94-001 Kujiua

KIPINDI HEWANI SASA

KAYA & FAMILIA

Mada: KUJITOA MUHANGA/ KUJIUA
http://tgvs.org/archives/2360
94-001

 

SABABU ZA KISAIKOLOJIA ZA KUJIUA

Muhtasari Wa Mawazo Makuu:

(1) Hisia ya hatia/ dhambi inaweza pelekea kujitoa muhanga

(2) Kushindwa kunaweza pelekea kujitoa muhanga

(3) Kujilipiza Kisasi kunaweza pelekea kujitoa muhanga

(4) Dharau inaweza pelekea kujitoa muhanga

(5) Kushindwa kunaweza pelekea jaribio la kujitoa muhanga


 

HISIA YA HATIA

Mathayo 27 (Yuda)

3 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia.

4 Wakasema, Basi, haya yatupasani sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.

5 Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.

 

KUSHINDWA

1 Samweli 31: 4 (Sauli)

Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.
KUJILIPIZA KISASI

Waamuzi 16:26-30; (Samsoni)

26 Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.

Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.

28 Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
DHARAU

2 Samweli 17:23

Naye Ahithofeli alipoona ya kuwa shauri lake halikufuatwa, akatandika punda wake, akaondoka, akaenda nyumbani kwake, mjini mwake, akaitengeneza nyumba yake, akajisonga; akafa, akazikwa kaburini mwa babaye
KUKABILIWA NA HUKUMU KALI

Matendo 16:27 (mlinzi wa gereza)

Yule mlinzi wa gereza akaamka, naye alipoona ya kuwa milango ya gereza imefunguka, alifuta upanga, akataka kujiua, akidhani ya kuwa wafungwa wamekimbia.


 

MASWALI YA MJADALA.

(1) Tutafanyaje ili kuelemisha watu kuhusu dhambi ya kujiua?

(2) Utamsaidiaje yule anayetaka/ aliye na hisia za kutaka kujiua?

(3) Tutafanyaye katika familia zetu ili kuelemisha watoto/ vijana ili wasikumbwe na majaribu haya?

(4) Mafungu gani ya Biblia utatumia?
MWISHO.

(Karibuni kwa mjadala)