Upendo uliopotoshwa

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi: April 06, 2017

SOMO: UPENDO ULIOPOTOSHWA

Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua” Zaburi 105:26.
Haruni alikuwa mtu mwenye hulka ya upole, ambaye Mungu alimchagua ili kusimama pamoja na Musa na kuzungumza kwa niaba yake

Mungu angeliweza kumchagua Haruni kama kiongozi; lakini Yeye afahamuye mioyo, ajuaye tabia, alitambua kuwa Haruni alikuwa mtu aliyekubali kushindwa kirahisi na alikosa ujasiri wa kimadili wa kusimama akiitetea haki katika mazingira yote, bila kujali matokeo.

Shauku ya Haruni ya kuwatendea watu mema waliyopenda wakati mwingine ilimfanya atende makosa makubwa

Hali hiyohiyo ya kukosa uthabiti wa kutenda mambo sahihi katika familia yake ilisababisha vifo vya wanawe wawili.

Nadabu na Abihu walishindwa kuheshimu amri ya Mungu ya kutoa moto mtakatifu katika vyetezo vyao na uvumba mbele Yake

Hapa kunaonekana matokeo ya nidhamu dhaifu. Kwa sababu wana hawa wa Haruni hawakuwa wameelimishwa kuheshimu na kustahi amri za baba yao, na kadiri walivyopuuzia mamlaka ya wazazi, hawakutambua umuhimu wa kufuata kwa uangalifu wote maagizo ya Mungu….

Tofauti na maelekezo bayana kutoka kwa Mungu, walimfedhehesha kwa kuwasha moto wa kawaida badala ya ule mtakatifu. Mungu aliwapatiliza kwa ghadhabu Yake: moto ukatoka hapo mbele Yake na kuwaangamiza wote wawili.

Haruni alibeba maumivu yake makali kwa uvumilivu na upole wa unyenyekevu. Huzuni na masumbuko makali sana yalishinikiza roho yake.

•Alisadikishwa juu ya upuuziaji wake wa wajibu.

•Alikuwa kuhani wa Mungu Mkuu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu wake.

•Alikuwa kuhani wa nyumba yake, hata hivyo ilikuwa rahisi kwake kutojali upuuzi wa watoto wake.

•Alikuwa amepuuzia wajibu wake wa kuwafundisha na kuwaelimisha katika utii, kujikana nafsi, na ustahivu kwa mamlaka ya wazazi.

•Kupitia kuruhusu mwenendo potofu, alishindwa kuzijengea tabia zao ustahivu wa juu kwa ajili ya mambo ya milele.

• Haruni hakuona, kama vile wasivyoona wazazi wengi Wakristo sasa, kwamba upendo wake uliopotoka na udekezaji wa watoto wake katika makosa ulikuwa ukiwaandaa kwa ajili ya ghadhabu ya Mungu ya hakika ….

•Malalamiko yake ya upole, bila kutumia kizuizi thabiti kama mzazi, na huruma yake kwa wanawe isiyo na busara vilikuwa ukatili uliopita kiasi.

REHEMA ZA BWANA NI MPYA KILA SIKU ASUBUHI , MAOMBOLEZO 3: 22-23