20-003: Faida za Utii wa Sheria ya Mungu

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

 

USOMAJI WA BIBLIA KWA MPANGO

http://tgvs.org/archives/2456   

 • (a) 20-003: Faida za Utii wa Sheria
 • (b) Jamii: Kitabu cha Mithali
 • (c) Mfululizo: Sura kwa Sura

 

OMBI: Baba yetu wa Mbinguni tunakushukuru kwa zawadi nyingine ya uhai. Leo tunapofungua Neno Lako, tunasihi mwongozo wa Roho Wako. Baba, tusamehe, tusafishe, na kutuandaa kwa ajili ya marejeo Yako. Hebu sura hii ikapate kuwa mbaraka kwetu sote. Tunakushukuru na twaja katika Jina la Kristo, aliye Bwana na Mwokozi wetu, Amina.


 

MITHALI 3: (MUHTASARI WA SURA)

 1. Wahusika: Mungu, Sulemani, mwanawe
 2. Tabia ya Mungu: Hekima, Haki, Uaminifu
 3. Vitu katika kibiblia: Moyo
 4. Maneno ya kibiblia: Sheria, Imani, Ahadi
 5. Maeneo ya kibiblia: (Hakuna)
 6. Matukio ya kibiblia: (Hakuna)
 7. Fungu Kuu: Mithali 3:5-6
 8. Msisitizo: Sheria ya Mungu (2:8, 21-22)

 

MUHTASARI WA MAWAZO MAKUU:

 1. Utangulizi
 2. Sheria inayopendekezwa kwetu (Mithali 3:1 – 4)
 3. Sheria na Maisha yetu (Mithali 3:5 – 12)
  1. Suala la Imani yetu (3:5 – 6)
  2. Swali la Hazina yetu (3:7 – 10)
  3. Swali la Majaribu yetu (3:11 – 12)
 4. Utajirisho wa Sheria kwetu (Mithali 3:13 – 22)
  1. Uhakika wa Furaha (Mithali 3:13 – 15)
  2. Uhakika wa Afya (Mithali 3:16 – 17)
  3. Uhakika wa Mbingu (Mithali 3:18 – 22)
 5. Hitimisho
  1. Ombi kimungu (Mithali 3:21b)
  2. Ahadi takatifu (Mithali 3:22)
 6. Maswali Muhimu Katika Sura Hii
 7. Tufanye nini basi na Sura Hii?
 8. Sauti Ya Injili (Sauti ya Mungu kwako)

 

UTANGULIZI:

Sura hii ya tatu huanza na mwito sasa wa baba (Sulemani) kwa mwanawe (cf. Mithali 1:8, 10, 15; 2:1; 3:11, 21; 4:1, 10, 20, nk.). Sehemu ya ufunguzi wa sura hii (Mithali suara ya 1 – 12) lina msururu wa mashauri, kila kisha ikifuatiwa na zawadi zilizoahidiwa kwa wale ambao watazingatia. Hubiri/ nasaha ya kwanza imetolewa hapa, sababu ya kuitii inatajwa katika mstari wa 2 (Mithali 3:2)

Hatua muhimu/ masharti yanayotajwa hapa ni ‘sheria yangu’ na ‘amri zangu.’ ‘Sheria’ ni neno halisi la Kiebrania TORAH, ambalo mara nyingi linahusu Sheria Takatifu ya Mungu (k.m Mithali 29:18) na laweza kutumiwa kumaanisha torati nzima (PENTATEUCH); yaani, vitabu vitano vya Musa. Hata hivyo, hapa lina maana hasa kwa kile Sulemani anachotoa/ anachofundisha katika Mithali hizi (Kitabu cha Mithali) kama matumizi ya Sheria katika maisha ya kila siku (Mithali 1:8; 4:2; 6:20, 23). Tunaweza pia kutumia hii {neno Sheria} zaidi kwa ujumla kwa kile wazazi wanachofundisha watoto wao kuhusu jinsi ya kutumia Sheria ya Mungu katika maisha leo.

[John A. Kitchen, A Mentor Commentary, Proverbs 3] 


 

MITHALI SURA YA 3

1 Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu.

