NZK#1: Umtakatifu

SAA YA IBADA NA MAOMBI

http://tgvs.org/archives/2502
NZK # 1: “Umtakatifu”
Jamii: Injili katika Nyimbo
Muda: Kila Alfajiri

 

Nyimbo Za Kikristo NZK # 1
MTAKATIFU, MTAKATIFU.

1
Umtakatifu! Mungu Mwenyezi!
Alfajiri sifa zako tutaimba;
Umtakatifu, Bwana wa huruma,
Mungu wa vyote hata milele.

2
Umtakatifu! Na malaika,
Wengi sana wanakuabudu wote;
Elfu na maelfu wanakusujudu;
Wa zamani na hata milele.

3
U mtakatifu! Ingawa giza,
Lakuficha fahari tusiione,
U mtakatifu! Wewe peke Yako;
Kamili kwa uwezo na pendo.


Isaya 57:15
“Maana Yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye Jina Lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa Mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu”.

 

CHANGAMOTO ZA KUOMBEA LEO
(1) Dada anayehitaji kukua kiroho
(2) Anayetafuta mwenzi wa maisha
(3) Radio Morning Star
(4) Ujazo wa Roho Mtakatifu.
(5) Upendo, Umoja, Msamaha.
(6) Huduma ya Sauti ya Injili
(7) Wana ATAPE huko Musoma
(8) Mtoto Daniel: anaumwa sana.

(9) Dada Penuel amefiwa na mama yake, upareni-kimanjaro: ombea faraja kwa wafiwa na wote wanaosafiri kuelekea mazikoni.

(10) “Wimbi la mauti”; “Simanzi isiyoelezeka”; katika shule ya “Changarawe Sekondari” huko Iringa- Mafinga. Wamepoteza waalimu wawili. Tuzidi kuwaombea.


 

TUFANYE NINI BASI NA KIPINDI HIKI?

(1) Weka Ombi (Audio/Text)
(2) Weka Ushuhuda
(3) Weka mahitaji Yako
(4) Weka wimbo wa Sifa
(5) Jikabidhi kwa Mungu wako sasa.

Mathayo 26:41
Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; Roho i radhi, lakini Mwili ni dhaifu.”

BWANA ATUBARIKI SOTE!