123: 001-007: Injili Ya Asubuhi

 

4-23-17: (001) MKIKAA NDANI YANGU

“Ninyi mkikaa ndani Yangu, na maneno Yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”  (Yohana 15:7)

 

4-24-17: (002) WAKATI UKUPENDEZAO

“Nami maombi yangu nakuomba Wewe, Bwana, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili Zako unijibu, Katika kweli ya wokovu Wako” (Zaburi 69:13)

 

4-25-17: (003) UJASIRI TULIO NAO KWAKE

“14 Na huu ndio ujasiri tulio nao Kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi Yake, atusikia. 15 Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”  (1 Yohana 5:14-15)

4-26-17: (004) OMBEA WANAOTESEKA

“4 Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu. 5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.”  (Matendo 12:4-5)

 

 

4-27-17: (005) OMBA KATIKA SHIDA

13 Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
14 Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.
15 Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.
16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.

 

 

4-28-17: (006)UYAANGALIE MATESO YANGU

153 Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria yako.
154 Unitetee na kunikomboa, Unihuishe sawasawa na ahadi yako.
155 Wokovu u mbali na wasio haki, Kwa maana hawajifunzi amri zako.

 

 

4-29-17: (007)NAMI NIKAOGOPA

1 Sala ya nabii Habakuki. 2 Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.(Habakuki 3:1-2)