Tumizi la neno “Moyo”  katika Mithali 3:1 [DBL Hebrew]

4213 לֵב (lē): = MOYO

 1. MOYO: ogani ya kusukumia damu mwilini (Ps 38:11; Hos 13:8);
 2. KIFUA: kaviti ya Thorax ya kiumbe fulani (Ayubu 41:16);
 3. Moyo, Akili, Nafsi, Roho, Nafsi, yaani, chanzo cha maisha ya utu wa ndani katika nyanja mbalimbali, kwa kuzingatia hisia, mawazo, hiari, na maeneo mengine ya maisha ya ndani (Isaya 57:15; Muhubiri 2:1)

 

2 Maana zitakuongezea wingi wa siku. Na miaka ya uzima, na amani.

3 Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.

4 Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

7 Usiwe mwenye hekima machoni pako; Mche Bwana, ukajiepushe na uovu.

8 Itakuwa afya mwilini pako, Na mafuta mifupani mwako.

9 Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.

10 Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.

11 Mwanangu, usidharau kuadhibiwa na Bwana, Wala usione ni taabu kurudiwa naye.

12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe ampendezaye.

13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.

14 Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.

15 Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.

16 Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

17 Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.

18 Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.

19 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya nchi; Kwa akili zake akazifanya mbingu imara;

20 Kwa maarifa yake vilindi viligawanyika; Na mawingu yadondoza umande.

21 Mwanangu, yasiondoke haya machoni pako, Shika hekima kamili na busara.

22 Basi yatakuwa uzima kwa nafsi yako, Na neema shingoni mwako.

23 Ndipo utakapokwenda katika njia yako salama, Wala mguu wako hautakwaa.

24 Ulalapo hutaona hofu; Naam, utalala na usingizi wako utakuwa mtamu.

25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.

26 Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.

27 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.

28 Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe.

29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.

30 Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote.

31 Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake.

32 Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.

33 Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.

34 Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.

35 Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.


  

 

MASWALI MUHIMU KATIKA SURA HII

{Pitia majibu yaliyowekwa hapo chini}

 • Je, fundisho kuu ni nini hasa katika sura hii?
 • Je, kuna dhambi ya kuepukwa/ kutubu hapa?
 • Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
 • Je, kuna agizo au wajibu wa kufanya hapa?
 • Je, sura hii inatufundisha nini kuhusu Mungu?
 • Je, kuna dua/ ombi lolote la kuombwa hapa?
 • Je, kuna ahadi yoyote kwa ajili yangu hapa?
 • Je, sura hii ina umuhimu gani katika mpango wa wokovu wetu?

 

MAJIBU YA MASWALI MUHIMU:

MADA KUU? = “SHERIA YA MUNGU”

 • “Haikuwa rahisi kwa Myahudi na Agano la Kale kusahau Neno la Mungu. Yeye alikuwa analazimika kisheria kuandika mafungu ya Biblia juu ya miimo ya nyumba yake. Alopokuwa akiondoka nje, maandiko juu ya miimo ya milango yake yalimkumbusha: “unaenda wapi? Utakuwa nani? Swala gani gani linakutoa huko nje? Zingatia tabia/ mwendendo wako ukiwa huko. Linda mdomo/ mazungumzo yako. Zingalia tabia yako. Tii dhamiri yako. Kumbuka: Mungu kamwe halali. Aliporudi nyumbani mwake, maandiko juu ya miimo ya milango yake yalimuhoji: “Umekuwa kuwa? Umekuwa ukifanya nini?  Jichunguze mwenyewe. “Kamwe huwezi kutanga mbali na Mungu.” (John Phillips; Exploring Proverbs, Vol. 1)

 

Mithali 3:1: “Mwanangu, usiisahau sheria yangu, Bali moyo wako uzishike amri zangu”

SWALI: Je, inamaanisha nini “kutosahau sheria ya Mungu” katika Mithali 3:1

Kumsahau Mungu na Neno Lake si tu kupoteza kumbukumbu kuhusu Mungu, lakini ni:

 1. Kuishi katika hofu na ukosefu wa Imani (Isa 51:13),
 2. Kumpinga Mungu (Zab 106:13),
 3. Kupuuza amri Zake (Kum 8:11),
 4. Kwenda kwa miungu mingine (Kumbukumbu la Torati 8:19).

Tukumbuke kwamba tabia hii kwa kawaida kabisa hukua kutokana na  faraja ya kuridhika (Hosea 13:6).

