni mwangu nimeliweka neno Lako, Nisije nikakutenda dhambi.


 

123-012: NAKUNGOJA MCHANA KUTWA

 

Zaburi 25:4-5
4 Ee Bwana, unijulishe njia Zako, Unifundishe mapito Yako, 5 Uniongoze katika kweli Yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.


 

123-013: DUA, SALA, NA MAOMBEZI

 

1 Timotheo 2:1
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; 2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. 3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; 4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.


 

123-014: AKAKESHA USIKU KUCHA

 

Luka 6:12
Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha katika kumwomba Mungu.