4-12-17: Ukuhani wa kifalme

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA

http://tgvs.org/archives/2489

  • Robo hii: Lisha Kondoo Zangu
  • Wiki hii: Ukuhani wa Kifalme (3/13)
  • Jamii: Kila Jioni

Fungu La Kukariri: (1 Petro 2:9)

  •  “Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu”.

OMBI: Baba yetu na Mungu wetu. Jina Lako litukuzwe milele. Asante Bwana kwa nafasi nyingine ya uhai. Asante kwa zawadi ya Neno Lako. Kabala ya kuanza kipindi hiki, tunaalika uwepo Wako, Bwana. Tunaomba Roho Mtakatifu, katika tafakari ya somo hili, atukirimie hekima ya utambuzi wa sauti Yako na nguvu ya kuitii. Tusaidie kufanya uamuzi wa busara kila wakati, kuachana na dhambi, tukikuchagua Wewe na kuuchagua wokovu. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tubadilishe ili tufanane Nawe. Bariki kila mmoja Bwana. Tunaomba na kuamini katika Jina la Yesu Kristo. Amina!


 

Jumatano: (4/12/17)

UKUHANI WA KIFALME

Katika kitabu cha Kutoka, sura ya 19, Bwana alisema kwa Musa: “Utawaambia nyumba ya Yakobo, na kuwaarifu wana wa Israeli, maneno haya; Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi. Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu, nanyi mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu.” (Kutoka 19:3-6)

Hapa kuna ujumbe wa injili, ukidhihirishwa milenia kadhaa kabla ya Msalaba: Mungu anawakomboa watu wake, akiwaokoa kutoka katika dhambi na utumwa wa dhambi, na ndipo anapowaamuru wampende na kumtii kama watu maalumu wa agano mbele yake na mbele ya ulimwengu.

Soma 1 Petro 2:5, 9, 10 na Kutoka 19:6. Petro anamaanisha nini anapowaita Wakristo kuwa ni “ukuhani wa kifalme” na “taifa takatifu” (1 Petro 2:9). Lugha hii inasema nini kwetu kama Wakristo Waadventista wa Sabato kuhusu wajibu wetu?

 

1 Petro 2:5, 9, 10

  • 5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo. 9 Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; 10 Ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Kutoka 19:6.

  • Nanyi mtakuwa Kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.

 

“Nyumba ya Roho,” “mzao mteule,” “ukuhani wa kifalme,” na “watu wa milki ya Mungu” yote ni maneno ya heshima ambayo katika Biblia huelezea uhusiano maalumu ambao Mungu alikuwa nao pamoja na uzao wa Ibrahimu. Sasa, katika muktadha wa Yesu na Msalaba, Petro anatumia lugha ile ile ya agano na kuitumia kwa ajili ya washiriki wa kanisa. Ahadi za agano zilizofanywa kwa ajili ya Israeli sasa zimepanuliwa ili kujumuisha si tu Wayahudi wanaomwamini Yesu bali pia waumini wa Mataifa. Ndiyo, kupitia kwa Yesu, Mataifa, pia, wanaweza kudai kuwa wana wa Ibrahimu. “Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.” (Wagalatia 3:29). Kupitia kwa Kristo, mtu ye yote, bila kujali kuzaliwa kwake, anaweza kuwa sehemu ya huu “ukuhani wa kifalme.”

 

Taifa takatifu? Ukuhani wa Kifalme? Kutumika kwa ajili yetu sisi, maneno kama haya yangemaanisha nini kuhusu aina ya maisha tunayoyaishi, kama mtu binafsi na kama jamii? Tunawezaje kuishi kulingana na wito huu mkuu?