Hosea 13:6 

 • Kwa kadiri ya malisho yao, kwa kadiri iyo hiyo walishiba; walishiba na moyo wao ukatukuka; ndiyo sababu wamenisahau Mimi. 

 

DHAMBI ILI KUEPUKA / KUKIRI?

 1. Kusahau Sheria ya Mungu (Mithali 3:1)
 2. Kuacha Rehema na Kweli (Mithali 3:3)
 3. KIBURI: Kutomtumini Bwana (Mithali 3:5)
 4. KIBURI: Kutojiwasilisha Chini Ya Mapenzi / Maelekezo / Mwongozo Yake (Mithali 3:6)
 5. KIBURI: Kuridhika na Hekima yetu wenyewe (Mithali 3:7a)
 6. KIBURI: Kutojiepushe na uovu. (Mithali 3:7b)
 7. UWAKILI: Kutomheshimu Bwana kwa mali yako. (Mithali 3:9)
 8. KIBURI: Kudharau/ kupuuza kukemewa/ kuridiwa na Bwana

 

SALA/ OMBI LA KUIGWA?

Mithali 3:5-6

 • 5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
 • 6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.

 

MTAZAMO KUIGWA?

 • (1) Maombi
 • (2) Ibada
 • (3) Kuheshimu / Kumuogopa Mungu
 • (4) Kutii Sheria Yake
 • (5) Kuamini katika Bwana
 • (6) Kupumzika katika ahadi za Mungu
 • (7) Kupumzika kwenye ulinzi wa Mungu kifani

 

MAAGIZO AU WAJIBU WA KUFANYA HAPA?

Mithali 3:25-31

 • 25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
 • 26 Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
 • 27 Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
 • 28 Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe.
 • 29 Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.
 • 30 Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote.
 • 31 Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake.

 

AHADI ZA MUNGU?

 1. Wingi wa siku; Maisha marefu, na amani (Mithali 3:2)
 2. Yeye atayanyosha mapito yako (Mithali 3:6)
 3. Mibaraka:Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya” (Mithali 3:10)
 4. Kwa Bwana atakuwa imani yako (Mithali 3:26)
 5. Uhakika wa Furaha (Mithali 3:13 – 15)
 6. Uhakika wa Afya (Mithali 3:16 – 17)
 7. Uhakika wa Mbingu (Mithali 3:18 – 22)
 8. Utakuwa mbaraka kwa wengine (Mithali 3:18)
 9. Ulinzi: Bali siri Yake ni pamoja na wanyofu (Mithali 3:32) But His secret counsel is with the upright. (NKJV)
 10. Ulinzi: Bali huibariki Maskani Ya Mwenye Haki.. (Mithali 3:33)
 11. Neema: Bali huwapa wanyenyekevu (Mithali 3:34)
 12. Tuzo Kuu Kiliko Tuzo Yoyote: MBINGU – Wenye hekima wataurithi utukufu (Mithali 3:35)

 

JE, SURA HII INATUFUNDISHA NINI KUHUSU MUNGU?

Katika sura hii tunakukutana na:

 • Mungu asiye na upendeleo. 
 • Mungu ambaye anachukia dhambi, lakini anapenda wenye dhambi. 
 • Mungu ambaye hudhihirisha kwa watoto Wake wote (wenye haki na wadhambi) kuhakiki Sheria, Mapenzi na Ahadi Zake; na kufanya maamuzi yenye hekima kumtii.

Tunaona Tabia ya Mungu: Uaminifu, Haki, Hekima

Aidha, tunaona:

 • Jinsi matendo ya Mungu katika kukabiliana na Uovu/ Maovu
 • Jinsi anavyoshughulika na wenye dhambi
 • Jinsi Yeye anayotamka laana juu ya nyumba ya waovu
 • Jinsi Mungu anavyoongea, anayojifunua Mwenyewe
 • Mapenzi Yake kwa wenye haki
 • Thawabu Kuu, kwa wale ambao hutembea katika unyofu mbele Zake.

Pia tunaona karama za kiungu kwa watu walio na sifa fulani: Utii, Unyenyekevu, Upole; Bwana atawajazi NEEMA YAKE juu yao.


 

 

JE, SURA HII INA UMUHIMU GANI KATIKA MPANGO WA WOKOVU WETU? 

