19-3-17 Usadikisho wa Dhambi

BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”

MWONGOZO WA KUJIFUNZA BIBLIA

http://tgvs.org/archives/2353  

 • Jamii: Kila Jioni
 • Muundo: Mjadala
 • Muda: Dakika 15-20

Somo la 12: Machi 18-24, 2017:  KAZI YA ROHO MTAKATIFU

Fungu la Kukariri: (Warumi 15:13) Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.

OMBI: Baba yetu mwema, tunasema asante kwa nafasi nyingine ya tafakari ya Neno Lako. Tunaalika Roho Wako atufundishe na kutuelekeza katika kweli yote. Tusamehe dhambi, uovu, kasoro, na mapungufu yetu yote. Hebu mmoja aguswe na injili hii, na kukata shauri kukutii, na kuachana na uovu. Tuandae kwa ajili ya marejeo Yako. Tumeomba haya katika Jina la Yesu Kristo, Amina.


 

Jumapili: Machi 19, 2017

USADIKISHO WA DHAMBI: (Conviction of Sin)

SWALI # 1. Soma Yohana 16:8-11.  Je, ni ipi kazi muhimu sana ambayo Roho Mtakatifu anaifanya kwa ajili yetu, na kwa nini hili ni muhimu sana?

Yohana 16:8-11;

 • 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
 • 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
 • 10 kwa habari ya haki, kwa sababu Mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
 • 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

Soma aya ya 1, 2.

 • “Yesu amemwita Roho Mtakatifu kuwa ni paraclete, neno lenye maana nyingi ambalo linawasilisha dhana ya msaidizi, mtetezi, na mfariji. Roho Mtakatifu haifanyi kazi hii muhimu ya usadikisho kama mshitaki wa ndugu au mwendesha mashitaka yetu. Hakutumwa na Yesu ili kutuhukumu bali, hata hivyo, kutusaidia kuona hitaji letu la neema.”
 • “Ni mfariji tu ndiye atakayepokelewa kama msaidizi. Ni jambo la kusikitisha sana kwamba Wakristo, hata wale wenye nia nzuri, mara nyingi huwaendea wadhambi kwa roho ya kushutumu badala ya ile ya kusaidia. Ikiwa tutaenda huku na kule tukionesha dhambi katika maisha ya watu wengine tukiwa na roho hii ya shutuma, hapo ndipo tunafanya kitu kingine ambacho Yesu hakutuita kufanya. Hata hivyo sisi ni akina nani hata tufichue dhambi katika maisha ya wengine wakati ambapo ni nadra sana kwamba sisi wenyewe si watu wasio na dhambi?”

 

SWALI # 2. Soma Warumi 2:1 na Mathayo 7:3. Ni ujumbe gani ambao lazima tuuchukue kutoka kwenye mafungu haya ya Maandiko?

 • Warumi 2:1
  • Kwa hiyo, wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru; kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.
 • Mathayo 7:3
  • Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii?

 

Soma aya ya 3,4,5,6

 • “Sisi tu mashahidi wake, na siyo washitaki wake. Tunaitwa kuwa mashahidi wa uweza wake wa ukombozi, na si kuwahukumu wengine kwa sababu ya makosa yao. Katika kujaribu kuwasadikisha watu wengine juu ya dhambi zao, tunakuwa tunafanya kazi isiyo yetu; ni kazi ya Roho Mtakatifu.”
 • “Ni Yule Mfariji—na wala siyo sisi—Ndiye ambaye “atauhakikisha” ulimwengu juu ya maana hasa ya dhambi. Watu ambao hawajayakabidhi maisha yao kwa Yesu mara nyingi hawatambui hasa maana halisi ya dhambi, na jinsi inavyoweza kuleta uangamivu.”
 • “Wazo hapa si kwamba Roho ataorodhesha matendo maalumu maovu. Badala yake, anakwenda katika dhambi ya msingi kabisa miongoni mwa yote: kutomwamini Yesu Kristo (Yn. 16:9). Hali yetu mbaya kabisa ya taabu na kutengwa haipo katika upungufu wa kimaadili, bali katika uadui na Mungu na kukataa kwetu kumkubali Yule ambaye Mungu amemtuma kwa lengo la kutuokoa kutoka kwenye hali hii.”
 • “Tatizo la msingi kabisa la dhambi zote ni kuwa hatuamini katika Yesu na, kwa hiyo, tunakataa Yeye pekee ambaye anaweza kutuokoa kutoka katika dhambi na hatia yetu. Hii ni dhambi inayoweka nafsi kuwa kiini cha mambo na hukataa kuliamini Neno la Mungu. Ni Roho Mtakatifu pekee ndiye anayeweza kuifungua mioyo na akili zetu ili kutambua hitaji letu kuu la toba na la Ukombozi ambalo hupatikana kupitia mauti ya Kristo kwa niaba yetu.”