Bwana atatoa tuzo ya mwisho kwa watiifu: MBINGU

 • Mithali 3:35
  • Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
 • 1 Samweli 2:30
  • Kwa sababu hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.
 • Zaburi 73:24 (NKJV)
  • Utaniongoza kwa shauri lako, Na baadaye utanikaribisha kwa utukufu. 

 

 

TUFANYE NINI BASI NA SURA HII?

Katika Hosea 4:6  Bwana anasema: “ Watu Wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, Mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu Mimi; kwa kuwa umeisahau Sheria ya Mungu Wako, Mimi nami nitawasahau watoto wako.”

 

Wapendwa:

 • Hebu tuitikie mwito wa sura hii na kuomba maarifa ya kimbingu.
 • Hebu tumkumbuke Mungu wetu kwa kumtii
 • Hebu tutii maelekezo yote ya  Baba yetu wa Mbinguni
 • Hebu tuombe Ulinzi, Hekima na Ufahamu wake.
 • Hebu tuzingatie Sheria Zake, na Mausia Yake

 

TAFAKARI MAFUNGU HAYA:

 • Mithali 1:8
  • Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, 
 • Mithali 4:5
  • Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu
 • Mithali 31: 5
  • Wasije wakanywa na kuisahau sheria, Na kuipotosha hukumu ya mtu aliye taabuni. 
 • Zaburi 119:93
  • Hata milele sitayasahau maagizo yako, Maana kwa hayo umenihuisha. 

 

 OMBI LA MTUNGA ZABURI

 • Zaburi 119:153
  • Uyaangalie mateso yangu, uniokoe, Maana sikuisahau sheria Yako.
 • Zaburi 119:176
  • Nimetanga-tanga kama kondoo aliyepotea; Umtafute mtumishi wako; Kwa maana sikuyasahau maagizo Yako.

 

 

SAUTI YA INJILI

[Hebu sikiliza sauti ya Mungu ikinena nasi, tunapofunga kipindi hiki]

 

Kumbukumbu la Torati 6:6 – 9 (NKJV)

 • 6 Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;
 • 7 Nawe uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena uketipo katika nyumba yako, na utembeapo njiani, na ulalapo, na uondokapo.
 • 8 Yafunge yawe dalili juu ya mkono wako, nayo yatakuwa kama utepe katikati ya macho yako.
 • 9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako. 

 

Kumbukumbu la Torati 4:23-24

 • 23 Jihadharini nafsi zenu, msije mkalisahau agano la Bwana, Mungu wenu, alilolifanya nanyi, mkajifanyia sanamu ya kuchonga, mfano wa umbo la kitu cho chote ulichokatazwa na Bwana, Mungu wenu; 24 kwa kuwa Bwana, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.  

 

OMBI: Baba Tunakuja mbele Zako tena. Katika sura hii tumeona utupu wetu, maana maadiko yamesema: “Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele Zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni Pake Yeye aliye na mambo yetu”. (Waebrania 4:12-13). 

Baada ya tafakari ya sura hii, Neno Lako limenichoma, na nimegundua kuwa  mimi ni mwenye dhambi mbele Zako; kwani, kuna mambo mengi hapa ambayo bado ninamapungufu kwayo. Tumekutenda dhambi Bwana, kwa maneno, mawazo, vitendo, kutotimiza wajibu, kwa kiburi chetu, n.k.  Kwa hivyo Bwana, tusamehe makosa yetu, ukatusafishe, ukatupe mwamsho wa kipekee; na kuendelea na kutufundisha kweli hizi za Biblia, tena na tena, kupitia Roho Wako.

Asante kwa ahadi Zako nyingi katika sura hii. Tusaidie Bwana, tusije isahau Sheria na Amri Yako. Tuongezee “wingi wa siku, na miaka ya uzima, na amani”. Utukirimie “Rehema na kweli” Zako;  zisifarakane nasi.

Zaidi ya yote Bwana, katika siku hii ya leo: tukumbushe “Kutumaini Bwana kwa mioyo yetu yote”, tusije tukathubutu “kutegemea akili zetu wenyewe”; na “KATIKA NJIA ZETU ZOTE TUKUKIRI WEWE”,  na ahadi njema ni kwamba “UTAYANYOSHA MAPITO YETU”.

Asante Bwana, na twaja katika Jina la Kristo Yesu, Amina!


 

Sauti ya Injili SDA © 2017