 

MASWALI MUHIMU KATIKA SOMO LA LEO

(Rejea majibu yaliyotolewa hapo chini)

 1. Je, fundisho kuu la leo ni nini hasa?
 2. Je, kuna dhambi ya kuepukwa hapa?
 3. Je, kuna ombi la kuomba hapa?
 4. Je, kuna mtazamo wa kuigwa hapa?
 5. Je, kuna agizo au wajibu wowote?
 6. Je, kuna makosa ya kuepukwa hapa?
 7. Je, somo linasema nini kuhusu Mungu?
 8. Tufanye nini basi na somo la leo?

 

MAJIBU YA MASWALI MUHIMU:

 • Kazi ya Roho Mtakatifu kuusadikisha ulimwengu “kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.”
 • Dhambi ya kutomwamini Yesu kama Kristo (Masihi) na Mwana wa Mungu. Lakini pia, neno “DHAMBI” [μαρτία (hamartia)], lililotumika katika Yohana 16:9  lipo katika “umoja” likimaanisha  mtazamo wa dhambi mahsusi; pengine inaweza ikawa: uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo.
 • Ee Bwana, nisaidie niweze kumtii na kumwamini kama Yesu kama KRISTO (Masihi) na Mwana wa Mungu.
 • Mshukuru Mungu kwa zawadi kuu tuliyopatiwa: Roho Mtakatifu {paraclete}, msaidizi, mtetezi, na mfariji wetu. Elewa kwamba Yeye yupo kwa ajili yetu, si kutuhukumu, bali kutuelekeza kwa Baba, kutuwezesha “kumfikilia Mungu wetu” (cf. mwendelezo wa masomo yetu ya asubuhi)
 • (Yohana 16:13-14) 13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari.
 • ANGALIA Jibu # 02 (hapo juu)
 • Tabia ya Mungu: Upendo, Uaminifu, Utakatifu, na Uwezo Wake wa utambuzi wa fikra, nia na matendo yetu maovu. Lakini zaidi ya yote, uwezo Wake wa kutuokoa na hila za mwovu shetani.

 

TUFANYE NINI BASI NA SOMO LA LEO?

 • Zingatia tena Kazi ya Roho Mtakatifu (Fungu kuu)
 • Zingatia Umuhimu wa Kristo Yesu
 • Zingatia hukumu ijayo
 • Mruhusu Roho Wake akayatawale maisha yako

 

1 Yohana 5:12: Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima.

Yohana 16:8-11

 • 8 Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
 • 9 Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
 • 10 kwa habari ya haki, kwa sababu Mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
 • 11 kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.

 

SAUTI YA INJILI

Yohana 16:13-14

13 Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. 14 Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo Yangu na kuwapasha habari.

Warumi 8:13-14;

13 Kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.  14 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

 

MWITO WA LEO:

Wagalatia 5:25

“Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho.”

 

OMBI: Baba yetu mwema, tunasema asante sana kwa somo la leo. Tunaomba utusamehe dhambi, makosa, uovu na kasoro zetu zote. Roho wako anaponena nasi, tunaomba ikapate kutusadikisha kwa habari ya dhambi, haki, na hukumu ijayo. Tusaidie tuwe na “kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wetu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze”. Tusaidie tuwe “hodari, tupige moyo konde, sisi sote tunaomngoja Bwana, (Zaburi 31:24)”. Kaa pamoja na kila mmoja wetu, hadi hapo tena tutakapo kutana tena hapa kuzifunza Neno lako. Tumeomba haya tukiamini kuwa umesikia na utatenda kulingana na mapenzi Yako; ni katika Jina la Yesu Kristo, Amina.


 

The Gospel’s Voice © 2017